Rais Samia tafadhali soma hapa na ujumbe ukufikie

Bila kufanya machafuko tutaishia kwenye hizi lugha ngumu na hakuna lolote tutafanya. Wenzetu wataendelea kula tozo zetu na tutaishia kulialia tu.
Tukifanya machafuko tutakimbilia wapi?.
Tutumie njia za amani kushinikiza mabadikiko katika serikali,pamoja na katiba mpya.
 
Hali ya ufisadi ilivyo sasa Tanzania ni mbaya kuwahi kutokea.
Ni kama vile Nchi haina Kiongozi.
Pesa zinapigwa kila inayoitwa leo, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
 

Mkuu

Nikupe pongeze kwa kukaa chini na kutumia Muda na akili yako vizuri kujenga hoja hizi.

Unaongea kwa uchungu Sana, ni vijana wachache Sana wenye DNA ya kujenga hoja ngumu kiasi hiki..

Naomba nichangie kwa uchache Sana kipengele namba tano.

Kwenye kipengele hicho, uliyoyazungumza itakuwa ngumu kwake kuyatekeleza kwasababu moja kwa moja atapoteza Sifa ya kuwa hapo alipo kwa Sasa.

Vilevile, kwenye kipengele hicho tajwa, CCM inaenda kupoteza nafasi kwasababu ya lile pingamizi la Matokeo ya Uchaguzi Mahakamani. Labda pafanyiwe marekebisho hapo.

Kama ningekuwa Ps wake bs ningemshauri alete hicho tajwa halafu apumzike zake, jamii ya Watanzania wangemuimba kila siku na siyo tu kuwapa watoto wao nomino yake.

Hitimisho, naomba niitimishe kwa kusema kwamba ile njia ya kwenda kwenye maendeleo siyo njia nyepesi. Ni ngumu yenye gizo zito ambalo unahitaji ujasiri ( Guts) kwa kufanya maamuzi mazito ( bold decisions) kwa maslahi ya Taifa hili.

Muda utasema!

Asante!
 
Tanzania ni shamba la bibi. Kila mwenye uwezo wa kuvuna, anajivunia tu mchana kweupe! Na hakuna wa kumzuia.
 
Tatizo hao marope na yule wa Korosho ndio MASTERMIND wake wa 2025.
 
Watanzania ukiwanongoneza tu jambo wanavyojua kutiririka nalo hatari sana!
 
Wakati mwingine mnaweza kuharibu, mkaharibu jumla kama ilivyo Somalia na Libya. Bora tuendelee na umaskini wetu kwenye amani, kuliko kutafuta utajiri kwa kuanzisha vurugu!
Mbona Kenya hapo haijaharibika? Wazee ndio mnapandikiza woga kwakuwa mnafaidika na mfumo uliopo.
 
Na hapa nilipo umeme umekatika
Yaani Kuna vitu unashangaa sijui kwanini vinafanyika kwa nchi yetu Hadi unahisi huenda tumelaaniwa.

Kuna kipindi fulani nilikuwa Norway for two years kimasomo. Hata siku moja sikuwahi kuona umeme umekatika.

Kilichonishangaza: mwaka mmoja baadae, nikiwa nchini uholanzi nikapokea email kutoka Norway kuwa niwatumie akaunti namba yangu ya benk Ili wanirudishie kiasi Cha pesa ambacho nilikatwa kimakosa katika matumizi ya umeme ( yaani nilikuwa nalipia chumba/ rent including water and electricity), Sasa ikaonekana kwa kipindi chote nilichokaa bill ya umeme ilichajiwa zaidi ya ilivyotakiwa kukatea na hayo makosa yalifanyika na kampuni ilivyokuwa inahisika na umeme.

Nakumbuka ilikuwa almost 1.8 mill Tz shillings niliyorudishiwa. Hii ni habari ya kweli kabisa.

Tanzania tuna safari ndefu sana. Tunahitaji viongozi wenye maono na huruma kwa watanzania walio wengi. Shida iliopo viongozi wengi wapo kwa ajili ya maslahi binafsi na ufisadi.

By the way, ndoto yangu ipo pale pale, besides dark side of JPM, Mungu akinijalia kuwa Rais wa nchi hii by 2030s, watanzania hawatoamini jinsi nitakavyo watumikia kwa kuondoa huu uozo uliopo.

Ifike wakati tuseme hii nchi ni ya watanzania na sio ya wachache wanao ona kuwa ndio Wana hati miliki na nchi hii.
 
Mtoa mada pongezi zako nyingi huu ukumbusho utamfikia Mh Raisi bila shaka atapata kutafakari zaidi dhidi ya nafasi yake Kwa Tanzania , Kwa kuongezea hapo
. Mh Raisi amezungukwa na watu wanao amini katika sifa ndiyo Mambo yaende na Hilo yupo kulichekea sana kama vikundi vya chawa n.k abalishe mfumo kwani chama Kiko na watu wa kukisemea Kwa nafasi zao na zaidi ukifanya Jambo Kwa vitendo kila mtu ataona bila hata ya kutumia nguvu hapa kunafanya akiletewa/kuambiwa orodha ya wabadhilifu anajikuta wanaomsifia wamo hivyo anapata kigugumizi na kubakia yeye kwenye mngojeo wa fedhea toka kwa wananchi .
.Atambue mtu pekee wa mwisho kuulizwa juu ya hatma ya nchi ni yeye Kwa wakati huu kisha ayadhoofishe makundi yote ili awe na nguvu ya kuogelea kwenye nafasi yake aige Kwa mtangulizi wake jinsi alivyowanyoosha vigogo Hadi wakawa ruler ni vile Tu na yeye mfumo wa ubadhilifu ndiko alipokulia lakini tofauti na hapo tungeona mazuri zaidi ya aliyotuachia.
Mh Raisi fumbua macho regacy haiji kirahisi na udhalili ni m'baya sana.
 
Kufeli Kwa mama ni hukumu Kwa wanawake wote Tanzania Kwa kuonekana hawawezi kumudu nafasi ya urais tumwombee afanye maamuzi magumu
Ukituo wabunge wa Ccm wanaosifia kila kitu na kuuanza kuwalaum wateule wake kila mtu anajua mama hapo alipo tumepigwa na kitu kizito kichwani
 
Hakika inasikitisha sana na ukiangalia sana shida ni viongozi nakuombea heri ndoto yako itimie hofu ya Mungu ikuongoze kuokoa Taifa hili maana kila muda unavyokwenda na shida zinaongezeka .

Na ukisikia experience hiyo ya nchi za wenzetu unaweza ukaona kama tumelaniwa kwa kweli
 
Kwanchi kama yetu hii,jukumu hilo tumuachie Hakimu wama Hakimu.
INSHA_ALLAH.
 
Kurudisha watu kama Rishad Bade, Mafuru, Mbarawa,Makamba,Nape

Ilipendeza hata kama akuhitaji kuwa na wale wa hayati angechukua wake siyo wa JK au JPM
 
Kwenye kampeni yako ya urais nitajitolea lakini sharti moja tu.
FOR THE PEOPLE
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…