Rais Samia: Tanzania haitajengwa na chama kimoja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1649232545815.png

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania haitajengwa na mtu mmoja au chama kimoja bali itajengwa na Watanzania wote.

Rais Samia ameeleza hayo Jumanne Aprili 5, 2022 Jijini Dodoma wakati akizindua mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), unaojadili maridhiano, haki na amani.

“Tulichagua kuingia mfumo huu wa vyama vingi tukijua kwamba ndani ya mfumo huu tutakwenda kupata maendelo ya haraka kwa sababu vyama viko vingi, macho yako mengi, maono yapo mengi wanavyoona chama kimoja ambacho kipo ndani ya serikali pengine hawatokuwa na macho makubwa ya kuona kama wengine walio nje ya Serikali, na ndio maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendelea ndani ya Serikali na kutoa maoni yao, jamani hivi tunakwenda hivi, lakini mbona mmh, mbona tunaona hivi, mbona sheria hii ingebadilishwa hivi, mbona sera hii tungekaa tukazungumza hivi.

“Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania.

"Tukikubaliana, tunakwenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosaji, awe ametoka kokote kule kwa sababu tulijadiliana na kukubaliana tunaiweka hivi na hiyo ndio itakayokwenda kutuongoza katika utendaji wetu na maisha yetu kwanza ushirikishwaji kutoka serikalini ni uhakika “ Rais Samia Suluhu Hassan
 
"Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania.

HAONI KUWA HAPO ANAMANISHA TUTENGENEZE KATIBA?
AU ANAOGOPA KUTAJA NENO KATIBA MPYA?AU HAJUI ASEMACHO?
 
Maneno matupu hayavunji mfupa. Hayo Maneno kina Kizito kabwela wanayapenda sana.
 
Ushauri wa bure kwa serikali na CCM. Umefika wakati wa kukiandaa chama mbadala cha kuwapokea mzigo.

Wananchi wanapaswa waandaliwe kutawaliwa na chama mbadala, chenye sifa na kinachokubalika kwa wananchi.

Hii itaisaidia nchi kuona uwezo wa vyama mbadala, na kama faida zipo za kubadili sera kwa kipindi fulani kwa maslahi mapana ya taifa.

Wasipofanya hivyo, na kusubiri watolewe kwa nguvu ya umma, basi wajiandae kuingizwa kwenye makumbusho ya taifa.
 
"Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania.
"Tukikubaliana, tunakwenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosaji, awe ametoka kokote kule kwa sababu tulijadiliana na kukubaliana tunaiweka hivi na hiyo ndio itakayokwenda kutuongoza katika utendaji wetu na maisha yetu kwanza ushirikishwaji kutoka serikalini ni uhakika “ Rais Samia Suluhu Hassan

HAONI KUWA HAPO ANAMANISHA TUTENGENEZE KATIBA?
AU ANAOGOPA KUTAJA NENO KATIBA MPYA?AU HAJUI ASEMACHO?
Bado hajajitambua au hajaweka vipaumbele vyake. Anajaribu kina cha maji aone kama akiingia hayatamsomba.
 
"Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania.
"Tukikubaliana, tunakwenda kutekeleza wote kama Watanzania. Atakayekiuka hapo ni mkosaji, awe ametoka kokote kule kwa sababu tulijadiliana na kukubaliana tunaiweka hivi na hiyo ndio itakayokwenda kutuongoza katika utendaji wetu na maisha yetu kwanza ushirikishwaji kutoka serikalini ni uhakika “ Rais Samia Suluhu Hassan

HAONI KUWA HAPO ANAMANISHA TUTENGENEZE KATIBA?
AU ANAOGOPA KUTAJA NENO KATIBA MPYA?AU HAJUI ASEMACHO?
Katiba itakuphila,kila ukijamba Katiba,ukigeuka Katiba...Katiba siyo mzizi wa matatizo ya nchi
 
Usimuamini mwanasiasa, kamwe...
 
Back
Top Bottom