Rais Samia: Tanzania haitajengwa na chama kimoja

Rais Samia: Tanzania haitajengwa na chama kimoja

Huyu mama anaelewa sana umuhimu wa katiba mpya.
Kama mkikumbuka wakati amepewa nafasi 2016 wakati walipokuwa wanawashukuru waandishi na wasanii kwa kuwasaidia kuingia ikulu, alizungumzia mchakato wa katiba mpya japokuwa mwenzie hakuipa nafasi kabisa.
Kinachomfanya kuwa na kigugumizi kuanzisha mchakato ni mazingira yaliyomuingiza kwenye urais. Kama angekuwa ameingia kwa kupigiwa kura moja kwa moja,na siyo kama mgombea mwenza naamini angeisha anzisha mchakato wa katiba mpya.
Kipindi anakuwa muoga akijua upinzani alionao ndani ya chama chake na wa vyama vya upinzani. Anajua katiba hii inampa mlango wa kuchaguliwa kirahisi,kwa kutumia mbinu walizozitumia huko nyuma,ndio sababu anaongelea katiba mpya ni baada ya 2025.
 
Hata walivyotangaza kuwa bunge litaanza kuoneshwa live,

Kiukweli kwa hali ya sasa ambapo hakuna wabunge kupitia vyama vya upinzani mvuto wa kufuatilia na kusikiliza mijadala ya bunge umeondoka!

Mwamko wa kufuatilia mijadala ya bunge hakuna tena hata wakirudisha bunge mubashara.

Sababu ya kukosekana Kwa wabunge wa vyama vingine.

Bunge la wabunge wanaotokana na chama kimoja tu hupooza sana na kuondoa hamasa ya kusikiliza.
 
Back
Top Bottom