Rais Samia: Tanzania inakusudia kuandaa Mashindano ya AFCON 2027. Viwanja 3 vipya kujengwa

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Nawasalimu Wapenzi wote wa Michezo Tanzania kwa jina la JMT..

Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa Rais Samia kuupiga mwingi, amesema Serikali yake inajipanga na kujiandaa kwa ajili ya kuomba kuandaa na kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027.

Hayo yamesemwa na Rais Samia wakati akipokea Kombe la Dunia na kuwataka Viongozi wa Michezo na wengine kwenye sekta mbalimbali wajiandae Ili kufanikisha Nia hiyo.

Aidha, Rais Samia amesema inahitajika walau viwanja vikubwa vingine kama 3 hivi Ili kufanya jumla ya viwanja vyenye hadhi vipatavyo 6.

Mimi kama mdau wa Michezo naunga mkono wazo hili la Serikali na Kwa hiyo kuanzia mwaka huu waanze kutenga pesa za kujenga viwanja na miundombinu mingine.

Napendekeza Viwanja hivyo vipya na training grounds vijengwe kwenye miji ifuatayo;

1. Dodoma-Seating Capacity 80,000-100,000

2. Mbeya -Seating Capacity 50,000-60,000

3. Arusha- Seating Capacity 40,000-50,000

4. Unguja/Zanzibar- Seating Capacity 20,000-40,000

Aidha, Serikali ifanye maboresho makubwa katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza, Uhuru Dar es Salaam na Jamhuri Morogoro Ili miji hiyo pamoja na viwanja vipya vitakavyojengwa iweze kuandaa Mashindano kwa pamoja.

Kazi iendelee👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220606-143748.png
    122.4 KB · Views: 22
  • Screenshot_20220606-142738.png
    106.4 KB · Views: 22
  • Screenshot_20220606-142556.png
    114 KB · Views: 23
Ujenge uwanja huko mbeya porini..? Kama ni viwanja kujengwa hapo wajenge kiwanja kimoja mwanza, arusha na Tanga basi
 
Ujenge uwanja huko mbeya porini..? Kama ni viwanja kujengwa hapo wajenge kiwanja kimoja mwanza, arusha na Tanga basi
Kutoka Dar hadi Mbeya ni km? Vs Kutoka Dar hadi Mwanza? Wapi porini?

Huko Usukumani kungekuwa mjini si mungekuwa na timu japo moja Ligi Kuu?
 
Kutoka Dar hadi Mbeya ni km? Vs Kutoka Dar hadi Mwanza? Wapi porini?

Huko Usukumani kungekuwa mjini si mungekuwa na timu japo moja Ligi Kuu?
Tunaangakia uhitaji. Mbeya hapana aisee. Mwanza kuna miundo mbinu tayari. Mfano uwanja wa ndege mkubwa na hoteli nyingi nzuri nzuri. Sasa huko mbeya mmmh
 
Tunaangakia uhitaji. Mbeya hapana aisee. Mwanza kuna miundo mbinu tayari. Mfano uwanja wa ndege mkubwa na hoteli nyingi nzuri nzuri. Sasa huko mbeya mmmh
Wewe ni mpumbavu,uhitaji wa nini labda?

Kungekuwa hakuna uhitaji timu 3 Ligi Kuu,timu 3 Championship,timu 3 Second Division..Hapo wapi kuna uhitaji sasa?
 
Wewe ni mpumbavu,uhitaji wa nini labda?

Kungekuwa hakuna uhitaji timu 3 Ligi Kuu,timu 3 Championship,timu 3 Second Division..Hapo wapi kuna uhitaji sasa?
Kuwa na timu tatu ligi kuu sio tatizo. Afu jifunze kujitambua mm sio mpumbavu mpuuzi wewe. Hizo timu basi zijijengee viwanja vyao. Viwanja vitakavyo jengwa na serikali sio mali ya vilabu hivyo. Tumia akili yalo vzr? Huna hoja afu unatukana watu.
 
Kuwa na timu tatu ligi kuu sio tatizo. Afu jifunze kujitambua mm sio mpumbavu mpuuzi wewe. Hizo timu basi zijijemgee viwanja vyao. Viwanja vutakavyo jengwa na serikali sio mali ya vilabu hivyo. Tumia akili yalo vzr? Huna hoja afu unatukana watu.
Wewe ni zwawa kabisa,unabisha vitu genuine..

Uhitaji kwako ni upi? Na huo uhitaji uko Mwanza ila Mbeya hakuna au?

Nani aliyesema kiwanja kitakuwa mali ya timu? Wapi serikali itapata mapato mengi kwenye timu au ambako viwanja vinakaa bure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…