Rais Samia: Tanzania inakusudia kuandaa Mashindano ya AFCON 2027. Viwanja 3 vipya kujengwa

Rais Samia: Tanzania inakusudia kuandaa Mashindano ya AFCON 2027. Viwanja 3 vipya kujengwa

Ipo miji ambayo ina hivyo vitu kwa udogo toka kitambo na ina utalii ndani yake na mazingira yake yana ruhusu tatizo haisemwi. Mfano Tanga ni mji ambao hautajwi kwenye vitu kama hivi lakini ni mji ambao ungesimamiwa vzr naimani ungekua karibu na ilivyo dar.
Nakubaliana na wewe mkuu.
Lakini, Tanzania imebahatika kwenye vivutio,karibu mikoa yote ina vivutio.
Hizi shughuli za kimataifa zinatakiwa ziwahamasishe wawekezaji wa ndani na nje wakishikwa mkono na serikali,kwenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo bado hayajaamka. Rejea stand za mabus zilizo jengwa nje ya maeneo yaliyo changamka, wafanyabiashara wamezifuata zilipo.

Kama ni kiwanja kikubwa cha mpira hata Mtwara au Kigoma kinaweza kujengwa na kikaenda sambamba na ujenzi wa miundombinu husika, lakini kung'ang'ania kila kitu kiwe miji fulani matokeo yake ni watu kujazana kwenye hiyo miji huku mingine ikibaki miji mfu
 
Zile gari / mabasi ya Umeme yenyewe ni mwaka gani ?

Kukusudia kuandaaa na ku-bid ili kuandaa na kupewa uandaaji are different ball games
 
Nakubaliana na wewe mkuu.
Lakini, Tanzania imebahatika kwenye vivutio,karibu mikoa yote ina vivutio.
Hizi shughuli za kimataifa zinatakiwa ziwahamasishe wawekezaji wa ndani na nje wakishikwa mkono na serikali,kwenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo bado hayajaamka. Rejea stand za mabus zilizo jengwa nje ya maeneo yaliyo changamka, wafanyabiashara wamezifuata zilipo.

Kama ni kiwanja kikubwa cha mpira hata Mtwara au Kigoma kinaweza kujengwa na kikaenda sambamba na ujenzi wa miundombinu husika, lakini kung'ang'ania kila kitu kiwe miji fulani matokeo yake ni watu kujazana kwenye hiyo miji huku mingine ikibaki miji mfu
Vizuri mkuu. Sasa kwa idadi ya viwanja vitatu miji gani kwako wewe kwa sasa unapendekeza.?
 
Vile viwanja vya chama vinakarabatiwa na chama au serikali? Nikipata jibu namimi nitapata pakuchangia
 
Mkuu mm.sio sukuma gang mm ni mtu wa kaskazini na sina hata chembe ya sukuma gang. Na siwapendi hao sukuma gang ila napenda kusimamia usawa kwa kuangalia uhitaji uliopo.
Sukuma gang ni itikadi iliyoasisiwa na Wasukuma wa Mwendazake
 
Tanga kuna utalii milima ya Usambara, Barabara zipo vizuri, Bandari ipo,Usafiri upo ambao una kidhi viwango....Mama afikirie Tanga (Coastland)
 
Pamoja na kuwa serekali imeahid kujenga pia vilabu navyo viwe na malengo hayo Kama simba na yanga wanapaswa kuwa na viwanja vyao
 
Nawasalimu Wapenzi wote wa Michezo Tanzania kwa jina la JMT..

Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa Rais Samia kuupiga mwingi, amesema Serikali yake inajipanga na kujiandaa kwa ajili ya kuomba kuandaa na kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027.

Hayo yamesemwa na Rais Samia wakati akipokea Kombe la Dunia na kuwataka Viongozi wa Michezo na wengine kwenye sekta mbalimbali wajiandae Ili kufanikisha Nia hiyo.

Aidha, Rais Samia amesema inahitajika walau viwanja vikubwa vingine kama 3 hivi Ili kufanya jumla ya viwanja vyenye hadhi vipatavyo 6.

Mimi kama mdau wa Michezo naunga mkono wazo hili la Serikali na Kwa hiyo kuanzia mwaka huu waanze kutenga pesa za kujenga viwanja na miundombinu mingine.

Napendekeza Viwanja hivyo vipya na training grounds vijengwe kwenye miji ifuatayo;

1. Dodoma-Seating Capacity 80,000-100,000

2. Mbeya -Seating Capacity 50,000-60,000

3. Arusha- Seating Capacity 40,000-50,000

4. Unguja/Zanzibar- Seating Capacity 20,000-40,000

Aidha, Serikali ifanye maboresho makubwa katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza, Uhuru Dar es Salaam na Jamhuri Morogoro Ili miji hiyo pamoja na viwanja vipya vitakavyojengwa iweze kuandaa Mashindano kwa pamoja.

Kazi iendelee
Atakuwa Alikuwa anaigiza Royo Tua... au labda kuna mkopo anafukuzia...
 
Tunahitaji watoto wawe wanafundishwa michezo sana kutegemea na vipaji vyao na michezo wanayoipenda

Tatizo hatuwekezi sana kwenye michezo
Yaani Olympic tunaishia kupeperushiwa bendera tu
 
Mleta uzi ni mshamba uache kujenga Tanga ukajenge kwa ujinga wako sijui Arusha na mbeya Kama hujui soka kaa utulize kibox manyoya
 
Wewe ni mpumbavu,uhitaji wa nini labda?

Kungekuwa hakuna uhitaji timu 3 Ligi Kuu,timu 3 Championship,timu 3 Second Division..Hapo wapi kuna uhitaji sasa?
Timu zipi kelele kibao kwa kipi mlicho nacho kaeni porini unyakyusa mwingi ushamba tu
 
Nakubaliana na wewe mkuu.
Lakini, Tanzania imebahatika kwenye vivutio,karibu mikoa yote ina vivutio.
Hizi shughuli za kimataifa zinatakiwa ziwahamasishe wawekezaji wa ndani na nje wakishikwa mkono na serikali,kwenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo bado hayajaamka. Rejea stand za mabus zilizo jengwa nje ya maeneo yaliyo changamka, wafanyabiashara wamezifuata zilipo.

Kama ni kiwanja kikubwa cha mpira hata Mtwara au Kigoma kinaweza kujengwa na kikaenda sambamba na ujenzi wa miundombinu husika, lakini kung'ang'ania kila kitu kiwe miji fulani matokeo yake ni watu kujazana kwenye hiyo miji huku mingine ikibaki miji mfu
Mzeya lazima uangalie pia baada ya mashindano hayo mahotel kweli watu wataenda. Five star hotel ukajenge lindi sii majanga hayo
 
Back
Top Bottom