#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

“Tanzania tuna wagonjwa wa wimbi la Tatu la Corona. Hili jambo bado lipo, tuchukue hadhari zote na tunawaomba viongozi wa dini mseme hili kwa sauti kubwa"

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na baraza la maaskofu katoliki (TEC) #Tanzania #COVID19

=========

Rais Samia Suluhu: Wahashamu, baba Maaskofu kama mnavyofahamu, dunia kwasasa inakabiliwa na mlipuko wa Covid-19 na nafahamu kanisa tangu mwanzo limekuwa na msimamo Thabit katika kupambana na ugonjwa huu hivyo basi niwaombe sana Maaskofu msisahau kuwakumbusha waumini kuhusu wa kujikinga na kuchukua Tahadhari zote zinazoelekewa na wataalam wa Afya dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kwakuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba, tusiache kutumia kila kitakachotukinga na maradhi haya ili kuepesha vifo vya makundi.

Kama tunavyojua, duniani sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia, limekwenda limepungua kidogo, tumeingia wimbi la pili tumekwenda nalo na sasa kuna wimbi la tatu.

Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika kwenye wimbi hili la Tatu.

Kama mnakumbuka siku nilitembelea hospitali ya Mwananyamala, kuna wodi daktari mfawidhi alikuwa ananiingiza akaniambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, nikamwambia hebu kuwa muwazi, ni covid, akaniambia ndio Covid wakati wapiga picha wangu tayari wameshatangulia, nikawaambia nyie tokeni haraka huko.

Kwahiyo ni kusema kwamba hili jambo bado lipo, tusijiche, bado lipo tuchukue hadhari zote na tunawaomba sana viongozi wa Dini mliseme hili kwa sauti kubwa, kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi.

Pamoja na yote hato, ni vyema pia tumuombe Mungu kwa kiasi kikubwa aendelee kutuepusha na kutupa hifadhi yake kutokana na maradhi hasa Janga hili la Corona kwakuwa yeye ndio Muweza wa Yote.



Ujumbe kuntu kutokea kwa rais wetu kipenzi Mama Samia rais wa JMT.
 
Si ndio kasema hivyo? Ama unataka avue waliovaa barakoa kwa nguvu kama yule kichaa?
Mwambie afunge nchi! Akataze mikusanyiko, kusafiri na afunge hata ibada, mwenzio museven kafanya hivyo ndio nlichkuwa namaanisha sasa wewe kwakuwa bado una mimba ya yule kichaa basi kila kitu lazima umuhusishe!

Wanawake wengine mna shida hasa mkiwa wajawazito
 
Asante kwa matusi. Ndicho ulichobakiza tu hicho. Tutafika huko tu kama ndio maombi yako. Wengine tunaomba Mungu tusifike huko. Chuki imekujaa mpaka hata Rais mwana CCM pia haumpendi! Lo!
Mwambie afunge nchi! Akataze mikusanyiko, kusafiri na afunge hata ibada, mwenzio museven kafanya hivyo ndio nlichkuwa namaanisha sasa wewe kwakuwa bado una mimba ya yule kichaa basi kila kitu lazima umuhusishe!

Wanawake wengine mna shida hasa mkiwa wajawazito
 
Mbona hukufa kama hukuambiwa ukweli?
Na kama umeambiwa ukweli anza kujifungia home maana watu wengi bado wanajichanganya tu.

Na bado. La Corona sasa liko pazuri. Baada ya hili katiba mpya. Hamtaki Burundi watawapokea kwa mikono miwili.
 
Asante kwa matusi. Ndicho ulichobakiza tu hicho. Tutafika huko tu kama ndio maombi yako. Wengine tunaomba Mungu tusifike huko. Chuki imekujaa mpaka hata Rais mwana CCM pia haumpendi! Lo!
Nani kakwambia smpendi rais?
 
Kunyweni bupiji mkitembea kifua mbere ka-korona ni kaugonjwa kadogo tulishawahi kukashinda kwa staili hii, au nasema uongo ndugu zangu ?
 
Moja ya tahadhari ni kupunguza au kuacha mikusanyiko isiyo ya lazima!

Sasa yeye badala ya kuonyesha mfano kwa vitendo, anaenda kukusanyika na hao mapadri! Tena wamekusanyika ndani ya jengo. Siyo nje kwenye hewa inayozunguka vizuri.

Halafu kuna kwaya ilikuwa inaimba. Unapoimba huwa kuna vichembe chembe vya mate vinavyoruka. Na kama upo karibu na wengine, vinaweza kuwadondokea hao watu kirahisi sana.

Hayupo serious huyo mama. Anatoa tu maneno ya kuwafurahisha baadhi ya watu lakini vitendo vyake havionyeshi kama yuko serious.

Marekani huko shughuli za kikanisa zilisitishwa kabisa na watu wakawa wanasali kupitia mitandao, Zoom, YouTube, Facebook, nk.

Boya umejitahidi kuzama!

Ila ukweli ni kuwa, iwaje hakuwana taarifa ya sehemu aliuokua akitembelea kwenye hiyo hospital mpaka eti wapiga picha wake wakawa wameingia kimakosa??
 
Hekima ya kudungwa machanjo yenye sumu?

Nyie madalali wa chanjo ni vituko kweli kweli!
Kama wewe siyo mtu wa kusafiri, nani kakulazimisha kuchanjwa? Lakini Kama unasafiri kwa wenzetu, jua kwamba ni lazima uchanjwe. La sivyo huwezi kuingia kwenye nchi zao. Tumia akili siyo blah blah na “blanket statements”. For one size does not fit all. Hamjazoea ukweli kuwa siyo wote wenye mawazo sawa?
 
Wimbi la pili lilikuwepo wakati gani ? Dunia inaweza ikawa inakabiliana wimbi la tatu ila kuna kipindi sisi tulijitenga na dunia nawaomba wapitie vizuri wajue tupo wimbi la ngapi
 
Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!
Watu kama wewe ndio huwa haichelewi kuwanyoosha matokeo yake mnatusumbua kuwasingizia magonjwa ambayo sio yenu ili kutaja cause of death.

Uwe msikivu na usikilize wataalamu.
 
1624624175864.png
 
Back
Top Bottom