#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

IMG-20210625-WA0143.jpg
IMG-20210625-WA0142.jpg
 
Kama wewe siyo mtu wa kusafiri, nani kakulazimisha kuchanjwa? Lakini Kama unasafiri kwa wenzetu, jua kwamba ni lazima uchanjwe. La sivyo huwezi kuingia kwenye nchi zao. Tumia akili siyo blah blah na “blanket statements”. For one size does not fit all. Hamjazoea ukweli kuwa siyo wote wenye mawazo sawa?
haya kadungwe
 
Moja ya tahadhari ni kupunguza au kuacha mikusanyiko isiyo ya lazima!

Sasa yeye badala ya kuonyesha mfano kwa vitendo, anaenda kukusanyika na hao mapadri! Tena wamekusanyika ndani ya jengo. Siyo nje kwenye hewa inayozunguka vizuri.

Halafu kuna kwaya ilikuwa inaimba. Unapoimba huwa kuna vichembe chembe vya mate vinavyoruka. Na kama upo karibu na wengine, vinaweza kuwadondokea hao watu kirahisi sana.

Hayupo serious huyo mama. Anatoa tu maneno ya kuwafurahisha baadhi ya watu lakini vitendo vyake havionyeshi kama yuko serious.

Marekani huko shughuli za kikanisa zilisitishwa kabisa na watu wakawa wanasali kupitia mitandao, Zoom, YouTube, Facebook, nk.
Ni usanii tu kinachofanyika,hiyo Corona haipo kiviile hata yeye mama mwenyewe anajua ni vile kuonyesha tu na yeye kama anajali.
 
Ingalifaa wizara ya afya ianze tena kutoa takwimu za wagonjwa walioko kwenye hospitali zetu mbali mbali kila wiki kama ilivyokuwa kwenye wimbi la kwanza. Hii itasaidia wananchi wetu ku comply na njia za kupungupunguza maambukizi. Takwimu za kuchokonoa pua watu mitaani ambao ni wazima, ambazo ndizo WHO wanazitaka, waachane nazo kwani zoezi hilo linatisha, halina maana yo yote na linaweza kusambaza virusi vya corona.

Pesa itakayokopwa IMF (Tsh 1 trillion) itumike kununua mashine za kuzalisha oxygen kwenye kila hospitali zetu na vituo vyetu vya afya. Pesa hiyo inunue ventilators, respirators na vifaa tiba muhimu kuboresha huduma za hospitali zetu. Hii itasaaidia na wagonjwa wengine wasio na corona wanaohitaji uangalizi huo na vitakuwa ni vya kudumu hata pale corona itakapoondoka.

Pesa hiyo isinunue chanjo wala mabarakoa. Haya watupatie bure.
 
Tunakushukuru Madam President kwa Tahadhali sasa yunaomba utoe maelekezo haya
1. Daladala iwe kukeep social distance seat 1 iwe empty kila baada ya mtu

2. Mbio za Mwenge wa Uhuru zisimame ni kueneza ugonjwa

3. Bunge la bajeti nalo likatishwe kuepuka phase 3 ya Covd 19.

4. Piga Curfew, bar mwisho saa 1 jioni na shughuli zingine

5. Twanga Lockdown angalau siku 30. Mtu asitoke zaidi ya kata yake.

6. Fanya Mass Testing mtaa kwa mtaa , door to door.

7. Vurumisha Chanjo kwa kila anayepumua Tz

Nashukuru kwa kuwa huwa unapitia humu na kusoma naamini utalitekeleza vzr.

Ni hayo tu mama
 
“Tanzania tuna wagonjwa wa wimbi la Tatu la Corona. Hili jambo bado lipo, tuchukue hadhari zote na tunawaomba viongozi wa dini mseme hili kwa sauti kubwa"

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na baraza la maaskofu katoliki (TEC) #Tanzania #COVID19

=========

Rais Samia Suluhu: Wahashamu, baba Maaskofu kama mnavyofahamu, dunia kwasasa inakabiliwa na mlipuko wa Covid-19 na nafahamu kanisa tangu mwanzo limekuwa na msimamo Thabit katika kupambana na ugonjwa huu hivyo basi niwaombe sana Maaskofu msisahau kuwakumbusha waumini kuhusu wa kujikinga na kuchukua Tahadhari zote zinazoelekewa na wataalam wa Afya dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kwakuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba, tusiache kutumia kila kitakachotukinga na maradhi haya ili kuepesha vifo vya makundi.

Kama tunavyojua, duniani sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia, limekwenda limepungua kidogo, tumeingia Wimbi la Pili tumekwenda nalo na sasa kuna Wimbi la Tatu.

Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika kwenye wimbi hili la Tatu. Kama mnakumbuka siku nilitembelea hospitali ya Mwananyamala, kuna wodi daktari mfawidhi alikuwa ananiingiza akaniambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, nikamwambia hebu kuwa muwazi, ni covid, akaniambia ndio Covid wakati wapiga picha wangu tayari wameshatangulia, nikawaambia nyie tokeni haraka huko.

Kwahiyo ni kusema kwamba hili jambo bado lipo, tusijiche, bado lipo tuchukue hadhari zote na tunawaomba sana viongozi wa Dini mliseme hili kwa sauti kubwa, kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi.

Pamoja na yote hato, ni vyema pia tumuombe Mungu kwa kiasi kikubwa aendelee kutuepusha na kutupa hifadhi yake kutokana na maradhi hasa Janga hili la Corona kwakuwa yeye ndio Muweza wa Yote.


Anzeni kutoa takwimu
 
Mungu wa Mbinguni alitushindia mawimbi yote mawili ya awali ndiye atakaye tushindia hili linaloitwa la tatu.Pamoja na kwamba uongozi wake hautilii manani kuhimiza anao waongoza kumtegemea Mungu kwanza lakini bado Mungu wa Mbinguni amemletea Ujumbe, kuwa barako zitavaliwa na wanamzunguka tu si huku mitaani.

Kwa kutumia kutokuvaa barakoa mitaani ajue Mungu wa Mbinguni kampa Ujumbe kwamba Watanzania hawata acha ule msingi walio jengewa na mtangulizi wake 'JPM' wa KUMTEGEMEA na KUMPA KIPAUMBELE CHA KWANZA Mungu wa Mbinguni kwa kila jambo.
Asihadaiwe na anao kutana nao kwenye mikutano wamevaa barakoa uhalisia uko huku mitaani kwenye maisha ya kila siku. Wengine huvaa barakoa kulinda ajira ila nyoyo zao hazifurahishwi wala hazihiari.
 
Hata kama sikufa Mimi wengi walikufa kwa kuaminishwa uongo na yule tapeli Mwendazake
Hii biashara ya kusema "eti wengi walikufa" walikufa wapi huko ambapo wengine hawafiki?.

Kuna watu humu mnakuwa wanafiki sana.

👉🏾 Wewe ndiye mmojawapo wa wale waliosema "mlioenda Kilimarathon mjiandae kupukutika" leo kuna nini?.

Kwa kuwa kuna wimbi wa tatu na leo kuna mechi ya Biashara United na Yanga SC huko Tabora, watu waliojazana huko mpaka nafasi hakuna so, ni nini mnaaminisha watu?.

Kuna wakati tumia akili yako badala ya kutumia ya mtu mwingine 🤐!.
 
Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!
Hii ndiyo legacy ya mwendazake; kuwabadilisha watu wenye akili timamu kuwa majinga na maghalasha ya ajabu! Watu wanafariki kwa COVID 19 wewe 'unagaya' tu, unataka kujaribu sumu kwa kuionja!?
 
Back
Top Bottom