Rais Samia, tengua uteuzi wa Waziri Makamba na Bodi nzima ya TANESCO. Au na wewe una maslahi na kinachoendelea?

Rais Samia, tengua uteuzi wa Waziri Makamba na Bodi nzima ya TANESCO. Au na wewe una maslahi na kinachoendelea?

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,271
Reaction score
9,113
Kauli yako, ya waziri mkuu na ya waziri January Makamba inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa sana kwa mamlaka unaoendelea nchini.

Kauli zenu ndio zinafanya Watanzania watilie shaka weledi wenu kama viongozi wakuu wa nchi.

Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno, unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua?

Sababu zote mlizozitoa zinatushangaza Watanzania, tena ni za ghafla na kinzani.

Haiwezekani kuondoa wabobezi wa fani ya masuala ya umeme wote kwa mkupuo ukafanikiwa, never!

Hii teuzi ukiing'ang'ania itakuharibia kila jema uwazalo kwa Watanzania, hafai, lawama zote zitakuangukia wewe kiranja mkuu.

Ulisema, unasoma mitandaoni sana, kilio na mtazamo wa wananchi umeusikia, hivyo kwa sasa ni ngumu kwadanganya Watanzania.

Amua haraka kwa faida ya nchi, si dhambi kurekebisha kosa.

Soma pia

1) Kwa nia njema kabisa, Rais Samia mfute kazi Waziri Makamba

2) January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

3) Waziri January Makamba hana msaada wowote kwenye wizara ya Nishati, Tumechoka aisee
 
Ni wivu tu hamna lolote.

Huyo Makamba hiyo nafasi ana muda gani tangu ateuliwe. Yani muda huo mfupi ndio atatue matatizo tuliyojitengenezea miaka kibao?
Tatizo siyo mtu ila hiyo timu inayoogelea kwenye maziwa:

IMG_20211119_091739_123.jpg
 
Tatizo siyo mtu ila hiyo timu inayoogelea kwenye maziwa:

E
Ewaaaa...

Sasa hii timu mwendazake inadhani kutunbua ndio suluhisho la matatizo. Wametumbuliwa wangapi na bado tuko palepale

Tatizo ni watu walioamua kujipa madaraka uongozi wa nchi kwa.kutumia nguvu za dola.

Akili zilizoleta mharibiko ndio akili hizohizo eti zinataka kuondoa mharibiko na kuleta maendeleo

CCM yajenga nchi
 
Huo ukoo uache kama ulivyo.

Hadanganywi wala nini.

Huwa wanasuka wenyewe, Makamba hakuwa na jeuri ya kusafisha uongozi mzima wa Tanesco. Kama ambavyo Spika aliapisha wabunge feki, unadhani Ayoub ndiye aliwaandaa.

Ukiona nchi tatizo la vyoo vya shule au soko vinajadiliwa Rais akisimamishwa awapo ziarani ujue kuna shida kubwa ya mfumo.
 
Makamba ndiye kazuia mvua zisinyeshe? Ndiye amesababisha muwe wajinga na kutegemea chanzo cha umeme kimoja cha maji badala ya kugeukia njia mbadala (Gas)? Na kwa mabadiliko haya ya hali ya hewa hilo libwawa lenu mnalojenga bila akili litajaza matope na vyura tu...
 
Makamba ndiye kazuia mvua zisinyeshe? Ndiye amesababisha muwe wajinga na kutegemea chanzo cha umeme kimoja cha maji badala ya kugeukia njia mbadala (Gas)? Na kwa mabadiliko haya ya hali ya hewa hilo libwawa lenu mnalojenga bila akili litajaza matope na vyura tu.
Kusoma na kuelewa ni two different things, umesoma hujielewi dogo
 
Rais wa Tanzania ni Mh. Samia Suluhu Hassan kwa sasa. Waziri wa Nishati ni Mh. January Yusuph Makamba. Jina jingine mwite akili kubwa kabisa na hazina katika nchi yetu.
 
Huo ukoo uache kama ulivyo.

Hadanganywi wala nini.

Huwa wanasuka wenyewe, Makamba hakuwa na jeuri ya kusafisha uongozi mzima wa Tanesco. Kama ambavyo Spika aliapisha wabunge feki, unadhani Ayoub ndiye aliwaandaa.

Ukiona nchi tatizo la vyoo vya shule au soko vinajadiliwa Rais akisimamishwa awapo ziarani ujue kuna shida kubwa ya mfumo.
Kwani huo ukoo unataka kuufananisha na ule ukoo was panya.
 
Ni wivu tu... hamna lolote.

Huyo Makamba hiyo nafasi ana muda gani tangu ateuliwe. Yani muda huo mfupi ndio atatue matatizo tuliyojitengenezea miaka kibao?
Hawa misukule ya dikteta wapumbavu sana, kwanza kutwa wanamtukana Rais humu mitandaoni, halafu wanajitia kumshauri, imewauma sana msukuma mwenzao kutolewa uwaziri wapuuzi hawa
 
Nyie Ni wapumbavu kabisa,kutwa mnamtukana Rais,halafu mnajitia kumshauri, hivi mnataka Makamba aondolewe hili arudishwe msukuma mwenzenu Karimane, wapuuzi nyie
Stupidity reply [emoji35]
 
Back
Top Bottom