Rais Samia, tengua uteuzi wa Waziri Makamba na Bodi nzima ya TANESCO. Au na wewe una maslahi na kinachoendelea?

Rais Samia, tengua uteuzi wa Waziri Makamba na Bodi nzima ya TANESCO. Au na wewe una maslahi na kinachoendelea?

Kauli yako ,ya waziri mkuu na ya waziri January Makamba inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa sana kwa mamlaka unaoendelea nchini ,

Kauli zenu ndio zinafanya watanzania watilie shaka weledi wenu kama viongozi wakuu wa nchi.

Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno ,unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua ?

Sababu zote mlizozitoa zinatushangaza watanzania ,tena ni za gafla na kinzani.

Haiwezekani kuondoa wabobezi wa fani ya masuala ya umeme wote kwa mkupuo ukafanikiwa, never !

Hii teuzi ukiingangania itakuharibia kila jema uwazalo kwa watanzania,na lawama zote zitakuangukia wewe kiranja mkuu .
Ulisema, unasoma mitandaoni sana ,kilio na mtazamo wa wananchi umeusikia, hivyo kwa sasa ni ngumu kwadanganya watanzania .

Amua haraka kwa faida ya nchi ,si dhambi kurekebisha kosa
Anaachaje kuwa na interest ya kinachoendelea wakati ndo alomteua January hapo ilhali akijua January alikuwa miungoni mwa mabepari yalokuwa yakipinga ujenzi wa bwawa la Nyerere?
 
Anyway, ukimtoa Makamba unamweka nani ?
Ina maana expatriates wote tulionao hakuna wa kukalia kiti kile😆?

Mbona unanichekesha mkuu, wako watu waliobobea katika management ya electric industry toka abroad ni diaspora tunaweza waweka.

Najua wabongo hatuaminiani hasa waliosomea vyuo vya humu humu ila wako walio exposed ulaya they can play part n parcel ya kuokoa jahazi!
 
Kauli yako, ya waziri mkuu na ya waziri January Makamba inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa sana kwa mamlaka unaoendelea nchini.

Kauli zenu ndio zinafanya Watanzania watilie shaka weledi wenu kama viongozi wakuu wa nchi.

Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno, unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua?

Sababu zote mlizozitoa zinatushangaza Watanzania, tena ni za gafla na kinzani.

Haiwezekani kuondoa wabobezi wa fani ya masuala ya umeme wote kwa mkupuo ukafanikiwa, never!

Hii teuzi ukiing'ang'ania itakuharibia kila jema uwazalo kwa Watanzania, hafai, lawama zote zitakuangukia wewe kiranja mkuu.

Ulisema, unasoma mitandaoni sana, kilio na mtazamo wa wananchi umeusikia, hivyo kwa sasa ni ngumu kwadanganya Watanzania.

Amua haraka kwa faida ya nchi, si dhambi kurekebisha kosa
Atawezea wapi kumtengua mswahilii mwenzake, waswahili hujuana kwa vilemba. Wote hao wa mwambao wa pwani tabia ni moja, wanajuana vema.
 
Ewaaaa...

Sasa hii timu mwendazake inadhani kutunbua ndio suluhisho la matatizo. Wametumbuliwa wangapi na bado tuko palepale

Tatizo ni watu walioamua kujipa madaraka uongozi wa nchi kwa.kutumia nguvu za dola.

Akili zilizoleta mharibiko ndio akili hizohizo eti zinataka kuondoa mharibiko na kuleta maendeleo

CCM yajenga nchi
Kwani washamba wako bado wapo madarakani?

Si chama kimerudi kwenye mikono salama?
 
Atawezea wapi kumtengua mswahilii mwenzake, waswahili hujuana kwa vilemba. Wote hao wa mwambao wa pwani tabia ni moja, wanajuana vema.
Kweli kabisa yule aliyekuwa TAMISENI aliboronga akabadilishiwa wizara lakini msukuma akaliwa kichwa !
 
Kauli yako, ya waziri mkuu na ya waziri January Makamba inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa sana kwa mamlaka unaoendelea nchini.

Kauli zenu ndio zinafanya Watanzania watilie shaka weledi wenu kama viongozi wakuu wa nchi.

Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno, unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua?

Sababu zote mlizozitoa zinatushangaza Watanzania, tena ni za gafla na kinzani.

Haiwezekani kuondoa wabobezi wa fani ya masuala ya umeme wote kwa mkupuo ukafanikiwa, never!

Hii teuzi ukiing'ang'ania itakuharibia kila jema uwazalo kwa Watanzania, hafai, lawama zote zitakuangukia wewe kiranja mkuu.

Ulisema, unasoma mitandaoni sana, kilio na mtazamo wa wananchi umeusikia, hivyo kwa sasa ni ngumu kwadanganya Watanzania.

Amua haraka kwa faida ya nchi, si dhambi kurekebisha kosa
Makamba JR na bodi ndio wameleta ukame? Hivi ni chuki zinawasumbua au ni ni hasa?

In fact wapuuzi wa awamu ya 5 ndio wametufikisha hapa,haiwezekani unaweka pesa nyingi Kwenye mradi ambao haujui utaisha lini maana pesa za kuukamilisha huna na hujawekeza kujiandaa na hali ya dharura kama ukame huku ukitegegemea kudra za Mungu.Huu ni utaahira kabisa.
 
Back
Top Bottom