Kauli yako, ya waziri mkuu na ya waziri January Makamba inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa sana kwa mamlaka unaoendelea nchini.
Kauli zenu ndio zinafanya Watanzania watilie shaka weledi wenu kama viongozi wakuu wa nchi.
Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno, unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua?
Sababu zote mlizozitoa zinatushangaza Watanzania, tena ni za gafla na kinzani.
Haiwezekani kuondoa wabobezi wa fani ya masuala ya umeme wote kwa mkupuo ukafanikiwa, never!
Hii teuzi ukiing'ang'ania itakuharibia kila jema uwazalo kwa Watanzania, hafai, lawama zote zitakuangukia wewe kiranja mkuu.
Ulisema, unasoma mitandaoni sana, kilio na mtazamo wa wananchi umeusikia, hivyo kwa sasa ni ngumu kwadanganya Watanzania.
Amua haraka kwa faida ya nchi, si dhambi kurekebisha kosa.