Rais Samia: Tuache alama ili nchi yetu ipate maendeleo ya haraka

Sikumfahamu kwa ndani marehemu Mfugale lakini kwa yale aliyoyafanya, hakika ameacha alama katika maisha yake ya hapa Duniani. Hakuna shaka juu ya uchapakazi wake, hakuna shaka juu ya uzalendo wake, na mapenzi yake kwa Taifa. Hakuna shaka juu ya uwezo wake mkubwa wa utaalam wake. Amevitumia vema vipaji alivyopewa na Mungu.

Mungu wetu tunakushukuru kwaajili ya maisha na utumishi wake ndugu yetu Mfugale. Kwa kuwa umemwita kwako kwa wakati ulioona unafaa, japo ni kwa majonzi, tunalazimika kuyapokea mapenzi yako.

Tunakuomba muumba wetu, iipe faraja familia ya huyu ndugu yetu. Kwaajili ya mema mengi aliyoyafanya mzazi na mwanafamilia wao kwao kama familia na Taifa, itoshe kukushukuru wewe uliyemfanya akawa kama alivyokuwa.

Kwa mapenzi na huruma yako, tunakuomba yale mema aliyoyafanya kwaajili ya watu wako, yakatoshe kuwa sadaka ya yale ambayo hakuyatenda vema.

Kwetu tuliobakia, matendo mema ya huyu ndugu yetu yakawe shule, injili na mafunzo kwa maisha yetu.

Kuambiwa sababu ya kifo chake hakuwezi kubadilisha chochote kwa marehemu, lakini ni jambo ambalo linaondoa gossiping. Kifo na ugonjwa, siyo kosa la yeyote, na hakuna mwenye uwezo wa moja kwa moja katika kuvizuia. Sijui kwa nini siku hizi baadhi ya watu, na hasa viongozi, sababu za vifo vyao hazielezwi.
 

Pana mambo mawili tofauti:

1. Katiba mpya
2. Mikutano ya kisiasa

#2 ni haki ya vyama haihitaji ruksa ya mtu. Kuyachanganya mawili haya kumeongeza hali kutokuaminiana.

Kumbuka hata lile la kuonana na vyama vya siasa halina majibu Mama ataonana nao lini.

Uzi huu hapa chini uliandikwa Jun 22mapema kabisa kabla ya mkutano wake na wanahabari:

--------
My take:

Pana watu karibu na mama wanaofanya jitihada sana kumfarakanisha Mama na yeyote kwa lolote hata kama la kijinga. Pana wanaokaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune.

Angalia pia uzi huu:


Jipe muda kupitia kuiona hali halisi.
 
Rais aliahidi kukutana na viongozi wa kisiasa. Huko huenda wakazungumza mengi na kuja na mrejesho wenye kutosheleza akili na ufahamu.
 
Rais aliahidi kukutana na viongozi wa kisiasa. Huko huenda wakazungumza mengi na kuja na mrejesho wenye kutosheleza akili na ufahamu.

Kama nilivyoandika awali haipo nia njema tokea kwa washauri wa karibu wa rais.

Haipo nia ya kuwakutanisha rais na angalau Chadema. Nia iliyopo ni kuchochea mfarakano zaidi.

Pangekuwapo na nia njema rais asinge changanya suala la mikutano ya kisiasa na mambo ya katiba.

Uwezekano ni kuwa Mama ana mashinikizo ya ndani yasiyo na nia njema.
 
Mbona simple tu.......
unaujua umri wa Joe Biden raisi wa Marekani???
Afu hizo nafasi za kitaalamu wenzetu huwa wanapewa mda mrefu wa kustaafu sababu wanakuwa adimu hata hapa nafikiri walibadirisha kwa madaktari bingwa.
 
Ni mapema mno.
 
Ni mapema mno.

Dalili ya mvua ni mawingu. Ninakazia: msingi wa ngoma uko hapa:

 
Mh h
Mh Rais SSH nimemuelewa, kwamba amezungumza kuacha alama ya kiungonzi, thanks president


Sasa mungu anasema na wewe mh rais ,ACHA alama ya katiba mpya kadri inavyowezekana , jina lako likutakua ukurasa muhim asema bwana , achana na Ccm wengi wao wanafiki , Kama wanaona Chama ni muhim kuliko NCHI ,japo ndivyo walivyo ,tenda yako na Kama ccm watakuzingua pale ulipo fikia basi nenda Chama chochote Cha upinzani na chukua NCHI wahuni hao rais ,tenda uonavyo na imani ya Mungu ikiwa juu yako basi
 
Amen, Rais amezungumza kutoka moyoni na kutukumbusha sisi sote kuwa tunatakiwa kuacha alama.
Naamini naye ataacha alama kama alivyosema, alituomba tumpe muda; mema yanakuja.
 
Kumbuka kulegalega sio kufa. Ni katika siasa mtu anaweza kufa na kufufuka.
 
Amen, Rais amezungumza kutoka moyoni na kutukumbusha sisi sote kuwa tunatakiwa kuacha alama.
Naamini naye ataacha alama kama alivyosema, alituomba tumpe muda; mema yanakuja.
Mda upi ,kuanzia KWA rasm ya Warioba bado Kuna mchakato namshauri uanze ili uweze kamilika mapema , why SSH rais kuanza jitafutia lawama na laana ilihali Jambo lawezekana ,mh SSH , angalia Sana wanaccm waliokuzunguka ni wanafiki ,wapo pale KWA matumbo yao na familia zao ,Kama vile izo pesa watafutao KWA NJIA za wizi watazikwa nazo au hawatakufa
 
Kumbuka kulegalega sio kufa. Ni katika siasa mtu anaweza kufa na kufufuka.

Msingi wa ngoma uko hapa: kuna watu wamekuwa yamini kumfarakanisha Mama na yeyote na kwa lolote hata kama ni la kijinga.

Yeyote ni mwananchi mmoja mmoja au makundi. Mama upande mmoja na hao upande mwingine. Yataka busara sana kuuruka mtego huo hasa hasa tokea kwa Mama.

Agenda ni kuwa na Magufuli anayetawala asiyekuwapo.
 
Tuvumilie kidogo, mambo yatakuwa sawa. Mama atatimiza ahadi.
 
Busara itatumika kama unavyosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…