Rais samia: tumeondoa njaa kwa asilimia 100 kilichobaki ni mtu mmojammoja kuhakikisha halali njaa

Rais samia: tumeondoa njaa kwa asilimia 100 kilichobaki ni mtu mmojammoja kuhakikisha halali njaa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa sasa Tanzania imeondoa njaa kwa asilimia 100, akifafanua kuwa kilichobaki ni kuondoa kwa mtu mmojammoja.

Akizungumzia namna Tanzania inavyotekeleza Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) Rais Samia amesema nchi inajitosheleza chakula chake na zilizobaki ni jitihada za kuondoa njaa kwa mtu mmojammoja.

Ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 8, 2025 akihutubia katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake inayofanyika kitaifa jijini Arusha.

 
Mahindi yanakauka; Ngoja hizi mvua zisinyeshe mpaka Mei, Mungu asaidie tu, maana nikiangalia mashamba naogopa
 
Njaa inafika, mkoa Ruvuma, ukitembelea Tunduru njaa inakuja Kasi sana Lisa ukame
 
Kuna watu wapo hapo Tandale, 8km toka Ikulu wanabangaiza, na vijijini je? Hata 60% Bado
 
Ngoja muda ufike mtasema tu ukweli
Ukame kila kona mahindi yamekauka mpunga umekauka niko pale kuanzia mwezi wa 6 mtaongea tu
 
Kipensi changu sijapata mshahara na mda sasa nashindia dagaa na mchicha ata sijabadili mboga nawasilisha 😞😞💔
Ile niliacha imekwisha haya .... niambie nikutumie wapi maana kwa kubadili namba za kupokelea hela nimekushindwa
 
Mahindi yanakauka; Ngoja hizi mvua zisinyeshe mpaka Mei, Mungu asaidie tu, maana nikiangalia mashamba naogopa
Kwa waliolima mahindi/ mazao ekari 10, 20 30, 40 etc na wanategemea mvua ... Doooohhh.... Huruma sana....
 
Wewe na viongozi wako na watoto wenu ndiyo hamna njaa kwa asilimia mia Ila si kwa raia wa kawaida!
Ngoja hichi kizazi cha single mother kinacho kuja kwa kasi kikiwa akina maadili wala uwoga kwa Mambo wanayo yashuhudia toka wadogo ccm ndiyo mtajua hamjuh.
 
Siasa hizi
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa mkuu... Aje vijijini huku aridhi Haina rutuba Tena kama zamani kilimo kimekuwa ghali kinatakiwa uwekeze pesa walau uvune mazao ya kueleweka. Kama mwaka huu watu wamelima mazao yamenyaukia shambani halafu unaambiwa tumepinguza njaa
 
Back
Top Bottom