Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
===
Serikali ya Tanzania imesema imeingia mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya abiria 89, vichwa vya treni ya umeme 19, seti za treni za kisasa 10 zenye behewa 80 vikiwa na gharama ya US$381,428,465 karibu TZS 880BL,
Hayo yamebainishwa leo siku ya Jumanne Desemba 28, 2021 na Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora.
Kipande hiki kina urefu wa kilometa 368, kitakachogharimu Dola za Marekani bilioni 1.908 sawa Sh4.41 trilioni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka Uturuki.
Amesema pamoja na hayo Serikali inaendelea kukamilisha ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1,430 yenye thamani dola za Marekani US$127,206,300 sawa na TZS 292BL,
“Nitumie fursa hii kuagiza wizara na TRC kuhakikisha kuwa inasimamia kwa karibu ili kasi ya ujenzi iendane na kasi ya kusimamia ununuzi wa vifaa hivyo"
"Hii itafanya vifaa viwe vimekamilika sambamba na kukamilika kwa ujenzi wa reli. Vinginevyo miundombinu ya reli itakamilika huku tukisubiri kuwasili kwa vifaa na kuhakikisha ubora unaendana na thamani ya fedha."
“Nasema hivi kwa sababu miezi michache nimekaa katika Serikali hii nimeona kuna mambo yanataka kuanza kufanyika na mimi sitakubali yafanyike"
"Kwamba mradi unasimamiwa na wizara kupitia sekta husika, anatafutwa mkandarasi anapopatikana anakuwa na wasemaji wengi ndani ya nchi, na hasemewi bure watu wanajua watavuna"
"Sasa nasema mimi sijali mkandarasi atasemewa na watu elfu ninachotaka kusema nataka reli iwe ya viwango tulivyokubaliana,” amesisitiza
===