Rais Samia: Tumeshalipia treni 19 za Umeme na mabehewa 89, Seti 10 za treni na mabehewa 80 kwaajili ya mizigo

mradipic
Serikali imesema imeingia mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya abiria 89, vichwa vya treni ya umeme 19, seti za treni za kisasa 10 zenye behewa 80 vikiwa na gharama Dola za Marekani milioni 381,428,465.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Desemba 28, 2021 na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora chenye urefu wa kilometa 368, kitakachogharimu Dola za Marekani bilioni 1.908 sawa Sh4.41 trilioni kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka Uturuki.

Amesema pamoja na hayo Serikali inaendelea kukamilisha ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1430 yenye thamani dola za Marekani milioni 127,206,300.

“Nitumie fursa hii kuagiza wizara na TRC kuhakikisha kuwa inasimamia kwa karibu ili kasi ya ujenzi iendane na kasi ya kusimamia ununuzi wa vifaa hivyo. Hii itafanya vifaa viwe vimekamilika sambamba na kukamilika kwa ujenzi wa reli. Vinginevyo miundombinu ya reli itakamilika huku tukisubiri kuwasili kwa vifaa na kuhakikisha ubora unaendana na thamani ya fedha."

“Nasema hivi kwa sababu miezi michache nimekaa katika Serikali hii nimeona kuna mambo yanataka kuanza kufanyika na mimi sitakubali yafanyike. Kwamba mradi unasimamiwa na wizara kupitia sekta husika, anatafutwa mkandarasi anapopatikana anakuwa na wasemaji wengi ndani ya nchi, na hasemewi bure watu wanajua watavuna. Sasa nasema mimi sijali mkandarasi atasemewa na watu elfu ninachotaka kusema nataka reli iwe ya viwango tulivyokubaliana,” amesisitiza
Kaziindelee, Tuko vizuri sana
 
Ndo maana nasema , tz bado hutajapata watu sahii, katika mifumo yetu, unalipia tren za umeme pesa inabaki tu WAKATI mradi wa reli bado, achana na changamoto ya umeme, sijui zitakua zatumia umeme wa kufua zenyewe,

Tunakimbizana lipia kitu ambacho hakianzi kesho fanya kazi wakati ,zipo Sehem kibao kunauhitaji wa kuelekeza pesa, then matokeo yake tozo, kukimbilia kukopa

Tatizo nilionalo ni Kwamba , tunashindwa kutambua kipi kianze ,na kifuatie kipi katika matumizi ya pesa,

Mfano unanunua ndege keshi, kumbe unaweza kuzikopa ukawa unalipa kidogodogo
 
Ndo maana nasema , tz bado hutajapata watu sahii, katika mifumo yetu, unalipia tren za umeme pesa inabaki tu WAKATI mradi wameme bado, achana na changamoto ya umeme, sijui zitakua zatumia umeme wa kufua zenyewe,

Tunakimbizana lipia kitu ambacho hakianzi kesho fanya kazi watu ,zipo Sehem kibao kunauhitaji wa kuelekeza pesa, then matokeo yake tozo, kukimbilia kukopa

Tatizo nilionalo ni Kwamba , tunashindwa kutambua kipi kianze ,na kifuatie kipi katika matumizi ya pesa,

Mfano unanunua ndege keshi, kumbe unaweza kuzikopa ukawa unalipa kidogodogo
Duuuh, nyie mmeshazoea kuanza ujenzi wa madarasa mwezi January as if hamkujua kwamba kuna wanafunzi watatakiwa waanze shule January. Mama amekuja kitofauti, planning chain. Sasa ulitaka reli ikishakamilika ndipo mtoe oda halafu ichukue miaka 10 ili treni zifike ndipo reli ianze kazi??? Hivi watanzania vichwani mmejaza mavi au?
 
Duuuh, nyie mmeshazoea kuanza ujenzi wa madarasa mwezi January as if hamkujua kwamba kuna wanafunzi watatakiwa waanze shule January. Mama amekuja kitofauti, planning chain. Sasa ulitaka reli ikishakamilika ndipo motor oda halafu ichukue miaka 10 ili treni zifike ndipo reli ianze kazi??? Hivi watanzania vichwani mmejaza mavi au?
Mkuu nafikili,shida Yangu sio kuweka order ambayo inaweza endelea lipiwa kidogokidogo, KWa sababu tren za umeme, reli sio mradi wa kuanza ndani ya miaka nne, Ayo ni maneno tu, kulipia kesh wakati mradi ndo kwanza kipande KINGINE kimetiwa sain, ni kukosa au shindwa pangilia vipaumbele
 
Jiji la pili kwa ukubwa Tanzania linaitwaje?

Unajua kwa nini daraja la Kigongo busisi linajengwa?

Unajua kwa nini meli kubwa sana inajengwa ziwa victoria?

Unajua Uganda wanapitishia wapi mizigo yao?

Unaijua population ya kanda ya ziwa?

Mungu akubariki sana Samia
 
Mkuu nafikili,shida Yangu sio kuweka order ambayo inaweza endelea lipiwa kidogokidogo, KWa sababu tren za umeme, reli sio mradi wa kuanza ndani ya miaka nne, Ayo ni maneno tu, kulipia kesh wakati mradi ndo kwanza kipande KINGINE kimetiwa sain, ni kukosa au shindwa pangilia vipaumbele
Wakati mwingine waaminini walioko Serikalini. They're too Tanzanians, educated and some are patriotic and highly exposured.
 
Back
Top Bottom