Rais Samia: Tunaandaa mradi wa kuomba hela za kujenga stendi. Hayati Magufuli asingethubutu kusema kitu cha kujitweza utu wetu namna hiyo... never!

Wanaandaa mradi wa kuomba hela! Au mimi sijui kiswahili, yaani kuomba hela nako unakatengenezea mradi ili ukizipata hizo hela unazitumia kutumia kwenye mradi wa kujenga stendi!
Mimi cha kwanza kilichonishangaza Ni hicho ila sikutaka kuhoji kama ulivyofanya nikihofia labda yalikuwa Ni makosa ya Mleta Uzi. Na kama amenukuliwa vilivyo basi tuna Kiongozi ambaye Ni JANGA.
 
Wewe msukule wa mbowe, mikopo unapinga na tozo unapinga.

Unataka nini ?

Atolewe makengeza jela aje kukupelekea moto ?
Mikopo tunapinga na tozo tunapinga ?

Kwa hiyo serikali imeamua kufanya lipi, kuendelea kuomba omba au kuondoa tozo ??????
Mkuu, huyu mtu tulishasema na yeye amekiri hana uwezo kama wa Magufuli lakini cha ajabu anataka tena miaka mitano. Miaka Kitano ya nini? Mimi nadhani baadhi ya watu wa Pwani wana matatizo ya kupenda kuombaomba.
Yani anafanana nae kupita maelezo, wote wawili wanapenda kuomba omba.

Spichi ya Mbezi Luis Magufuli alisema "hata ukitaka kujenga nyumba ukisubiri upate hela yote hutajenga.... tutafanya mambo haya kwa ujasiri wa kujitegemea."

He made us proud. He was the truest apostle of Tanzanian identity and pride since Julius Nyerere.

Samahani mkuu, ni misunderstands tu. Heshima kwako
 
Huwezi kuandika pumba alafu tupite bila kukuonya, take easy with wrong logic.
Wewe una ubongo wa kujua pumba? Thubutu!! Kama umeshindwa kuwlewa hoja yangu.

Rudi pale kahesabu "Likes" ndiyo utajiona uko sawa na sisimizi
 
Magufuli alikuwa MWONGO na akasababisha hata wa chini yake kuwa waongo. Na hata alipokufa tuliendelea kuambiwa uwongo na Majaliwa kuwa yuko ofsini anapitia mafaili.

Rais SSH endelea kuwa mkweli, penye hatuna pesa ongeza tozo au kakope, period
Licha ya hii comment yako bado sikuaminigi kabisa. Huna msimamo na hicho kitu kinanikera kupita maelezo. Mwanaume unatakiwa kuwa thabit siyo legelege.

brazaj
 
Licha ya hii comment yako bado sikuaminigi kabisa. Huna msimamo na hicho kitu kinanikera kupita maelezo. Mwanaume unatakiwa kuwa thabit siyo legelege.

brazaj
Wewe unaishi kwa kukariri ndiyo maana unaniona Sina msimamo. Unataka niseme Mbowe siyo gaidi, Mimi nasema Mbowe ni mtuhimiwa wa ugaidi, tuiachie mahakama.

Unataka Katiba Mpya, ninataka Katiba Nzuri kwa matakwa ya wananchi na siyo kwa msukumo wa CHADEMA.

Unaponda kila kitu anachofanya Rais SSH, nina muunga mkono kwa hatua anazochukua kuhusu kujenga uchumi
 
Uchumi gani?
 
Mkuu 'Overspoon', sielewi kwa nini umenihusisha kwenye andiko lako hili uliloniunganisha pamoja na 'Matola'! Ni wapi nilipompigia kampeni huyo mama aendelee mapaka huko unakokusema wewe?

Lakini inawezekana hukuelewa nilichoandika , na ulipofika kwa 'Matola' ukaona unirukie mimi bila kuelewa nilichoandika. Naona huna muda mrefu sana hapa jukwaani, kwa hiyo inawezekana bado unajifunza jinsi ya kuutumia huu ukumbi.
 
Licha ya hii comment yako bado sikuaminigi kabisa. Huna msimamo na hicho kitu kinanikera kupita maelezo. Mwanaume unatakiwa kuwa thabit siyo legelege.

brazaj

Ninakusoma mkuu wangu. Kuna mambo yanafikirisha sana.
 
Mkuu uko sawa kabisa. Magufuli asingethubutu kusema haya hadharani, ule alikuwa wanaume hasa. Ni jasiri pekee anayeweza kula mpaka pesa za wastaafu na kisha kuwaacha njaa. Kumbuka habari za pssf kudaiwa 6tln. Haya angeweza kufanya magufuli pekee yake. Huyu mama ana huruma sana ndio maana anajitahidi kuomba kwa jirani kama watoto wake hawa watapona njaa kubwa waliachiwa na mzazi wa kambo.
 
Magufuli alikuwa MWONGO na akasababisha hata wa chini yake kuwa waongo. Na hata alipokufa tuliendelea kuambiwa uwongo na Majaliwa kuwa yuko ofsini anapitia mafaili.

Rais SSH endelea kuwa mkweli, penye hatuna pesa ongeza tozo au kakope, period
Mara ngapi tuliambiwa SGR, Stiglers Gorge /JNHEP vyote vinajengwa kwa pesa za ndani. Je, ukweli kwa sasa upo wazi. Ni mikopo kwenda mbele.
 
Magufuli alikuwa MWONGO na akasababisha hata wa chini yake kuwa waongo. Na hata alipokufa tuliendelea kuambiwa uwongo na Majaliwa kuwa yuko ofsini anapitia mafaili.

Rais SSH endelea kuwa mkweli, penye hatuna pesa ongeza tozo au kakope, period

πŸ™πŸ™πŸ™
 
Usimfananishe magu na Hangaya, Hangaya ni mkweli, mtulivu, ameleleka kimaadili, leo watu wanapata kazi kumtetea marehemu, kisa mapungufu yake, acha kumpa sifa mtu/marehemu aliye umbuka!
 
Je, wajua magu akitaka kutupeleka N.korea?
 
Magufuli alikuwa anadanganya kuwa mradi huu au ule umejejengwa kwa hela za ndani. Maneno kama "hela zipo" yalikuwa ya kawaida masikioni mwa watu. Kitu ambacho kilikuwa kikisemwa ni kuwa alikuwa anakopa ile mbaya kwa miradi ambayo anadai inagharamiwa kwa pesa ya ndani. Samia yeye ni muwazi. Anasema wazi kuwa anakopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…