Pre GE2025 Rais Samia: Tunaelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nileteeni Watu wazuri ili nikishusha Mahela yatumike vizuri

Pre GE2025 Rais Samia: Tunaelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nileteeni Watu wazuri ili nikishusha Mahela yatumike vizuri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ok,kila la heri ndugu zetu watz.
naona uchaguzi upo mlangoni.
 
Eti shangazi!😄
Halafu wale wanamuita mama yetu wengine bibi yetu. Hivi marais waliopita tulikuwa tunawaitaje? Uncle, mjomba? Ukiachia mbali baba wa taifa.
Uncle Magu
 
Nilimsikia akiwaambia acheni kusokotana! 😆😆 nikakumbuka kipindi nipo Unguja
 
View attachment 3059831
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza na wananchi wa Dumila mkoani Morogoro na kuwaunga kwa kununua nyanya, bamia, tangawizi, mahindi yeboyebo na vitu vingine vilivyokuwa vikiuzwa na wajasiliamali wadogo wadogo pamoja na kuwapatia shilingi milioni 20 kwa ajili ya genge lao.

Aidha Rais Samia amewataka wakazi hao kuchagua viongozi wazuri katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa ambao watamsaidia kuwafikishia maendeleo.
Waliopo wote kwa sasa ni CCM je wamefanya nini? akawadanganye CCM wenzake
 
CDM mnawaza ugomvi tu mna muda wa kuwaza maendeleo ya wananchi.
 
Na viongozi wazuri na bora wenye uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo na fedha za maendeleo ni lazima watoke CCM tu.huko kwa wapinzani ni wababaishaji tu.angalia mtu kama Lissu aliwachangisha watu pesa ili anunue gari la kifahari kwa raha zake ,lakini mpaka sasa yupo kimya na hasemi pesa zimekwenda wapi na zilipatikana kiasi gani.

Wananchi nawasihi sana kuhakikisha mnachagua viongozi wa CCM katika ngazi zote.maana CCM itawaleteeni wagombea wazuri, waadilifu, wachapakazi,waaminifu na wazalendo.
Umechukua formu mujenziii.
 
Hii pesa alochangiwa Lissu inaonekana imekuuma sana tena sana sasa nakushauri nitafute inbobo tuongee nikufanyie utaratibu wa kupata hela
 
Akishusha mahela baada ya kuchukua mahela ?; Kwahio Sera ni kushusha mahela na sio kuleta Sera za watu kuweza kupata mahela ?
 
Back
Top Bottom