Rais Samia tunakuomba hutubia taifa, omba radhi, fanya maamuzi magumu ya kuvunja mkataba huu nchi ipone

Rais Samia tunakuomba hutubia taifa, omba radhi, fanya maamuzi magumu ya kuvunja mkataba huu nchi ipone

Tatizo la Sa100 bhn ni mvivu wa kusoma makabrasha ndio maana wasaidizi wake wana take advantage wanamuingiza chaka, rejea kauli yake maarufu "hili nalo muende mkalitazame"!!.
Mie naamini alikuwa na nia nzuri kabisa mama wa watu juu ya mkataba wa bandari...kuongeza ufanisi bandarini ila sasa UVIVU umemkosti, anawategemea wasaidizi zaidi.
Wasaidizi wenyewe wahuni tu, nadhani wanamdharau kwa uanawake wake pamoja na upole, JPM aliogopwa sana na wasaidizi wake kwasabb ya ukali na ubabe...makosa wakati wake ni yake binafsi!.
Mama punguza upole na kuwa mkali kidogo, utafanikiwa.
 
Sidhani kwani hii mechi ilishachezwa siku nyingi na hata kabla ya mechi kuchezwa walikuwa na 'matokeo yao mkononi'!
 
,Wajibisha wanaopaswa kuwajibishwa ,Toa dira mahsusi, Kemea uzembe wote
Hangaya hana huu msamiati wa kuwajibisha katika taratibu zake.

Ni raisi dhaifu kupitiliza....mbaya zaidi hana maamuzi anategemea mwongo kutoka uchochoroni.
 
Wakati wa Sakata la Tegeta ESCOW Rais Msaafu alitumia Mbinu nzito kipropaganda-Tenzi dume na kwenda USA Kutibiwa huku taifa likijurishwa Kwa picha na taarifa Za mara Kwa mara..Alipata Public sympathy kubwa..

Aliporudi tu akafanya Press Conference kubwa Kwa minajiri ya kuzungumza na wazee wa Dar Kama sikosei..

Lakini Kwa unyenyekevu alichutama akachukua hatua Kwa kuomba wote waliogubikwa na sakata la uchotwaji na umma ukajua wampishe..Wakajiuzuru kadhaa akiwemo Prof Mama Tibaijuka..Siku chache baadae akavunja Baraza la Mawaziri..Na hatua nyingi zingine

Nchi ikapoa..Maisha yakaendelea..
 
DP World
 

Attachments

  • 85A10A50-1028-483F-8B51-C109F455EE32.jpeg
    85A10A50-1028-483F-8B51-C109F455EE32.jpeg
    37.4 KB · Views: 3
Wasiwasi wangu mkubwa Upo Kwa wasaidizi wenye uchu wa madaraka Makuu ya nchi,Lakini pia Upo Kwa chawa waunga mkono hoja sababu ya maslahi Yao tu..

Hawa wasaidizi wanaoutaka Urais kwao ni furaha kubwa sana Mama akiharibu Sifa zake nzuri kiutendaji (Siasa na uchumi)..Wapo wanaotamani uchaguzi Uwe kesho..Watajitokeza Kwa wingi wakiwa wakavu na watajitenga na mabaya yote Bali mema watayabeba..

Wataka Urais wana kiu na uchu Kwa kusukumwa na ubinafsi,wafadhiri walio nyuma yao na visasi ..Wengi wanatenda sio Kama wasaidizi Bali kujijenga kisiasa Kwa kuonyesha wanaweza kushika hatamu ya taifa..Mama utendaji wako umewafunika sasa sidhani Kama wanafurahia..At times watakushauri ukosee,watatenda uonekane mbaya..wajenge msingi wao..

Chawa..Hawa ni ndugu zetu walio kindakindaki ktk kuunga mkono kila jambo liwe baya,Zuri,..Waelewe/wasielewe..Lengo Lao kubwa ni kukufurahisha Kwa wakati husika..Ni waimbaji wazuri wa mapambio na singeli..Kundi hili maslahi yao kukidhi haja Za ndogo ndogo za kiuchumi,kutetea viti vyao kisiasa ndio nguzo kuu..

Chawa huhama toka mtawala mmoja kwenda mwingine..Alipokuwepo Mwamba wa Chato walikuwa waliunga mkono kila jambo..walimtukuza Kwa kila mbwembwe wengine kudiriki kuwachapa viboko wakosoaji wote..wengine kudiriki hata kuhamasisha makabira yao kujiandaa Kwa vita ya kulinda maslahi..wanasema Kiongozi wa milele..hufiii,ukifa nasi twafa na weye…Tajiriiii,Ulipo tupoooo….Hawa sio wa kuwaamini sana..
 
Katika jambo linalonihuzunisha ni kuambiwa kwamba sisi na vizazi vyetu tutakuwa watumwa wa mwarabu milele.
 
Atahutubia kuwaambia nini?
 

Attachments

  • 0ED391C5-C517-4703-BE1B-2D34801AABA9.jpeg
    0ED391C5-C517-4703-BE1B-2D34801AABA9.jpeg
    55 KB · Views: 4
Mleta mada wahi mirembe. Yaani Rais aombe radhi kwa kufanya jambo lenye maslahi mapana na faida kwa Taifa?
 
Rais umefanya mema na mazuri kupitia uongozi wako. Mungu mtakatifu ana kusudi la kukupa nafasi kuu ktk nchi yetu ktk mazingira uliopewa si Kwa mapenzi ya wanadamu Bali Mungu tu..Si Kwa wewe kutaka Bali neema tu.

Wengi sana walijitokeza (Watangaza nia)ili kupewa kijiti cha kupeperusha bendera ya CCM..Walilipa fedha, Walizunguka nchi nzima wakijinadi Kwa wanachama (Wajumbe) na wananchi. Mwenyezi Mungu hakuwapa nafasi kupitia michakato mbalimbali ya Chama na kitaifa..

Ilimpendeza Mungu Hayati JPM awe kiongozi Mkuu wa taifa hili tajiri na wewe kuwa Msaidizi wake au makamu wake. Mungu alimpangia Siku,saa,mazingira ya kutwaliwa ktk mwili..Mwili wake umefariki huku roho yake ikisubiri hukumu Kama ilivyo Kwa wanadamu wote Kwa mujibu wa maandiko..

Yamkini nia na makusudi ni njema kabisa Kwa mujibu wa upembuzi wa viongozi wetu haswaa ktk kukuletea taifa tija Kina endelea ELIMU, AFYA, MIUNDOMBINU, N.K. Kwa lilivyo hili jambo sio jepesi ni zito mnoo. Limeenea mnoo..Lina ukakasi mnoo,Halina amani. Halina furaha. Halina utulivu. Linachakata mioyo, roho, fahamu Za wananchi maskini, wenye kipato cha kati na wasomi (Elimu bure imeleta effect ktk fikra)..

Viongozi wetu, Mitihani ktk maisha ya Uongozi haina budi kuruhusiwa kuwapata..Fanyeni toba Kwa Mwenyezi Mungu. Ombeni hekima na busara. Fanyeni maamuzi magumu yenye kuleta amani,Utulivu na mshikamano..

Kwa Heshima na unyenyekevu mkubwa nikuombe Mh Rais ikikupendeza hutubia taifa Kwa muda utakaokufaa na Utoe ufafanuzi wa mapana,Omba radhi kwenye mapungufu, Elimisha itakapobidi,Wajibisha wanaopaswa kuwajibishwa ,Toa dira mahsusi, Kemea uzembe wote (Watumishi na Viongozi wote wa umma hutenda kazi Kwa niaba yako Mh Rais,..Huwezi kufika kila mahali. Huwezi soma kila kitu,Huwezi fuatilia kila jambo..Huwezi saini kila nyaraka.

Mwisho usisahau kuwasamehe wote wate waliokukosea,Kukuudhi,Kuumiza moyo,na kukukwaza sana ktk kipindi hiki..Ni mtihani kwako. Mwenyezi Mungu anatusamehe makosa yetu tunaposamehe wengine wanaotukosea.

Kwa kuwa watendaji wako na wasaidizi wako ni binadamu hivyo wana mapungufu Kwa namna moja au nyingine hivyo hawawezi kuwa sahihi Kwa kila jambo Kwa kuzingatia changamoto za kimazingira, elimu, Utandawazi na mengineo.

Nina imani Watanzania wana imani na uongozi wako na jitihada zote ufanyazo ktk kuimarisha na kujenga umoja wa kitaifa. Kwa hotuba yako mjadala utakoma na mengi mema yako na serikali yatatamalaki zaidi..
Kisa wewe but acha uzuzu tafuta pesa
 
Back
Top Bottom