Tunapoomba hata Kwa Mwenyezi Mungu majibu huwa ni ya kusubiri,Mungu Mwenyezi hujibu Kwa wakati wake sababu yeye hapangiwi..
Vivyo hivyo Mh Rais ktk nchi Ana majukumu mengi ,makubwa na mazito..Kila Siku anapokea mengi na kufanyia kazi yeye mwenyewe au wasaidizi..
Hivyo tumeomba Kwa unyenyekevu,ikimpendeza atajibu maombi yetu..na majibu yaweza kuwa ndio au hapana..
Majibu yaweza kawia kuja..Kama ambavyo bosi hafokewi,anuniwi,hatiswi..Tuendelee kuomba Kwa upole,busara,staha..Tumejariwa Rais msikivu mnoo..Tumwombee sana Mwenyezi Mungu amjalie ujasiri,maarifa,nguvu na kibali cha kufanya maamuzi yenye haki,kweli na tija Kwa vizazi vya sasa na vijavyo..