Rais Samia tunakuomba hutubia taifa, omba radhi, fanya maamuzi magumu ya kuvunja mkataba huu nchi ipone

Tatizo la Sa100 bhn ni mvivu wa kusoma makabrasha ndio maana wasaidizi wake wana take advantage wanamuingiza chaka, rejea kauli yake maarufu "hili nalo muende mkalitazame"!!.
Mie naamini alikuwa na nia nzuri kabisa mama wa watu juu ya mkataba wa bandari...kuongeza ufanisi bandarini ila sasa UVIVU umemkosti, anawategemea wasaidizi zaidi.
Wasaidizi wenyewe wahuni tu, nadhani wanamdharau kwa uanawake wake pamoja na upole, JPM aliogopwa sana na wasaidizi wake kwasabb ya ukali na ubabe...makosa wakati wake ni yake binafsi!.
Mama punguza upole na kuwa mkali kidogo, utafanikiwa.
 
Sidhani kwani hii mechi ilishachezwa siku nyingi na hata kabla ya mechi kuchezwa walikuwa na 'matokeo yao mkononi'!
 
,Wajibisha wanaopaswa kuwajibishwa ,Toa dira mahsusi, Kemea uzembe wote
Hangaya hana huu msamiati wa kuwajibisha katika taratibu zake.

Ni raisi dhaifu kupitiliza....mbaya zaidi hana maamuzi anategemea mwongo kutoka uchochoroni.
 
Wakati wa Sakata la Tegeta ESCOW Rais Msaafu alitumia Mbinu nzito kipropaganda-Tenzi dume na kwenda USA Kutibiwa huku taifa likijurishwa Kwa picha na taarifa Za mara Kwa mara..Alipata Public sympathy kubwa..

Aliporudi tu akafanya Press Conference kubwa Kwa minajiri ya kuzungumza na wazee wa Dar Kama sikosei..

Lakini Kwa unyenyekevu alichutama akachukua hatua Kwa kuomba wote waliogubikwa na sakata la uchotwaji na umma ukajua wampishe..Wakajiuzuru kadhaa akiwemo Prof Mama Tibaijuka..Siku chache baadae akavunja Baraza la Mawaziri..Na hatua nyingi zingine

Nchi ikapoa..Maisha yakaendelea..
 
DP World
 

Attachments

  • 85A10A50-1028-483F-8B51-C109F455EE32.jpeg
    37.4 KB · Views: 3
Wasiwasi wangu mkubwa Upo Kwa wasaidizi wenye uchu wa madaraka Makuu ya nchi,Lakini pia Upo Kwa chawa waunga mkono hoja sababu ya maslahi Yao tu..

Hawa wasaidizi wanaoutaka Urais kwao ni furaha kubwa sana Mama akiharibu Sifa zake nzuri kiutendaji (Siasa na uchumi)..Wapo wanaotamani uchaguzi Uwe kesho..Watajitokeza Kwa wingi wakiwa wakavu na watajitenga na mabaya yote Bali mema watayabeba..

Wataka Urais wana kiu na uchu Kwa kusukumwa na ubinafsi,wafadhiri walio nyuma yao na visasi ..Wengi wanatenda sio Kama wasaidizi Bali kujijenga kisiasa Kwa kuonyesha wanaweza kushika hatamu ya taifa..Mama utendaji wako umewafunika sasa sidhani Kama wanafurahia..At times watakushauri ukosee,watatenda uonekane mbaya..wajenge msingi wao..

Chawa..Hawa ni ndugu zetu walio kindakindaki ktk kuunga mkono kila jambo liwe baya,Zuri,..Waelewe/wasielewe..Lengo Lao kubwa ni kukufurahisha Kwa wakati husika..Ni waimbaji wazuri wa mapambio na singeli..Kundi hili maslahi yao kukidhi haja Za ndogo ndogo za kiuchumi,kutetea viti vyao kisiasa ndio nguzo kuu..

Chawa huhama toka mtawala mmoja kwenda mwingine..Alipokuwepo Mwamba wa Chato walikuwa waliunga mkono kila jambo..walimtukuza Kwa kila mbwembwe wengine kudiriki kuwachapa viboko wakosoaji wote..wengine kudiriki hata kuhamasisha makabira yao kujiandaa Kwa vita ya kulinda maslahi..wanasema Kiongozi wa milele..hufiii,ukifa nasi twafa na weye…Tajiriiii,Ulipo tupoooo….Hawa sio wa kuwaamini sana..
 
Katika jambo linalonihuzunisha ni kuambiwa kwamba sisi na vizazi vyetu tutakuwa watumwa wa mwarabu milele.
 
Atahutubia kuwaambia nini?
 

Attachments

  • 0ED391C5-C517-4703-BE1B-2D34801AABA9.jpeg
    55 KB · Views: 4
Mleta mada wahi mirembe. Yaani Rais aombe radhi kwa kufanya jambo lenye maslahi mapana na faida kwa Taifa?
 
Kisa wewe but acha uzuzu tafuta pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…