Rais Samia, tunaomba Umtoe Mkurugenzi wa NBS, atatuharibia Sensa. Hili ni suala la Kitaifa

Rais Samia, tunaomba Umtoe Mkurugenzi wa NBS, atatuharibia Sensa. Hili ni suala la Kitaifa

Salaam Wakuu,

Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa, tunaomba apumzishwe ili kazi hii ya Sensa iende Vizuri. Hili ni Suala la Kitaifa si Swala la CCM. Kila mtanzania anatakiwa ashiriki hata asiyekuwa na chama.

Tutafute Mtu asimamie Sensa kwa Manufaa ya Nchi. Dk Chuwa tunamshukuru kwa muda wote aliofanya kazi NBS, apangiwe kazi nyingine. Tunafanya hivi kwa Manufaa ya Umma na Taifa kwa Ujumla.

Sheria ya Takwimu inaumiza sana Nchi. Pale NBS weka mtu mwenye uchungu na Nchi hadi hili jambo lipite ndo tuendelee na mambo ya Mazoea.

Mtakwimu huyu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, anadai eti tathmini iliyofanywa hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imebaini asilimia 97 ya Watanzania wako tayari kuhesabiwa. Na Rais Samia akaaminishwa hivyo. Wakati kuna Sehemu hata hawajui tarehe ni lini, Au hawajapewa hela ya kuzunguka nchi kutangaza au kutumia Mitandao ya kijamii?

Sifurahii kuona hii Sensa inaenda vibaya sababu ya watu wachache wanaotaka kumharibia Rais Samia aonekana anabeba watu.

Tunaomba Kamishina wa Sensa Anna Makinda, apewe mtu sahihi wa kufanya naye kazi, Makinda kajitengenezea heshima kubwa kwa muda mrefu, Msimchafulie CV yake.

Pia kama ameamua kufanya kazi na vyama vya Siasa, angeita vyama vyote akae navyo kuliko kushirikisha CCM tu na vyombo vyake vya habari



View attachment 2304298
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa
Mbona hujaeleza jinsi sensa inavyoenda vibaya badala yake umeongelea porojo za sheria ya Takwimu aliyotunga Jiwe na ambayo iko ignored?
 
Sensa imeharibiwa na idadi ndogo ya makarani. Watu takribani 200,000 wawafanyie tathmini ya kina vile takribani watu 60 m sawa na karani 1: 300 watu.
 
Sensa imeharibiwa na idadi ndogo ya makarani. Watu takribani 200,000 wawafanyie tathmini ya kina vile takribani watu 60 m sawa na karani 1: 300 watu.

42 per day? mbona average kaka?

Yaan Watu 42 ni wengi per day? binafsi hata watu 60 ningehesabu bila mizaha na kujipiga mapicha[emoji3]
 
Back
Top Bottom