Rais Samia tunaomba uwambie kweli ZESCO na Wazanzibari hakuna Umeme wa bure wagharamikie kama TANESCO na wabara.

Rais Samia tunaomba uwambie kweli ZESCO na Wazanzibari hakuna Umeme wa bure wagharamikie kama TANESCO na wabara.

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Baada ya Mh Rais kusema wazi kuwa wananchi waambiwe kuwa gharama za umeme sio 27,000 tena kama alivyotangaza Rais mwaka jana.
Hivi gaharama za kuunganishiwa Umeme zanzibar zikoje?
ZESCO imekuwa ikidaiwa madeni mengi sana ya Umeme na Tanesco na wamekuwa wakitegemea kusamehewa na wakisha samehewa maana yake mzigo wa Umeme unabebwa na wananchi wa bara na ambao wameambiwa wazi kuwa gharama zinarudi kama kawa na wana matozo kama yote.
Kuna kipindi walitishia kutumia vibatari wakilazimisha wapewe umeme bure na Tanesco

Ni wakati Muafaka Mh Rais uwambie wazi wazanzibari na ZESCO kama ulivyo wambia Tanesco na watanganyika kuwa Umeme gharama zirudi kama kawaida na hakuna umeme wa 27,000/=
Hivyo ni wakati muafaka wa kuwambia ZESCO kuwa hakuna umeme wa bure lazima wachangie gharama za Umeme kama watanzania wote.......
.................
 
Ahahhaaaa mkuu umegusa kidonda kibichi, issue ya umeme Zanzibar ni sawa na mtoto anayedaiwa ada skuli alafu mzazi hayupo nyumbani 😂😂!.
 
Zanzibar isiponeemeka kipindi hiki basi Tena!!!Nasikia na Spika wanataka waweke mzanzibar!
 
Zanzibar isiponeemeka kipindi hiki basi Tena!!!Nasikia na Spika wanataka waweke mzanzibar!
Usitake kuvuka daraja kabla hujalifikia!! Usipandikize hisia hasi bila sababu yoyote!! Ninajua hekima ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu ili kuepusha mgogoro ndani ya muungano ni kuridhia matakwa ya upande mwingine ili wasikwazike!! Japo hii ina kikomo chake!! Naona hicho kikomo kinakaribia, mama aongezewe hekima katika hili!! Hili bomu lisilipukie kwenye awamu yake!!
 
Huu upendeleo Kwa ZANZIBAR naona utavuka mipaka halafu tutawateka na ka kisiwa kao.
 
Ki ukweli huu muungano unatuumiza Sana watanganyika ila ndio hivyo wakutusemea wanawaza matumbo Yao na nafasi kwa ajili ya ndugu na watoto wao.
 
Huu Muungano wetu ni wa kipumbavu sana aisee inabidi tuambiwe ukweli kuna kitu gani kinachosababisha tuwanyenyekee namna hii hawa wazanzibar
 
Zanzibar haina tofauti na yule mdudu anayeitwa Kupe. 🐞Imejaa wananchi wavivu, wategemezi, walalamishi na watu wa kudeka deka muda wote.

Muda wote wanashinda maskani wakinywa urojo na kupiga umbea! Halafu kodi za Watanganyika ndizo ziwaletee maendeleo.
 
Umeme utaambiwa sio jambo la muungano

Hapa tunaongelea swala la watu kulipia umeme kama wafanyavyo watanganyika! Kwanini ZeCo isamehewe madeni halafu watanganyika waambiwe kuwa umeme wa 27,000 haupo na hauwezekani?
 
Ahahhaaaa mkuu umegusa kidonda kibichi, issue ya umeme Zanzibar ni sawa na mtoto anayedaiwa ada skuli alafu mzazi hayupo nyumbani [emoji23][emoji23]!.

Basi kama ni msamaha wapewe watanzania wote na si wazanzibari tuu kupitia ZECO
 
Zanzibar isiponeemeka kipindi hiki basi Tena!!!Nasikia na Spika wanataka waweke mzanzibar!

Waweke wamtakae lakini swala la umeme kupewa bure linafikirisha sana tena sana huku wabara wakiambiwa hakuna umeme wa 27,000!
 
Back
Top Bottom