Rais Samia: Tunazaliana wengi mno, mahitaji makubwa mno ndio maana kila tukiajiri Watumishi hawatoshi

Rais Samia: Tunazaliana wengi mno, mahitaji makubwa mno ndio maana kila tukiajiri Watumishi hawatoshi

Sasa hivi mnazaa tu watoto wadogo , kila siku nawaambia hakuna faida ya kuzaana labda wale matajiri .
Nchi hii tuna rasilimali nyingi ambazo zinatumika kuwaneemesha watu wachache hakuna shida ya watu kuongezeka ni jambo la kushangaza mgombea kununua pikipiki zaidi ya 700 za kufanyia kampeni ili huduma zingine zinaendelea kusuasua
 
Mh Rais, leo umenifurahisha.. umegusa moja ya sababu ya MSINGI kabisa ya UFUKARA wetu..yaani tunazaliana kama PANYA hasa hii Mikoa Simiyu , Kigoma na Singida.. elimu endelevu ya UZAZI wa MPANGO itolewe

Mwisho tuletee KATIBA MPYA iliyo bora na imarisha vyombo vya kuzuia UFISADI, nchi isonge mbele
 
Watanzania tuendelee kuzaliana lakini iwe kwa mipango hasa kwa kufuata mpango wa uzazi, kwa sababu tunatakiwa kuangalia wakati ujao kwa kupanga mipango madhubuti hasa ya kifamilia na kuwezesha maendeleo pia.

Kidumu chama Cha mapinduzi
CCM for life.
Samia mitano Tena
 
mkoa wa simiyu dogo wa miaka 29 ana watoto 5 hata nyumba hana ukimuuliza sababu za kuzaliana kwa pupa hana sababu za maana

wanaona kuzaliana sana kunakuza brand
Serikali haitekelezi majukumu yake ya kuelemisha na kuhamasisha watu ipasavyo kuhusu uzazi wa mpango.
 
Ni masimango kwa wanawake wenzie km rais anatamka kauli za kejeli namna hiyo manesi si watatuua na kutuulia watoto huko leba, ye anao wangapi? Aanze na wapemba wenzie, kakosa akili ya kuipanga serikali yake yupo kubwabwaja tu
 
Tukizaliana inamaana walipa kodi wanaongezeka na uchumi unakua,inakuaje iqngaliwe katika negativity... tu?
Anazingua.
 
Hivi kweli amesema haya au amesingiziwa au hio ni AI; Sitaki kuamini kabisa....

Kuna madaktari wangapi kitaa kwanini wasiongeze ajira ? Walishatangaza ajira wakakosa watu ? Pili hata kuwahudumia ni kwamba wamepunguza watu wanachangia BIMA, Tatu wakati wanachukua Tozo kwanini wasiseme basi Tozo tunapunguza sababu wachangiaji wamekuwa wengi sababu ya watu kuongezeka ?

Yaani Wanasiasa wa Karne hizi ni Full kusingizia watu lisingekuwa hili basi COVID, Ukame au hata vita vya Kule Ukraine (yaani tunalalamika kuhusu Ukraine kuliko Ukraine wenyewe)
 
Shida sio kwamba kuzaliana hii Nchi ni vile umekoswa viongozi wenye maono tu. Maana tuna Kila kitu isipokuwa akiri
Ishu ya msingi kuzaliana ,kunq nchi zina population pressure kubwa kuliko Tanzania, But sie tuna resources kibao but hakuna maono ,uroho, ubinfsi.

I think kuna mtu ataingiza kukubalian na wakina Gates foundation kuhusu depopulation, Yuko sawasawa na Dada Tina yule muimbaji ( Wanawake wasizae, she said)
 
Nimeelezea njia ya kutatua changamoto hii ya uchache wa watumishi katika sekta ya umma katika stories of change 2024.
 

Attachments

  • Screenshot_20240731-161251.jpg
    Screenshot_20240731-161251.jpg
    180.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom