#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuagiza chanjo ya COVID19

Amesema ni muhimu iwepo ili anayetaka kuchoma aipate kiurahisi kwa kuwa matumizi ya chanjo hiyo itakuwa hiyari

Amesema hayo alipokuwa katika Kongamano la Kumbukumbu ya Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa

Samia Corona.jpg
 
Najiuliza hii chanjo kutolewa kwa hiari hakuwezi kuleta madhara huko mbele ya safari kwa wale watakaokuwa hawajachanjwa kuendeleza maambukizi?

Sikumbuki kama na huko kwingine duniani hiyo chanjo ilitolewa kwa hiari, mfano tunaona nchi kama Uganda, japo wapo waliochanjwa lakini bado Corona inawasumbua.

Hii Corona tusipoichukulia serious tutakuwa tunajaza maji kwenye ndoo iliyotoboka, kama chanjo wanaziamini hazina madhara, kwanini zisiwe lazima, wengine wataelewa umuhimu wakishachanjwa.
 
Good, tuache maigizo kwenye afya za watu, mara sijui mapapai, mbuzi, kujifukiza, tangawizi, maembe na ujinga mwingine.
Eti papai lina corona!! Hivi ukichukua sample ya mkojo ukaweka kwenye kipimio cha malaria unategemea majibu yatakuwaje? Kwanza kipimio chenyewe unakuwa umekichanganya kabisa! Jiwe sijui chemistry yake alisomea wapi.
 
Watuletee tu maana ni kawaida kutufanya panya wa maabara, leteni COVAX tuchome nyie mmeishachoma Pfizer!, kama ARV tunazotumia sisi ni Made in India na Pakistan wakati wenyewe wanameza Made in Italy na UK alafu wanatwambia zote ni Sawa tu!
 
Ni ipi hasa inayoletwa Pfizer,Johnson&Johnson au Moderna?

Au ni Ile Abdala ya Cuba ama bado ni Siri.

Badala ya kuendelea na kauli kama,"Itakuwa hiari" ni vyema elimu itolewe kuhamasisha watu waone umuhimu wa hiyo chanjo.
 
... Mh. waziri wa fedha keshafafanua inaletwa chanjo ile ile waliyochanjwa Biden na Trump! Mbona hamuelewi?
 
Ni ipi hasa inayoletwa Pfizer,Johnson&Johnson au Moderna?

Au ni Ile Abdala ya Cuba ama bado ni Siri.

Badala ya kuendelea na kauli kama,"Itakuwa hiari" ni vyema elimu itolewe kuhamasisha watu waone umuhimu wa hiyo chanjo.
... now you are talking! Tunaongea lugha moja sasa!
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuagiza chanjo ya COVID19

Amesema ni muhimu iwepo ili anayetaka kuchoma aipate kiurahisi kwa kuwa matum,izi ya chanjo hiyo itakuwa hiyari

Amesema hayo alipokuwa katika Kongamano la Kumbukumbu ya Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa

Mataga watakuua mama, kuwa nao makini, mlichelewa kuileta mpaka corona ikamuua Joni Kilevi makufuli
 
Nyungu SEASON 1

Nyungu SEASON 2

Nyungu SEASON 3

SHIKAMOO KAKA JAFO!
 
Good, tuache maigizo kwenye afya za watu, mara sijui mapapai, mbuzi, kujifukiza, tangawizi, maembe na ujinga mwingine.
Hhaahahhaa...!! Wanaosema wanataka kuitoa CCM waitoe ila Mama yetu watuachie hapohapo alipo
 
... asante sana Mheshimiwa Rais; harakisheni hizo chanjo watanzania tunateketea! Asiyetaka akafie mbali; hutaki tiba tupishe.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuagiza chanjo ya COVID19

Amesema ni muhimu iwepo ili anayetaka kuchoma aipate kiurahisi kwa kuwa matum,izi ya chanjo hiyo itakuwa hiyari

Amesema hayo alipokuwa katika Kongamano la Kumbukumbu ya Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa

Hongera sana Mama kwa moyo wa kishujaa wapendwa wetu wengi wamekwenda na Corona sababu wataalam hawakupewa nafasi zikabaki siasa na kubrainwash watu ambao mpaka sana kuna wengine wako gizani
 
Back
Top Bottom