#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

Najiuliza hii chanjo kutolewa kwa hiari hakuwezi kuleta madhara huko mbele ya safari kwa wale watakaokuwa hawajachanjwa kuendeleza maambukizi?

Sikumbuki kama na huko kwingine duniani hiyo chanjo ilitolewa kwa hiari, mfano tunaona nchi kama Uganda, japo wapo waliochanjwa lakini bado Corona inawasumbua.

Hii Corona tusipoichukulia serious tutakuwa tunajaza maji kwenye ndoo iliyotoboka, kama chanjo wanaziamini hazina madhara, kwanini zisiwe lazima, wengine wataelewa umuhimu wakishachanjwa.
Mkuu duniani karibu kila sehemu chanjo ni hiari. Ulaya, Marekani na Asia kote ni hiari. Uzuri ni kuwa nchi nyingi watu wana akili hivyo wamejitokeza kuchanja. Upinzani wa kijinga naona upo Bongo tu. Nadhani hata wanaopinga ni wajinga wachache tu. Utashangaa zikija watu watakavyozigombania.
 
Good, tuache maigizo kwenye afya za watu, mara sijui mapapai, mbuzi, kujifukiza, tangawizi, maembe na ujinga mwingine.
Kwani kuna mtu alilazimishwa kutumia hizo tangawizi na malimao?
 
Corona ni shetani anayetafuna mamia ya watu, na haitakaa iishe hii, inawachukia zaidi wanaotoka hadharani kuikemea na kuonyesha mpango wake muovu dhidi ya dunia ya leo

Wasema ukweli wote watatafunwa na corona kwa njia yoyote Ile, lengo lake ni ili ipate nguvu kote duniani na kupunguza idadi ya watu ili kuendana na rasilimali za dunia ya leo, Sure, Biblia ni kitabu cha ajabu sana haijapata kuwako kitabu kingine chote chenye kufunua mambo ya kabla ya miaka elfu

Hii korona, haitakaa iishe, itakuwa kama ukimwi na malalia, kirusi chenye uwezo wa kujibadirisha mara nyingi zaidi, Ni hatari na changamoto kwa wabobevu wa sayansi ya tiba

Mungu Tulinde na uwape uwezo zaidi wanasayansi hasa wa Kiafrica ili tuondokane na mpango wa kibinadamu kwa nguvu za lusifa
 
Kwani kuna mtu alilazimishwa kutumia hizo tangawizi na malimao?
Hata ingekuwa lazima bado ukitumia utaonekana mwendawazimu tu. Kuna mambo mengine common sense tu inakuambia huu ni ujinga. Mwendazake alikuwa amegeuza nchi ikawa kama ya mataahira watu wanakimbizana na malimao na tangawizi!
 
Najiuliza hii chanjo kutolewa kwa hiari hakuwezi kuleta madhara huko mbele ya safari kwa wale watakaokuwa hawajachanjwa kuendeleza maambukizi?

Sikumbuki kama na huko kwingine duniani hiyo chanjo ilitolewa kwa hiari, mfano tunaona nchi kama Uganda, japo wapo waliochanjwa lakini bado Corona inawasumbua.

Hii Corona tusipoichukulia serious tutakuwa tunajaza maji kwenye ndoo iliyotoboka, kama chanjo wanaziamini hazina madhara, kwanini zisiwe lazima, wengine wataelewa umuhimu wakishachanjwa.
Kwa kuanzia ni vema iwe hiari. Tumegawanyika sana kwa hili.
 
Haya mtaaalam wa chanjo naona uko kaini kutoa elimu 🤣 🤣 🤣. naona elimu yako imekukomboa kweli kweli.
Kuna watu wakishaugua ndo wanakimbilia kutafuta chanjo......sasa hiyo chanjo itakusaidia nini zaidi ya kuzidisha ugonjwa.
 
Corona ni shetani anayetafuna mamia ya watu, na haitakaa iishe hii, inawachukia zaidi wanaotoka hadharani kuikemea na kuonyesha mpango wake muovu dhidi ya dunia ya leo

Wasema ukweli wote watatafunwa na corona kwa njia yoyote Ile, lengo lake ni ili ipate nguvu kote duniani na kupunguza idadi ya watu ili kuendana na rasilimali za dunia ya leo, Sure, Biblia ni kitabu cha ajabu sana haijapata kuwako kitabu kingine chote chenye kufunua mambo ya kabla ya miaka elfu

Hii korona, haitakaa iishe, itakuwa kama ukimwi na malalia, kirusi chenye uwezo wa kujibadirisha mara nyingi zaidi, Ni hatari na changamoto kwa wabobevu wa sayansi

Mungu Tulinde na uwape uwezo zaidi wanasayansi hasa wa Kiafrica ili tuondokane na mpango wa kibinadamu kwa nguvu za lusifa
Unaweka ulokole kwenye mambo ambayo Mungu amekupa akili?
 
Ni vizuri kuanza na hiari kisha inakuwa sharti kwa wanaotoka nje ya nchi na wanaoingia. Itasaidia sana.
 
Chanjo siku zote ni hiari, kinachohitajika ni elimu kwa umma, kampeni za kuhamasisha wananchi kuipokea chanjo, kinachohitajika ni majority wawe wamechanjwa ili kufikia "herd immunity"
Sawa kabisa mkuu
 
Ni hiari nchi nyingi lakini kule Houston, Texas USA kuna Wafanyakazi wa hospital ikiwemo nurses na doctors waligoma kupewa chanjo kwa kudai kwamba ni miili yao hivyo wana haki ya kukataa chanjo. Muajiri akawaambia nyinyi mnadeal na Wagonjwa directly hivyo hamuwezi kuwa chanzo cha kuwaambukiza wagonjwa wetu wenye magonjwa mengine hivyo ni lazima mchanjwe au mtafukuzwa kazi. Wakagoma na kibarua kikaota manyasi.
Huu ugonjwa ukiendelea hadi 2022 basi Waajiri wengi wanaweza kabisa kulazimisha waajiriwa wao wapate chanjo au watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Najiuliza hii chanjo kutolewa kwa hiari hakuwezi kuleta madhara huko mbele ya safari kwa wale watakaokuwa hawajachanjwa kuendeleza maambukizi?

Sikumbuki kama na huko kwingine duniani hiyo chanjo ilitolewa kwa hiari, mfano tunaona nchi kama Uganda, japo wapo waliochanjwa lakini bado Corona inawasumbua.

Hii Corona tusipoichukulia serious tutakuwa tunajaza maji kwenye ndoo iliyotoboka, kama chanjo wanaziamini hazina madhara, kwanini zisiwe lazima, wengine wataelewa umuhimu wakishachanjwa.
 
Kuagiza ama kupewa bure na COVAX facility?
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuagiza chanjo ya COVID19

Amesema ni muhimu iwepo ili anayetaka kuchoma aipate kiurahisi kwa kuwa matum,izi ya chanjo hiyo itakuwa hiyari

Amesema hayo alipokuwa katika Kongamano la Kumbukumbu ya Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa

Kuna watu wakishaugua ndo wanakimbilia kutafuta chanjo......sasa hiyo chanjo itakusaidia nini zaidi ya kuzidisha ugonjwa.
Chanjo ya korona inaanza kufanya kazi baada ya angalau wiki mbili tangu upate chanjo ya kwanza na kinga bora zaidi inakuwa wiki mbili baada ya chanjo ya pili. Hizi ni zile zinazotakiwa chanjo mbili.
 
Ni kweli mimi ni mlokole, nakushauri, fanya yako na ufuate unachokiamini na siyo ninachokiamini mimi, utapotea vibaya mno mkuu
Unasali kwa Gwajima yule porn-star tapeli? Kma unasali huko utakuwa umepotea sana.
 
Unasali kwa Gwajima yule porn-star tapeli? Kma unasali huko utakuwa umepotea sana.
Unasehemu gani ya maisha yangu wewe??

Mbona unataka kuwa mjinga sasa! aisee, usitake kuiga maisha yangu, niwe nasali kwa gwajima ama wapi, inakuhusu nini wewe, inakunyima nini, au ni jambo lipi linakuhusu moja kwa moja na linakupa shida kwa kusali kwangu huko?
 
Chanjo ya korona inaanza kufanya kazi baada ya angalau wiki mbili tangu upate chanjo ya kwanza na kinga bora zaidi inakuwa wiki mbili baada ya chanjo ya pili. Hizi ni zile zinazotakiwa chanjo mbili.
Mzee mdiliko, hakuna cha chanjo mbili wala tatu.....hiyo ni biashara endelevu ya mabeberu, yaani itafikia watu wataishi kwa kutegemea chanjo ambayo utatakiwa kudunga kila baada ya miezi 6 na hapo ndo beberu atapiga pesa kwani hatatoa chanjo za msaada kama anavyofanya sasa. Na ataweza ku enforce hii kwa kuweka restrictions kwenye usafiri kama inavyotokea sasa kwenye ndege na ku access huduma mbalimbali za kijamii, that is a real trap.....
 
Back
Top Bottom