Nimejiridhisha kabisa kwamba, siwezi kukuulaumu tena, kwani sio wewe, nitamlaani huyo mdudu anayejulikana kwa jina la mjinga anayekula ubongo wako!
Huyo kakukalia vibaya sana, amekufanya usijitambue, amekufanya kuwa mbea na mtu usiyechambua ni kitu gani unaweza okota hapa ili kikusaidie
Amekufanya uone Jambo la kawaida kupoteza mb zako kuongelea ujinga kwa sababu ya mdudu anayekaa kichwani kwako (mjinga) nitamlaumu yeye na siyo wewe
Umekosa faida kwa sababu ya mdudu huyu (mjinga) eeh!! haikubaliki, kwani unaweza kuepukana naye tena na ukawa kijana safi mwenye akili zako
Cha kukushauri, acha umbeya na udaku, fuatilia yale yanayokufaa, yenye kuondoa huyo mdudu wako, kijinga tupa kule