#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

Aliyekwambia herd immunity inategemea chanjo ni nani? ni asilimia ngapi ya watu wamewahi kuchanja malaria.....nenda kawapime kama hawana hiyo kinga ya malaria, tatizo mnashadadia mambo ambayo hamna uelewa hata tone....
Mbona unatoka nje ya mada tena, naona hujui hata herd immunity ni kitu gani.
 
Haya wale panya wa majaribio someni hiyo fomu, serikali yenu tayari imejivua kuhusika kwenye madhara yoyote yatakayojitokeza. Hii inamaanisha hiyo chanjo bado ipo kwenye hatua za majaribio, kwa sababu chanjo ambazo zimepata final approval hutakiwi kujaza consent form. Makampuni ya chanjo yanakwepa kulipa fidia wahusika watakaojitolea kwenye majaribio ya chanjo, yaani kinachofanyika hapa ni uhuni mtupu....
 
Ujinga ni mwingi kwa sababu walidanganywa na Magufuli. Ikitolewa elimu wengi watabadilika. Siku zote sula la matibabu linatakiwa liwe ni hiari. Ila suala la lazima linaweza kutumika iwapo itaonekana kuna ulazima. Imagine nchi nyingine karibu zote zichanje ila Tanzania iwe kikwazo na kusababisha virus mutation kushika kasi. Hapo kutakuwa na ulazima wa kuingilia. Hata sasa hivi ugonjwa kama TB mtu akionyesha kutoka kufuata matibabu kwa hiari na akawa tishio kwa wengine sheria inaweza kutumika kumlazimisha atibiwe.
Ndio maana kule mwanzo nikasema bora hii kitu iwe lazima, tusipoteze muda wakati Corona bado inatumaliza.
 
Haya wale panya wa majaribio someni hiyo fomu, serikali yenu tayari imejivua kuhusika kwenye madhara yoyote yatakayojitokeza. Hii inamaanisha hiyo chanjo bado ipo kwenye hatua za majaribio, kwa sababu chanjo ambazo zimepata final approval hutakiwi kujaza consent form. Makampuni ya chanjo yanakwepa kulipa fidia wahusika watakaojitolea kwenye majaribio ya chanjo, yaani kinachofanyika hapa ni uhuni mtupu....
Hii itakuwa chanjo ya Kichina hii au ile ya CUBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ipi hasa inayoletwa Pfizer,Johnson&Johnson au Moderna?

Au ni Ile Abdala ya Cuba ama bado ni Siri.

Badala ya kuendelea na kauli kama,"Itakuwa hiari" ni vyema elimu itolewe kuhamasisha watu waone umuhimu wa hiyo chanjo.
Kuna uwezekano serikali isihusike na madhara yatakayotokana na matumizi ya chanjo hiyo. Kwa hiyo, uvumilie kidogo zije kikubwa upunguze 'mshawasha wa mambo'!
 
Sawa Mama lao.. waanze kuchanjwa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwanza.
 
Unazidi kutoka nje ya mada, wacha ujuaji dogo.
Unalialia nini sasa, peleka tackle ushindiliwe sindano ya sumu wambie wakupe na ya kunywa......unalilia herd immunity ya nini wakati umeshaji protect....
 
Haya wale panya wa majaribio someni hiyo fomu, serikali yenu tayari imejivua kuhusika kwenye madhara yoyote yatakayojitokeza. Hii inamaanisha hiyo chanjo bado ipo kwenye hatua za majaribio, kwa sababu chanjo ambazo zimepata final approval hutakiwi kujaza consent form. Makampuni ya chanjo yanakwepa kulipa fidia wahusika watakaojitolea kwenye majaribio ya chanjo, yaani kinachofanyika hapa ni uhuni mtupu....
Kila sehemu unajaza hiyo fomu. Ni nchi zote. Hivi unajua hata unapoenda hospital kuna vigezo vyake unakuwa umekubalina navyo? Na fomu za kujaza ziko mbili. Ya kwanza inahusu hali ya afya yako kwa siku ile na kama umeshapata tena chanjo na mswali mengine ya allergy, na nyingine ni hiyo unayolalamikia.
 
Kila sehemu unajaza hiyo fomu. Ni nchi zote. Hivi unajua hata unapoenda hospital kuna vigezo vyake unakuwa umekubalina navyo?
Yaa, wajaze consent form ili majaribio yaanze......serikali imeshajitoa kuhusika na madhara yoyote.
 
Kama chanjo ya corona ingekuwa ndo Kinga Ulaya na Marekani wangekuwa hawafi mpaka Sasa,maana ndo zinatengenezwa huko.

Kama virus wa Corona angekuwa habadiliki Basi ingekuwa na maana.

Kama waliochomwa wangekuwa hawaambukizwi na kufa baada ya kuchanjwa ingeleta maana.

Kama nchi jirani waliochomwa ndo wanaoongoza kwa vifo pamoja lockdown Basi chanjo itakuwa kuwafurahisha wazungu tu ili utawala huu uonekane was maana machoni pa wazungu.

Kama Kuna Jambo baya litakalokuja kumharibia mama yetu legacy yake Basi ni hili la Corona.
Muda utatoa wapotoshaji endeleeni kumpotosha mama .
 
Hiki kinachozungumziwa hapa ni sawa na "side effects" na dawa nyingi kwa kawaida zina "side effects" kwa watumiaji, ila sio watumiaji wote hudhuriwa na hizo "side effects", sasa hapa ni jukumu la serikali kuwaelewesha wananchi wake wajue hili jambo ili wengi wasiogope kuchanjwa.
Sawa wao watujazie tu hizo consent forms, tusije kugeukana huko mbeleni......mara serikali hivi au vile, serikali haina pesa ya kulipa watu fidia. Huo mzigo makampuni ya chanjo yameukwepa, maana swala la kulipa fidia watu waliojitolea kushiriki kwenye majaribio ni la wale watafiti wanaofanya hayo majaribio...
 
Sasa kama majaribio yalishapita chanjo ikapata final approval, consent forms ni za nini sasa........mfano ukienda hospitali ukapewa dawa za kumeza, huwa unajaza consent form.
Kwa sababu chanjo inaweza kuwa na side effects kwa baadhi ya watumiaji.
 
Sasa kama majaribio yalishapita chanjo ikapata final approval, consent forms ni za nini sasa........mfano ukienda hospitali ukapewa dawa za kumeza, huwa unajaza consent form.
Hata kama hupewi consent forms hospitali, lakini bado hizo dawa unazopewa ukienda kuzitumia zinaweza kukudhuru.
 
Back
Top Bottom