Rais Samia tusaidie, Uteuzi wa DCI Kingai, Watanzania tunaenda kuzikwa wazima wazima

Rais Samia tusaidie, Uteuzi wa DCI Kingai, Watanzania tunaenda kuzikwa wazima wazima

Huu uteuzi ni Mzuri sana namuunga mkono Samia.

Nadhani ile ahadi ya kuwa kupe badala ya chawa ikifika oktoba inaanza kutimia taratibu.
 
Uteuzi wa huyu mtu umetustua sana hasa tukiwaza matendo na utendaji wake uliojaa 'walakini" Anyway, Mola atatunusuru na kutupa wepesi kwani Mola hajawahi kuwaacha watu wake waumizwe.
 
Ndio maana na sisitiza ukipata nafasi ya kula mali ya umma kula. Ukipata nafasi ya kukwepa TRA we kwepa. Hii nchi haina maana kama hujawai kua kiongozi au huna pesa
 
View attachment 2298251
Shikamoo Rais Samia

Huyu Kingai anaenda kutumaliza, visasi vingi na atahakikisha wabaye wake wanakipata cha mtemakuni.

Kingai haijui hata PGO, atakuwaje Mkurugenzi wa Upelelezi? Twafwa.

Kesi dhidi ya Mbowe ya Ugaidi, nilitegemea imfumbue macho Rais ili ajue waliomzunguka. Naamini rais kashauriwa Vibaya. Tusimlaumu sana sababu bado anayo nafasi ya kubadilisha.

Huu ndo Ushauri Lukuvi anampa rais wetu? Kingai? Huyu wa Kinondoni au yupo Kingai mwingine Jeshini?

Kama Afande Kingai angesoma PGO vizuri, angegundua kuwa SHTAKA linafunguliwa BAADA ya mtuhumiwa KUHOJIWA! Ikibainika "maelezo ya onyo" yanafichua KOSA, ndipo Jalada la Mashtaka HUANDALIWA. Kingai alipoulizwa na Wakili wa Serikali kwanini aliwatoa watuhumiwa Moshi kuwaleta DSM,

alijibu, "huko ndiko mashtaka yao yalipofunguliwa!" Sasa, ilikuwaje ukafungua mashtaka ya hawa Vijana wakati bado hawajakamatwa, na wala KUHOJIWA!

PGO isomwe jamani, tena isomwe vizuri! Mnadhalilisha hili Jeshi.

Kingai alimnyima dhamana mtu aliyehoji kutaka kujua kama Hayati Magufuli anaumwa. Eti hakupasa kuhoji akakamatwa akapigwa na kunyimwa dhamana.

Aloshiriki kumdanganya rais Samia ili amteue Kingai, achukuliwe hatua.

View attachment 2298249
View attachment 2298250
Wengi wamesikitikia huu uteuzi,na hata alipoendelea kuwa RPC wa sijui kanda maalum watu hawakuwa na amani.Vyovyote iwavyo,lakini huyu jamaa kesi ya Mbowe ilimwacha mtupu Sana.
 
Polisi hawafungui mashtaka. Mashtaka yanafunguliwa na DPP.

Polisi wanapokea malalamiko na wakiona ni malalamiko ya jinai wanayaandika kwenye daftari la taarifa na kukupa namba ya taarifa (RB). Malalamiko yanazaa tuhuma. Tuhuma ndo zinakufanya ukamatwe na Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Mahojiano yatafanyika kule ambako malalamiko yalipokelewa.

Kwa hiyo hapo inatakiwa ujiongeze uelewe kwamba hayo ambayo huyo afisa wa polisi aliyaita "mashtaka" alikuwa anaaminisha malalamiko. Kama kukosea ni amekosa lugha tu, ila sio utendaji. Kama malalamiko yalipokelewa Dar, na mlalamikiwa yuko Moshi atakamatwa na kupelekwa Dar akahojiwe.
Ndugu kwa hali hii siyo kwamba alikosea lugha,alikosea msamiati/sentensi sahihi kueleza hilo.Na kwakuwa ni kiongozi mkubwa hatuwezi kuichukulia kawaida.Lazima tumshushe vyeo!
 
Yaani kuteuliwa tu vijana wake aliowatrain akiwa RCO Arusha wamemchoma katibu wa Chadema kisu wakijua mtetezi wao yupo atawakingia kifua.

mwendazake si keshakufa haya mambo yanatoka wapi tena!!!!
 
Tabia ya mtu kuwa chawa huwa inamaanza namna hii, we ni chawa bana
 
Aliyempelekea jina la Kingai mama kachemsha, lakini mama nawe geuza tuu huo mkeka sisi tutakuelewa. Huyu mtu siyo hiyo nafasi haimfai.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Nafurahi sana kwamba machadema mnateseka!

Kingai mi 5 tena!

By the way.. Mbaya wenu si alishakufa na sasa mnapumua?
Hacha maneno ya kujikweza, nchi nzima inapata cha moto.
Mitozo, kodi, mafuta, kupanda vitu bei inampiga kila mtu.
Mbweha wewe
 
Daah..
Kumbe kuna baadhi waadilifu bado wamo!
Yaani Kingai naye ni wa kuteuliwa kushika wadhifa nyeti[emoji849][emoji848]
Ukute alikuwa anatekeleza uovu kwa maelekezo toka juu!!!
Hapo ndio mtaamini kuwa wanganga wa jadi wapo, uyu samia kalogwa uyu
 
Polisi hawafungui mashtaka. Mashtaka yanafunguliwa na DPP.

Polisi wanapokea malalamiko na wakiona ni malalamiko ya jinai wanayaandika kwenye daftari la taarifa na kukupa namba ya taarifa (RB). Malalamiko yanazaa tuhuma. Tuhuma ndo zinakufanya ukamatwe na Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Mahojiano yatafanyika kule ambako malalamiko yalipokelewa.

Kwa hiyo hapo inatakiwa ujiongeze uelewe kwamba hayo ambayo huyo afisa wa polisi aliyaita "mashtaka" alikuwa anaaminisha malalamiko. Kama kukosea ni amekosa lugha tu, ila sio utendaji.

Kama malalamiko yalipokelewa Dar, na mlalamikiwa yuko Moshi atakamatwa na kupelekwa Dar akahojiwe.
Usicheze na makosa yako halafu matokeo ya makosa yako abebe mwingine..!!
 
Polisi hawafungui mashtaka. Mashtaka yanafunguliwa na DPP.

Polisi wanapokea malalamiko na wakiona ni malalamiko ya jinai wanayaandika kwenye daftari la taarifa na kukupa namba ya taarifa (RB). Malalamiko yanazaa tuhuma. Tuhuma ndo zinakufanya ukamatwe na Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Mahojiano yatafanyika kule ambako malalamiko yalipokelewa.

Kwa hiyo hapo inatakiwa ujiongeze uelewe kwamba hayo ambayo huyo afisa wa polisi aliyaita "mashtaka" alikuwa anaaminisha malalamiko. Kama kukosea ni amekosa lugha tu, ila sio utendaji.

Kama malalamiko yalipokelewa Dar, na mlalamikiwa yuko Moshi atakamatwa na kupelekwa Dar akahojiwe.
Kwa maelezo yako Ofisa wa polisi hajui malalamiko na mashtaka na ndo anakuwa DCI. Hii nchi ngumu Sana
 
Kama kingai kapewa uDCI basi hats makonda na sabaya watateuliwa tena.

Maji hufuata mkondo wake.

Udhalimu Haina aibu Wala Soni.

Kingai for uDCI what a waste.

Mtu asie na hata miiko ya kiungozi Wala ya haki za binadamu unamteua kuwa mpelelezo mkuu.

Ama kweli madaraka yanaleta UPOFU wa akili.

Hatutaka kusikia once mmestaafu mkisema mnajutia hili na lile wakati mnafanya vitu intentionay.makusudically.

Anyway. Wasiwasi ndio akili
 
Back
Top Bottom