Tulisha mshauri Raisi Samia na kumuonya kwamba anahujumiwa. Anahujumiwa na makundi mawali
1. Viongozi wanaotaka madaraka
2. Viongozi sio wengine wa vyombo vya usalama ambao wanataka kuleta fujo ili Raisi awaone wenyewe kwamba ni lazima awategemee. Wata zusha kila mbinu ili kumtisha Rais awaone wao ndiyo tegemezi
Ushauri wangu
1. Ukigundua uzembe na hujuma ndani ya usalama waseme wazi badala ya kubadilisha kwa sirisiri
2. Usalama na Polisi wasijihusishe na siasa kama katiba inavyo sema
3. Wahujumu ndani ya CCM watajwe wazi
4. Tume huru ipewe uhuru na katiba iendelee kwa asilimia 100% woga wako una cost taifa
5. Usionee huruma rushwa ya aina yeyote
2020 kuna mapolisi walitangaza Nia ya kugombea ubunge kule Singida kupitia CCM. Katiba inakataza polisi kuingia kwenye siasa . Cha ajabu bado wapo kazini na wanapandishwa vyeo
Polisi alijitangaza kama kada wa CCM ni dhahiri kuwa ataua kila asiye mwana CCM.
Mwishowe watauana wenyewe kwa wenyewe kwa kutuhumiana Kuwa ni ama wapinzani au kwa kuua ndugu wa polisi au mwanajeshi kama ilivyotokea wakati fulani kule Kenya,pale askari wa kabila la Wakikuyu walipokua wanawaua kwa makusudi wajaluo waliokua wanaandamana kupinga ushindi wa Mwai Kibaki.
Lakini pia ilikua ni kosa kubwa sana kumweka Wambura,Kingai na Awadhi kuongoza Jeshi la Polisi. Hao Watu hawana mbinu zaidi ya kuua na kutesa.
Chadema wanakosa mbinu kwa sababu walishindwa mapema kusimama na wananchi waliopoteza ndugu zao kama akina Akwilini , Mwangosi,Alfonsi Mawazo na wengine wengi kule Arusha.
Mfano Wanapopotea Watu ni vyema Chadema ikahamasisha wanachama mikoa yote na wilaya ili kukusanya michango ya Rambirambi na kuikabidhi kwa familia .
Watu wengi wanaogopa kujitokeza kwa sababu hakuna faidi yoyote lakini Fedha zikiwa zinatolewa kuwafariji ndugu na kulea watoto itakua ni mwanzo mzuri wa kujenga ujasiri kwa vijana kupigania haki. Hata hao wauaji wanaofadhiliwa na CCM wanafanya unyama huo kwa sababu ya pesa na madaraka . Hao wauaji wengi ni mabilionea mana wakati mwingine wanawalazimisha mateka kutoa pesa zote benki .
Uchaguzi huu unaokuja ni vyema wapinzani kama hawawezi kuwadhibiti wauaji na waporaji wa CCM basi waachane nao. Waamue kufanya maandamano makubwa siku zote za uchaguzi na kuhakikisha nchi nzima uchaguzi haufanyiki mpaka katiba mpya ipatikane hata kama ni 2027 basi uchaguzi ufanyike 2028.
Vinginevyo pesa za waarabu ni nyingi sana na zitawaua wapinzani wote. Bora JPM mana hakuwa na pesa za kutoka nje kwa waarabu wanaofadhili maugaidi wakishirikiana na Marekani.
Na kwa sasa kuna kuua kwa mgongo wa kisiasa lakini nyuma yake kuonekana kuna utanganyika ,uzanzibar ,Udini na uchama cha mapinduzi na kuhujumiana .
Siamini kama polisi peke yao wanaweza kuua watu mchana kweupe halafu usalama wa Taifa na JWTZ wasiwaone na kumpa Taarifa raisi Kuwa polisi wanaua watu.
Kwanza Polisi ni waoga na wanachukiwa na Taasisi nyingine na pia majeshi mengine ikiwemo TISS.
Lakini pia inaonekana kuna chuki ilijijenga kwa Wazanzibari wakati ule wa Mauaji kule pemba . Waliofanya mauaji kule Zanzibaaa walikua ni Wa kutoka bara na waliyafanya mauaji mchana kweupe dhidi ya Wanachama wa CUF ikituhumiwa Kuwa ni chama cha kidini.
Sasa kibao kimegeuka . Hawataki wetu wa pwani wajiunge na Chadema .
Tafakarini mtaelewa tu.
Kama Chadema hamutaweza kudhibiti hujuma na kuuawa na CCM achaneni na uchaguzi . Mtauawa wote hawa jamaa wamepewa pesa nyingi sana na waarabu. Wanamtisha mpaka Mungu Kuwa hawezi kuwafanya chochote zaidi ya wao kukaa madarakani kwa lazima na sio Mungu akipenda. Yale mambo ya kusema watawala wanawekwa na Mungu kwao hayapo.
Watu wasiomuogopa Mungu hata kidogo ni hatari sana. Hawana tofauti na Majambazi . Bora hata magaidi mana yanajinasibu Kuwa yanatetea haki lakini hawa ni kama majambazi yanapora na kuua alimradi yaibe na kupata pesa na mali.