Rais Samia: Tutaendelea kukopa kwaajili ya maendeleo ya Tanzania

Rais Samia: Tutaendelea kukopa kwaajili ya maendeleo ya Tanzania

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu jana katika uwekaji sahihi katika mradi wa SGR Rais Samia Suluhu alisema kuwa Pale tunapohisi pana faida tutaendelea kukopa. Kwa wanaosema awamu hii imekopa sana, waseme pia ndio awamu imejenga sana na kweli sisi ni mashahidi tumeona awamu hii imekopa sana lakini maendeleo yanaonekana

Lakini pia Rais Samia Suluhu aliongeza kuwa "Ukiacha Reli kuna mambo mengine kadhaa yamefanywa ndani ya awamu hii na tusingeweza kufanya lazima tukope na tunakopa ili tujenge leo kwa maendeleo endelevu ya leo na baadae, kwa hiyo kila pale tunapohisi pana faida, tutaendelea kukopa"

Kwaiyo mikopo itaendelea kwaajili ya maendeleo ya Tanzania
 
Kukopa si tatizo.

Mataifa yanayoongoza kwa utajiri ndiyo yanaongoza kwa madeni.

Na Tanzania kwa kuangalia Debt to GDP ratio, hatujakopa sana. Angalia link hapo chini.

Tatizo ni matumizi ya mikopo kiufanisi wa kiuchumi, kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi, kuweza kulipa deni bila kuathiri shughuli za kijamii, kuepuka kulipa riba kubwa, hususan baada ya grace period kuisha, kuweza kukopa bila kuathiriwa na economic espionage na sabotage za economic hitmen, kuepuka habari za kukopa deni moja ili ulipe deni jingine, hapo ndipo penye tatizo.

 
Kukopa deni moja ili ulipe jingine ni viable economically..wachumi huita conversion,unakopa kwenye grace period ndefu na riba ndogo unalipa kwenye riba kubwa na grace period fupi,Kama mikopo aliyokopa magu kwenye commercial banks inatakiwa kufanyiwa conversion
 
Ehh Mwenye Enzi Mungu nakuomba tupia JICHO lako juu ya nchi yetu Tanzania [emoji1241][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]tutalia mpaka lini ehh Mungu mkuu, tunakuja madhebahuni mwako tukilia na kukuomba uione nchi yetu na uiponye ehh Mola wangu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Kujenga Kwa pesa za ndani kumbe ilikuwa swaga tu.....achaneni na tozo Sasa maana inaonekana hazina impact yeyote
Tozo zitakuwepo tu.

Maana hiyo mikopo riba zikianza kuhitajika baada ya grace period, hailipiki bila tozo, tena si tozo tu, tozo plus plus.

Kwa hivyo usitie shaka.

Waswahili walisema "Kukopa harusi, kulipa matanga".

Remmy Ongala akaongezea "Kukopa sukari, kulipa Polisi".
 
Tozo zitakuwepo tu.

Maana hiyo mikopo riba zikianza kuhitajika baadabya grace period, hailipiki bila tozo, tena si tozo tu, tozo plus plus.

Kwa hivyo usitie shaka.

Waswahili walisema "Kukopa harusi, kulipa matanga".
Ndiyo maana wanataka kurasimisha umachinga na mama ntilie,yaani Kodi kila mtu alipe
 
Mkumbushe mama kuwa huku mitaani hali ni tete,
1. Hela haipatikani mitaani,
2. Kwa anayefanya muamala tozo ndo anasimulia,
3. Kg ya mchele inauzwa 3500/
4. Maendeleo tunahitaji ila hali ya mtu binafsi ukiachana na mafisadi uchumi unakuwa ni shida tupu.
Mwisho tutakuwa zaidi ya Ghana asilimia kubwa ya mapato ya nchi inalipa madeni.
 
Mkumbushe mama kuwa huku mitaani hali ni tete,
1. Hela haipatikani mitaani,
2. Kwa anayefanya muamala tozo ndo anasimulia,
3. Kg ya mchele inauzwa 3500/
4. Maendeleo tunahitaji ila hali ya mtu binafsi ukiachana na mafisadi uchumi unakuwa ni shida tupu.
Mwisho tutakuwa zaidi ya Ghana asilimia kubwa ya mapato ya nchi inalipa madeni.
Kwa aina ya utawala uliokuwepo, sidhani kama kuna hata mmoja wao tu atakaye elewa hiki ulichokiandika hapa. Tena wakiona habari kama hizi, wataishia tu kukukejeli.
Mfano hapo kwenye bei ya mchele watakuambia; "kama unaona mchele ni bei ghali, kwa nini usiende kulima?"

Ila kiukweli mtaani kwa sasa kunawaka moto! Maana kuna mfumuko wa kutisha wa bei za vyakula. Na ikumbukwe chakula ni mahitaji ya lazima! Ni tofauti kabisa na bidhaa kama za nondo, cement, nk.
 
Back
Top Bottom