Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Rais Samia amesema anasubiria ripoti ya Timu aliyoiunda Kupitia mashirika ya Umma yanayoripoti Kwa Msajili wa Hazina Ili juyafutilia mbali Yale ambayo hayana Tija Wala faida. Amesema Mashirika Yatakayokufa basi wahusika wajiandae kufa nayo.
“Serikali tumeamua kufanya tathmini ya utendaji wa mashirika yote ya umma na yale ambayo Serikali ina hisa kubwa. Lengo la tathmini hiyo ni kubaini mashirika yasiyo na faida ambayo yameshindwa kujiendesha na yanaitia Serikali hasara.”
"Nasubiri taarifa ya mwisho, ya mashirika gani yanabaki, gani yanaondoka, na gani yasaidiwe vipi kufanya biashara, na siku tutakayoyatangaza...haya mashirika yakifa, wafe nayo, sitaki kusikia shirika linazorota,meneja anapiga suti nzuri anatamba mitaani, hatutaenda pamoja".
---
My Take
Safi sana mh.Rais hakuna kulea ujinga ujinga wa miaka Mingi ambako watu waligeuza Mali ya Umma ni mashamba ya Bibi.
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya Sh45.5 bilioni (Gawio la Serikali) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya benki hiyo.
Wakuu wa mashirika ya umma na taasisi ambazo Serikali inamiliki hisa kubwa, wanapaswa kukaa mguu sawa wakati Msajili wa Hazina akikamilisha tathimini ya pili ya ufanisi wake, ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataitumia kufanya uamuzi.
Wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa benki ya NMB Plc yaliyofanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City, Rais Samia na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu walieleza juu ya hatua wanazokusudia kuchukua kwa mashirika yanayosuasua kiutendaji.
"Serikali tumeamua kufanya tathimini ya mashirika yetu yote makubwa na yale ambayo tuna hisa nyingi, lengo ni kubaini yasiyo na faida, ambayo yanashindwa kujiendesha na ambayo yanaitia Serikali hasara," alisema Samia na kuongeza:
"Msajili wa Hazina amefanya tathimini ya awali ameniletea ripoti. Nikamwambia nenda kafanye tathimini ya pili, kwa hiyo wale mnaoshika mashirika TFS (Wakala wa Misitu Tanzania) Dos Santos nakuona, kajitizame vizuri ndani ya shirika lako pamoja na kwamba misitu ni wewe peke yako, kajitizame vizuri”.
Rais alisema ujumbe huo ni kwa wakuu wote wa mashirika, na kwamba hatua hiyo haina kurudi nyuma kwa kuwa kuna yatakayofutwa, kusaidiwa na mengine yatapewa miongozo namna ya kujiendesha ili yote yapate faida.
Alisema Serikali ilianzisha mashirika hayo ili yasaidie kuzalisha mapato na kuisaidia Serikali kubeba mzigo, siyo yenyewe kula serikalini.
"Kwa hiyo msajili vaa njuga, nimekupa baraka zote, nasubiri taarifa ya mwisho ya mashirika gani yanabaki, yapi yanaondoka na yapi yasaidiwe nini kufanya biashara na siku tutakayoyatangaza, yale ambayo tutatoa fedha mfukoni kuyasaidia, nitawaambia hayo mashirika yakifa mfe nayo," alisema.
Alisisitiza kuwa hatavumilia wala hataki kusikia shirika linazorota, ilhali meneja wake anapiga suti nzuri na kutamba mitaani.
Chanzo: Mwananchi
Kwanza aanze na kuiuza Tanesco kwa kampuni za Dubai au Qatar , wote mle ni mijizi na haifikiri chochote kuhusu maslahi ya nchi