Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itanunua sukari kutoka Uganda baada ya Rais Museveni kuomba suala hilo.

Aidha Rais amesema kauli ya Waziri kusema hatotoa kibali cha kununua sukari nje ya nchi ni 'Nonsense'

Ameyasema hayo katika kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda.

images

 
Zamani nilidhani ukipelekwa au ukihamishiwa wizara ya kilimo na uvuvi na ufugaji kama wazir umekomolewa. Nimekuja kujuwa hii wizara ni nzuri sana kwenye deal na upigaji. Hela ipo unaweza kupiga hela ndefu sana.

Wizara ya hovyo ambayo ukipangiwa kama waziri ni ya habari na michezo. Utambulia tu kuendeshwa kwenye viyoyoz ma V8 GX.
 
Wenzake wanapozuia kuagiza maana yake ni kulinda viwanda vya ndani.
Ila kwa ardhi iliyopo Tanzania hatukutakiwa kuagiza nje sukari,ngano,mafuta ya kupikia nk.ni kwa vile tu Mungu alituumba bila ubongo.
Sasa kuna viwanda gani Bongo vya kulinda aisee?Acha leseni zitolewe Mangi apige hela ndefu MAZOMBIE wapate sukari ya kutosha. Kila leseni Mangi na 'wariayee' wahakikishe wana 10% percent yao.

No Mercy kwa MAZOMBIE!
 
Samia ana akili kwenye masuala ya uchumi. That is excellent.

Maana yake ni kwamba kama uzalishaji wa ndani hautoshi toa kibali cha kuagiza nje ya nchi ili isijekutokea uhaba na bei kupanda halafu mlaji mwananchi akaumia.

Hii masuala ya kulinda viwanda vya ndani ni upuuzi uliotukuka, viwanda vya ndani wanatakiwa kuongeza uzalishaji na kuacha uzembe.

Ingekuwa mimi ndo mtunga sera, ningeweka import duty free kwa sukari ili hawa sugar producer wapate akili.
 
Kwa ni Kagera Sugar, Mtibwa, Kilombero, Kilimanjaro, Manyara sugar n.k wameshindwa kuzalisha sukari ya kutosha?

Kwa namna nyingine pia naweza kukubaliana na mama maana mafisadi hawachelewi kutengeneza genge la kusababisha uhaba wa sukari ili ipande bei.
 
Wenzake wanapozuia kuagiza maana yake ni kulinda viwanda vya ndani.
Ila kwa ardhi iliyopo Tanzania hatukutakiwa kuagiza nje sukari, ngano, mafuta ya kupikia nk.ni kwa vile tu Mungu alituumba bila ubongo.
Tukiacha kununua kwao na wao wanaacha kupitishia mizigo yao kwenye bandari yetu

Sema cha kushangaa ni kwamba sukari yenyewe uganda ni shida

Sasa wanatuuziaje sie wakati wenyewe haiwatoshi?

Hizo ndio siasa za afruca
 
Wenzake wanapozuia kuagiza maana yake ni kulinda viwanda vya ndani.
Ila kwa ardhi iliyopo Tanzania hatukutakiwa kuagiza nje sukari,ngano,mafuta ya kupikia nk.ni kwa vile tu Mungu alituumba bila ubongo.
Sasa kwani hao wenye viwanda vya sukari wamezuiwa kulima miwa zaidi ili kupata malighafi ya kutosha? Hadi sasa viwanda vya ndani vimeshindwa kukidhi mahitaji ya soko sasa kwanini iwe nongwa kuagiza kufidia upungufu!
 
Tukiacha kununua kwao na wao wanaacha kupitishia mizigo yao kwenye bandari yetu,
Sema cha kushangaa ni kwamba sukari yenyewe uganda ni shida
Sasa wanatuuziaje sie wakati wenyewe haiwatoshi?
Hizo ndio siasa za afruca
Wilaya ya Missenyi iliopo mpakani mwa Tanzania na Uganda ndipo kilipo kiwanda kikubwa cha sukari Tanzania cha Kagera Sugar. Cha ajabu ukienda mpakani kununua sukari, sukari ya Uganda ina bei ndogo kuliko sukari ya Tanzania inayozalishwa ndani ya Wilaya hiyo hiyo. Wazee wa dili wanachofanya, badala ya kununua sukari ya Kagera Sugar ya bei juu hapo wilayani, wananunua vifungashio vya kagera Sugar kisha wanaenda mpakani kununua sukari ya Uganda kwa bei chee na kuja kuiuza ktk wilaya hiyo hiyo ya Missenyi yenye kiwanda kikubwa Tz kwa bei juu.

Mimi naona bora wapewe kibali tu ili wakanunue sukari kwa bei chee na waje kutuuzia walaji kwa bei chee ili viwanda vyetu navyo vijifunze uzalendo wa kuwajali wateja wake ktk maswala ya bei, na sio wao kulindwa tu huku wakimkandamiza mlaji wa chini kwa kumpiga bei ya juu kama wanamkomoa. Soon bei ya sukari itashka mpakw TZS 2,000 per Kg
 
Kwa staili hii mama ndo Mana hatilii kipaumbele Suala la umeme wa uhakika.

Tatzo la viwanda vya ndani si malighafi bali ni umeme wa uhakika ndo maana ya kujenga power plant ya Bwawa la nyerere.

ajabu mama hashughuliki na hyo Zaid ya kushikilia sera nyepesi za kiuchumi zinazoangazia solution la muda mfupi tu.

Tujenge miundombinu ya upatikanaji wa umeme wa uhakika,viwanda vitazalisha KWA wingi na kuuza KWA bei Chee,so exportation itakua simple sana .

otherwise Basi ategemee kalamu itamuandika vibaya KWA future generation na kumshangaa yeye kama mkuu wa nchi KWA maamuzi kama haya
 
Kwa staili hii mama ndo Mana hatilii kipaumbele Suala la umeme wa uhakika.

Tatzo la viwanda vya ndani si malighafi bali ni umeme wa uhakika ndo maana ya kujenga power plant ya Bwawa la Nyerere.

Ajabu mama hashughuliki na hyo Zaid ya kushikilia sera nyepesi za kiuchumi zinazoangazia solution la muda mfupi tu.

Tujenge miundombinu ya upatikanaji wa umeme wa uhakika,viwanda vitazalisha KWA wingi na kuuza kwa bei Chee, so exportation itakua simple sana.

otherwise Basi ategemee kalamu itamuandika vibaya KWA future generation na kumshangaa yeye kama mkuu wa nchi KWA maamuzi kama haya
Wakati wa uyo aliekuwa akiweka kipaombele cha Umeme wa uhakika. Sukari ilikua kiasi gani?
 
Back
Top Bottom