Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Chama kimoja lakini mawazo na mitazamo kinzani. Ni jambo la afya kidemokrasia.

Nina hakika chadema wangeruhusu hili Chacha Wangwe angekuwa hai leo.
Kama chacha Wangwe aliuawa, kwanini kina Kingai Polisi yao na Tiss wako kimya?

Nadhani wangetumia kesi hiyo kumpoteza MBOWE kuliko hii kesi ya ajabu inayoendelea hivi sasa mahakamani
 
Samia ana akili kwenye masuala ya uchumi.. That is excellent.

Maana yake ni kwamba kama uzalishaji wa ndani hautoshi toa kibali cha kuagiza nje ya nchi ili isijekutokea uhaba na bei kupanda halafu mlaji mwananchi akaumia.

Hii masuala ya kulinda viwanda vya ndani ni upuuzi uliotukuka, viwanda vya ndani wanatakiwa kuongeza uzalishaji na kuacha uzembe.

Ingekuwa mimi ndo mtunga sera, ningeweka import duty free kwa sukari ili hawa sugar producer wapate akili.
Excellent kwenye uchumi ipi wewee,kama hujui unyamaze.
Hivi hii hata muwekezaji wa ndani kama bakhresa atafaidika na uwekezaji wake?

Umeme hamna wa uhakika,afu auze bidhaa KWA bei nafuu!!

Au na wewe ni kundi la mama anaupiga mwingi,mnafikiria KWA kutumia
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itanunua sukari kutoka Uganda baada ya Rais Museveni kuomba suala hilo

Aidha Rais amesema kauli ya Waziri kusema hatotoa kibali cha kununua sukari nje ya nchi ni 'Nonsense'

Ameyasema hayo katika kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda
Huyu Rais anavuka mipaka ya kuwaona waTZ wajinga, kwahiyo kiwanda cha sukari cha Bagamoyo kilichoasisiwa na JPM na kupewa nguvu na mfanyabiashara Bahkressa kife na watu wakose ajira?
 
Wakati wa uyo aliekuwa akiweka kipaombele cha Umeme wa uhakika.. Sukari ilikua kiasi gani?
Shekhe wangu Acha kutetea ujinga kisa shungi,hii ni nchi banaaa.Unajua kwann kuna sera za kulinda viwanda vya ndani?Unajua KWA nn bakhresa alipewa eneo na kuezeshwa kujenga kiwanda cha sukari Bagamoyo!

Huelewi haya mambo KAZI YAKO kuzunguka kila page tu Ili umtetee huyo mama ukiamini ni wa upande wako Abuu/baba abdurahman.

Mimi ktk mambo ya Jambo la nchi siwezi kumpendelea mtu KWA sababu dini yangu hainifundishi hivyo
 
Huyu Rais anavuka mipaka ya kuwaona waTZ wajinga, kwahiyo kiwanda cha sukari cha Bagamoyo kilichoasisiwa na JPM na kupewa nguvu na mfanyabiashara Bahkressa kife na watu wakose ajira?
Sera za kiuchumi zimewapitia kushoto,Viwanda vya ndani hawana umeme wa uhakika kuendesha migambo na ndo sababu kubwa ya bei kua juu,baada ya watu kupigia kelele kia viwanda ni ngumu kuviendesha KWA sababu ya umeme wa uhakika,ndo Mana Bwawa la umeme la nyerere likaamuliwa kujenga Ili kuwaezesha viwanda kupata umeme wa uhakika KWA ajili ya udhalishaji,Sasa leo hii wanatumia cheapest economy policy,eti wametelekeza hilo Bwawa,wanategemea kia uchumi utapanda,wanafikiri JPM kuukuza uchumi mpaka kuingia uchumi wa Kati ilikua kama kunywa maji eeeh.

Sasa hivi viwanda vitageuzwa magodown KWA ajili ya kuhifadhia bizaa TOKA nje na si uzalishaji na kutoa ajira KWA wananchi.

KAMA TAIFA,TUNARUDI NYUMA KWA KASI SANA
 
Matamshi yenyewe ya huyo asiyeona 'mantiki' yana mantiki ipi?

Ameeleza huyo waziri kwa nini alisema hivyo? Kuvimbishwa kichwa na nafasi ya uongozi siyo inayoleta mantiki kwa jambo lolote.

Kwa hiyo mawaziri waogope kufanya kazi na maamuzi kwa kuhofia boss atawaambia wasemayo hayana mantiki?
Yale yale ya Jiwe. Nchi inaendeshwa kwa matakwa ya rais na siyo kwa katiba na sheria. Hivi hawa watu wakipata urais akili huwa zinayeyuka?
 
Profesa huyu akose 'mantiki', halafu mantiki hiyo ipatikane kwa 'Maza Mizinguo'? Kweli vichekesho nchi hii haviwezi kuisha.

Kuukwaa urais tu, kunamwongezea mtu uwezo wa kujua mantiki na ipi siyo mantiki?


Duh 🙄 Nadhani Prof Mkenda anajuta kuongozwa na mtu asiyejua ABCD za uchumi.

Rais Samia kuwa Rais hakumfanyi kujua kila kitu,anachokiita none sense kina sense kubwa kweli kweli.Labda washauri wake wa uchumi na biashara wanamwingiza chaka kwa kumlisha matango pori.

Nchi hii haiwezi kuendelea kwa kuwafurahisha mataifa mengine au kuifanya soko la bidhaa za mataifa mengine wakati Sisi tuna ardhi kubwa
Mara tano au zaidi ya Uganda.
 
Nchi hii haiwezi kuendelea kwa kuwafurahisha mataifa mengine au kuifanya soko la bidhaa za mataifa mengine wakati Sisi tuna ardhi kubwa
Mara tano au zaidi ya Uganda.
Mwacheni rais afungue nchi 😆😆😆
 
Sukari ni rushwa tupu, dawa sio kuzuia kuingiza sukari maana ukweli tunahitaji sukari, dawa ni kuondoa utaratibu wa vibali na kuruhusu yeyote mwenye uwezo na kufuata viwango aruhusiwe kuingiza sio watu wachache tuu, kama deficit ni tani laki mbili basi sukari iruhusiwe kuingia mpaka hizo laki mbili, na hivyo viwanda vya ndani vipewe tax break na ruzuku ili kuviendeleza na vipewe kutokana na perfomance ambayo iko fair
 
Back
Top Bottom