Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Rais Samia: Tutanunua sukari kutoka Uganda

Tukiacha kununua kwao na wao wanaacha kupitishia mizigo yao kwenye bandari yetu

Sema cha kushangaa ni kwamba sukari yenyewe uganda ni shida

Sasa wanatuuziaje sie wakati wenyewe haiwatoshi?

Hizo ndio siasa za afruca

Mbona wanasema ya Brazil ni rahisi labda wanatuuzia hiyo baada ya ku repacked [emoji848][emoji848]
 
Kweli Tanzania Ni nchi ya kuagiza sukari Uganda? Tumekosa nn au Nini hatuna Cha kutufanya tusizalishe .umasikini wa fikra au....Kuna vitu vya kuagiza aisee sio sukari au mafuta

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu, umekuwa mgeni wa uhaba wa sukari nchini na wakati viwanda hivyo vipo miaka yote?

Haya, viwanda vya ndani vinalindwa, je vipi bei na upatikanaji wake kwa mlaji wa mwisho?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samia ana akili kwenye masuala ya uchumi. That is excellent.

Maana yake ni kwamba kama uzalishaji wa ndani hautoshi toa kibali cha kuagiza nje ya nchi ili isijekutokea uhaba na bei kupanda halafu mlaji mwananchi akaumia.

Hii masuala ya kulinda viwanda vya ndani ni upuuzi uliotukuka, viwanda vya ndani wanatakiwa kuongeza uzalishaji na kuacha uzembe.

Ingekuwa mimi ndo mtunga sera, ningeweka import duty free kwa sukari ili hawa sugar producer wapate akili.
.....kama uzalishaji wa ndani hautoshi toa kibali cha kuagiza nje..... (Na huu ndio ulikuwa msimamo wa Waziri wa Kilimo) unless there are UNKNOWNS-UNKNOWNS (or)KNOWNS-UNKNOWNS.
 
Ila serikali isiangalie kuimport suakri, zaidi isaport initaive za ndani kuzalisha suakri nyingi yenye ushinda. Kwanini uganda wanazlaisha sukari nyingi hadi wanakuja kuuzia tz?
Hapo kuna tatizo' poor political decisions'
 
Kweli Tanzania Ni nchi ya kuagiza sukari Uganda? Tumekosa nn au Nini hatuna Cha kutufanya tusizalishe .umasikini wa fikra au....Kuna vitu vya kuagiza aisee sio sukari au mafuta

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ukiona yale mabilion yanayotajwaga kwenye habari na press mbali mbali Tanzania imechukua mkopo Bil.360 mara Tanzania imepokea msaad wa Trillion kadhaa!

Hivi kwa mfano hio hela ikapelekwa kufanya jambo moja kwa ukamilifu hatuwezi kusogea kama Taifa?
Mfano tuseme mwaka huu hatufanyi chochote 90% ya hela zitazopatikana serikali inaenda kutandaza mabomba ya maji na visima nchi nzima hilo swala linabakia historia! 10% ndio ibakie pengine.

Kwanini tusifanye hivi kuliko kupeleka billon 10 mahali mara zimedokolewa tatizo haliishi yani! Inakuwa miaka nenda rudi swala la maji ni tatizo tu kila kukicha!
 
Nakisi ya sukari ya nchi Ni kiasi gani?
Tusije kuwapa watu upenyo wakaagiza sukari nyingi zaid ya inayo hitajika ikaua soko la sukari ya ndani.

Kama vibali vya kuagiza sukari vikitolewa kwa wafanya biashara na sio wamiliki wa viwanda vya sukari hali itakua mbaya Sana kwa viwanda maana sukari itaingizwa nyingi na kwa bei ndogo, hii itaipa changamoto viwanda kujiendesha.


Itafika mahali sukari ya ndani haitakua na soko, Ni hasara kwa wawekezaji na wanaoingia kwenye industry ya sugar production watarud nyuma.

Maelfu ya ajira yatapotea!
 
Sawa, labda akanunue kwa ajili ya kunywa chai yeye ikulu, sio sisi watz, hatuwezi kuua viwanda vyetu kwa mambo ya kijinga jinga tu
 
Tukiacha kununua kwao na wao wanaacha kupitishia mizigo yao kwenye bandari yetu

Sema cha kushangaa ni kwamba sukari yenyewe uganda ni shida

Sasa wanatuuziaje sie wakati wenyewe haiwatoshi?

Hizo ndio siasa za afruca
Waache, kwani biashara ni kuoneana huruma? Biashara inaangalia wapi napata the best na the cheapest, kama Mombasa ni cheapest basi aende huko!
 
Kwa staili hii mama ndo Mana hatilii kipaumbele Suala la umeme wa uhakika.

Tatzo la viwanda vya ndani si malighafi bali ni umeme wa uhakika ndo maana ya kujenga power plant ya Bwawa la nyerere...
Pia anahangaika sana na Chanjo, sikui kwanini
 
Duh 🙄 Nadhani Prof Mkenda anajuta kuongozwa na mtu asiyejua ABCD za uchum...
Mkuu 'Ngogo', tatizo kubwa si huyu kuwadharau watu wanaojua kazi wanazofanya; tatizo letu kubwa kama nchi ni kukosa mipangilio ya maendeleo yetu.

Uamzi unafanywa na serikali, ambamo huyu wa sasa alikuwa na nafasi ya juu kabisa kwenye uongozi, kwamba tunataka kuendeleza uzalishaji wa viwanda vyetu vya sukari.

Sasa sijui kama alishirikishwa kwenye uamzi huo au la! Leo, anageuka nyuma kabisa na kufanya kivingine kinyume kabisa na yale yaliyokwishaamriwa.

Hata kama haukuwa uamzi mzuri ambao yeye hakuunga mkono, maadam taifa limekwishaingia gharama na mipango inaendelea, ina "mantiki" gani kuvuruga juhudi hizo?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itanunua sukari kutoka Uganda baada ya Rais Museveni kuomba suala hilo

Aidha Rais amesema kauli ya Waziri kusema hatotoa kibali cha kununua sukari nje ya nchi ni 'Nonsense'

Ameyasema hayo katika kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda
Ameigeuza Tanzania shamba la bibi
 
Mtoto umleavyo ndio akuavyo. Nakumbuka Martin Shigela alimkoromea Uhuru Kenyatta akasifiwa na kichaa aliyekwenda zake. Huyu naye alifikiri kuwa angesifiwa!!
Huyu Mkenda alitoa maamuzi/kauli ya kile anachokiamini kwamba ni sahihi.

Hakutoa hayo maamuzi ili asifiwe na yeyote, kama umesikiliza maelezo yake alisema yuko tayari kuachia ngazi kwa huo msimamo wake.

Watanzania tumeshazoea siasa za kujikomba na kusifu pamoja na kuwaabudu maraisi wanaokuwa madarakani...hii ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi.
 
Hapo vip!!

Kwanza kwaheshima kubwa nawiwa kumtia moyo mama yetu mpendwa na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania dhidi ya majukumu mazito alionayo katika maisha yake.

Ninaamini kazi ya urais sio rahisi kabisa kama watu wanavyojiongelesha simple kwenye space isiyokuwa na P.O.Box.

Ni wazi rais ndio msemaji wa mwisho katika maswala mbali haijalisha litakufuraisha au halikufurahishi.

Sisi watanzania ni mashahidi kipindi cha awamu ya tano ilivyozuia sukari kutoka nje nchi,kilichotokea nikuanza kupanga foleni kama ndio nchi inapata uhuru...pia sukari ilipanda gafla mpaka ikaw ni bidhaaa adimu sana mjini kipindi hicho..tumesahau eh?

Leo mtu anatoa kauli za kuzuia uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi alafu tunaona yupo sahihi..anataka aturudishe kwenye ile foleni eh....

Ongera mama kwa kukemea tena kwa ukali,wachache tunakuelewa.

Waziri mwenyewe anakiri yakwamba viwanda vingi bado hazijafanyiwa expansion kwa lengo la kuongeza uzalishaji w sukari...na akaenda mbali akasema ni ya moshi tu ndio imekizi vigenzo😲 moshi.

Sitaki niende mbali zaidi..ila kwa report yake anakiri yakwa bado viwanda vyetu havinauwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha..hii ni kwa tafsiri rahisi..alafu unazuia sukari kutoka nje...hii nonsense inaanzia hapa..

Haya maamuzi ya waziri nadhani sio kwa maslahi ya watanzania kwa anataka kutengeneza tatizonkama lile la wakati ule.

Maana yake mwisho wasiku rahis atanzaakutupiwa lawama na watanzania, kama tatizo lile litajirudia...mimi natafsiri tofauti kabisa..namuomba mama awe makini.

Mwisho wa siku mama aonekane ameshindwa kazi eh...

Mama kaza wala usimuogope mtu..unamamlaka ya kufanya chochote kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Kesho nitaendelea kufuatilia ile kesi ya ugaidi.Nchi lazima iwe salama chini ya mama yetu mpendwa.
 
Hapo vip!!

Kwanza kwaheshima kubwa nawiwa kumtia moyo mama yetu mpendwa na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania dhidi ya majukumu mazito alionayo katika maisha yake...
Usirukie mambo usiyoyajua wewe chawa. Waziri alikuwa anasimamia maamuzi ya Serikali. Teuzi za kimalaya malaya siku hizi hakuna.


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Usirukie mambo usiyoyajua wewe chawa. Waziri alikuwa anasimamia maamuzi ya Serikali. Teuzi za kimalaya malaya siku hizi hakuna.View attachment 2027648View attachment 2027649

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Balozi Ame Mpongwe amesema Tanzania haijaacha kununua sukari kutoka Uganda kikiwemo kiwanda cha Kilombero sugar kilichonunua tani 4300 licha ya bei za Uganda kutokuwa za kishindani ukilinganisha na maeneo mengine katika ukanda huu.

Hata Bakhresa ambaye kiwanda chake badi kinajengwa huko Sadani anaimport sukari kutoka Uganda, amesema balozi

Hivyo taarifa alizotoa Rais Museveni kwa Rais Samia hazikuwa sahihi sana, ameandika balozi kwenye ukurasa wake wa twitter.
 
Back
Top Bottom