PreGE2025 Rais Samia: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa Haki, Falsafa ya 4R kuendelea kutumika

PreGE2025 Rais Samia: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa Haki, Falsafa ya 4R kuendelea kutumika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu mama anadhani nchi inaendeshwa kwa utashi na ulaghai kama kupaka make up na kufunga ushungi.

Kama yupo serious afanye mabadiliko ya mifumo ya kikatiba na kisheria .
Ushungi umeengiaje ? Chuki zenu dhidi ya ushungi ndio maana chadema mnapoteza imani kwa waislam
 
Watu wanataniana na yule bibi,ila anachotufanyia,walio wengi 2030 na kuendelea tutajuta
 
Maelezo hayahaya yalitolewa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 lakini kilichotokea ni uchafuzi wa uchaguzi kama ilivyotokea 2019,2020.Mbaya zaidi watu waliuliwa na dola kisa tu uenyekiti wa kitongoji.
Nawaunga mkono CDM na No reforms,No election.
 
Huyu mama awe na aibu wakati mwingine. Watz siyo wajinga hata wanaccm wenziye walio wengi wanatambua hilo.

Eti milango ya Serikali iko wazi. Wapinzani wakazungumze nae wakati ni Mgombea tena anaelilia hicho kiti kwa gharama yeyote hata kwa kumwaga damu yuko tayari.

Watz tuamke tuweke pembeni uvyama, tujiulize huyu mama kakaa miaka tisa Ikulu ila hataki kuondoka kuna nn chakwake pale??? Kwanini anawalaghai Watanganyika anataka kutufanyia biashara gani??
 
Rais Samia amesema Uchaguzi Mkuu kufanyika kwa njia ya Haki, kwa kusimamia misingi yote ya Kanuni, Sheria na desturi zote za Uchaguzi, Falsafa ya 4R itaendelea kuwa moja ya nyezo kuu katika uchaguzi mkuu ujao

Hiyo ni siasa, Yaani wagombea wa upinzani wasienguliwe, mawakala wa upinzani wasitolewe vituoni mmmmh
 
Maelezo hayahaya yalitolewa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 lakini kilichotokea ni uchafuzi wa uchaguzi kama ilivyotokea 2019,2020.Mbaya zaidi watu waliuliwa na dola kisa tu uenyekiti wa kitongoji.
Nawaunga CDM na No reforms,No election.
Kinana aliwadanya kina zitto kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki, lakini kilichotokea duh...
 
Hata magufuli alisema hivyo hivyo Ile 2020 lakini yaliyotokea Kila mtu anajua.

Kumuamini mwanasiasa tena wa ccm ni kazi sana.

Juzi tu 2024 wameiba uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaengua wapinzani halafu Leo anatoa hizo kauli .. inatia hasira sana...

Mwaka 2024 uchaguzi wa serikali za mitaa umesimamiwa na makada wa ccm ngazi za kata.

Sehemu zingine walizosimamia walimu wasio makada wakatishwa wasipitishe mpinzani....

Sehemu zilizokuwa na upinzani kama BADI, MALAMPAKA wilayani Maswa mkoani Simiyu wakaambiwa wachukue fedha waachie ngazi au wapewe kesii...

HAWA NDIO CCM NI HATARI MNO ....

Leo unadai uchaguzi utakuwa wa huru na haki hilo haliwezekani KAMWE CCM mmeshajitengenezea kansa ya wizi wa uchaguzi..

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya Maswa kafanya hujuma kubwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 lakini umeamua hujuma ile aipeleke na Bunda kwenye upinzani mkali baada ya hapo umpeleke Mbeya Kwa sugu.. ..Leo unadai uchaguzi utakuwa wa huru na haki!!?

CCM wananchi tunajua Kila kitu kinachoendelea.
Kwa tume hii ccm wanafanya watakalo...
 
Ukitaka kuamini CCM ni mashetani yaaani hapo yupo kwenye kongamano la dini tena leo ni siku ya dini na wametoka kwenye mfungo alafu anaongea mambo ambayo hata mwenyewe anajua ni uongo na uzandiki.
Haya sasa, si ndio vioja hivyo!
Wanaamini uchaguzi wa serikali za mita ulikuwa wa haki na huru kabisa; na wao sasa hivi wanajivunia ushindi mnono.

Wanaamini kuwa uteuzi wa mgombea wa CCM kwa kiti cha Rais ulikuwa wazi kabisa na wajumbe wote waliridhia matokeo ya uteuzi huo.

Kwa hali hiyo hiyo, wanaamini kwa dhati kabisa kwamba uchaguzi mkuu utakuwa wa HAKI na HURU kabisa, hata kama mazingira yaliyopo wanajuwa hayaruhusu hali hiyo.

Hawa watu ni waumini wa dini na wacha Mungu, wanao amini kuwa wao wanaweza kuwadanganya watu wanao waongoza na huyo mungu wanaye mwamini mradi tu matakwa yao yatimie.

Kama huku siyo kuongozwa na shetani ni nini kinachowalaza akili hawa watu.
 
Samia anafahamu fika ushenzi uliofanyika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa chini yaWaziri wa TAMISEMI Mchengerwa si mpya!

Kuenguliwa wagombea wa upinzani si mpya! Mawakala wa upinzani kutoapishwa, kuzuiwa kuingia katika vyumba vya uchaguzi, kunyimwa nakala za matokeo vyote si vipya! Wapinzani kuwekewa figisu kufanya kampeni si kipya!

Sasa Samia anasema atarekebisha kwa kutumia sheria na kanuni gani ya uchaguzi! Je katiba imerekebishwa ili kuruhusu marekebisho ya haki?

Wananchi tumedanywa kiasi cha kutosha na sasa basi!

Inatosha!
 
Back
Top Bottom