Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono hoja.Yeye kwanza ndiyo anatakiwa anyongwe kwa kushindwa kusimamia na kushiriki kwenye wizi wa mali za umma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo tarehe 04 Oktoba, 2024.
RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.
RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Akizungumza wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mchakato wa ulipaji kodi unatakiwa kuwa rafiki ili kumwezesha mlipa kodi kukamilisha zoezi hilo ikiwemo mifumo inayotumika.
Amesema kuna umuhimu wa kutoa elimu zaidi kwa walipa kodi ili wajue wanamlipa nani na kiwango gani, akitoa mfano amesema alikutana na changamoto Mkoani Ruvuma ambapo alisema kuna Mama Lishe waliokuwa wakilalamika kuhusu kulipishwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
=========================
RAIS SAMIA: HATUA MPYA KATIKA MABORESHO YA MFUMO WA KIKODI TANZANIA
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza tangu Rais Benjamin Mkapa kuboresha mfumo wa kikodi nchini Tanzania, baada ya kuunda Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi. Tume hii ina lengo la kuangazia changamoto mbalimbali zinazokabili mfumo wa kodi na kutoa mapendekezo yanayoweza kuboresha ukusanyaji wa kodi na ufanisi wa matumizi yake.
Moja ya mambo makuu ambayo Rais Samia anatarajia kuyatekeleza kupitia tume hii ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa kodi. Hii ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa serikali na mfumo wa kodi, ambao mara nyingi umekuwa ukikabiliwa na malalamiko kuhusu ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Pia, tume hiyo inatarajiwa kuzingatia njia mpya za kukusanya kodi ambazo zitasaidia kuongeza mapato ya serikali bila kuweka mzigo mzito kwa wananchi. Hii inaweza kujumuisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji wa kodi, kama vile mifumo ya kielektroniki inayorahisisha malipo ya kodi na kuondoa urasimu usio wa lazima.
Aidha, Rais Samia amesisitiza katika ushirikiano na sekta binafsi ili kuboresha mfumo wa kikodi. Ushirikiano huu unaweza kuleta mawazo mapya na mbinu za kisasa katika ukusanyaji wa kodi na pia kutoa fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya uchumi wa nchi.
Kwa kufanya hivi, Rais Samia atasaidia kukuza mazingira ya biashara yanayovutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi. Hii ni muhimu katika kipindi ambacho uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto, na Tanzania inahitaji kuongeza mapato yake ya ndani ili kufikia malengo yake ya maendeleo.
Tunatarajia wewe ndio utupe report kwa kuwa,Unafahamu Zaid ya hili jamboReport ya uchunguzi kuhusu anaowateka ataitoa lini?
Bi Chura anaropokaga sana.Si aliwambia Jamaa wale kwa urefu wa Kamba zao.
Huyu bibi haishi kulalamika kama vile hajui jukumu lake la kuwa Rais!NDUGU ............ MENEJA WA TRA MKOA WA KODI KINONDONI ANAKUHIMIZA KULIPA KIASI CHA SH. 93,418,445.29 AMBAYO NI MALIPO YA VAT YA MWEZI AGOSTI 2024. LIPA KODI HII KABLA YA TAREHE YA LEO 30/09/2024. RIBA NA ADHABU ZITAJUMUISHWA KWA KUSHINDWA KULIPA KWA WAKATI.
"PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU"
Waaaambie silipi hata kwa fimbo, waniue! Hii ni Kodi au ni laana?
HafaiNaunga mkono hoja.