Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Nanukuu...Rais Samia Suluhu akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, amesema kuwa kodi tunayokusanya hailingani na idadi ya watu.
“Uchumi wetu unakua sana, lakini haulingani na tunachokikusanya. Tunakusanya kidogo sana, kingi kinaingia mifukoni kwa watu bure bure tu. Shughuli za kiuchumi zinazoendelea nchini na idadi ya watu hailingani na mapato tunayoyapata.”
My Take: Naunga mkono hoja, na huu ndio ukweli. Ukiangalia utajiri wa Watu na miradi wanayofanya na kile tunapata ni vitu 2 tofauti.
Serikali inawaonea Watumishi tuu ambao hawawezi kukwepa Mapato lakini huko Mitaani wafanyabiashara wanalipa robo ya wanachostahili au wanakwepa kabisa.👇👇
Pamoja na Kulalamikia kwamba watu ni wengi ila hawalipi Kodi ni lazima ujue kati ya hao watu mil.65 ,,ukiondoa under 18 na maskini,wanafunzi,wazee Je Nguvu kazi halisi ni kiasi gani?
Soma hapa: LIVE - Rais Samia akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Ikulu - Dar, Oktoba 4, 2024
Tunakusanya kidogo sana, kingi kinaingia mifukoni kwa watu bure bure tu.
Mwisho wa kunukuu...!!!
Wananchi walalamika
Rais analalamika
Viongozi wote wanalalamika
Sasa sijui nani atatatua tatizo linalolalamikiwa