Rais Samia: Ujasiriamali kuwa somo la lazima kwa Sekondari kidato cha kwanza hadi nne. Ili kuandaa vijana kujitegemea

Rais Samia: Ujasiriamali kuwa somo la lazima kwa Sekondari kidato cha kwanza hadi nne. Ili kuandaa vijana kujitegemea

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia amesema kuwa Ujasiriamali litakuwa somo la lazima kwa wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ili kuwaandaa kujitegemea. Akisisitiza kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuleta mageuzi katika sekta ya elimu ili iendane na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya taifa.

"Sera hii inajibu hitaji la muda mrefu la kuweka mfumo wa kutambua na kurasimisha ujuzi na stadi zinazopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo tulionao". amesema Rais Samia

Soma, Pia: Rais Samia atishwa na kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu

Sambamba na hilo, Rais Samia ameongeza kuwa ujuzi, sera na mitaala hiyo pia imeleta somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
 
Lile somo la historia la kiswahili liliishia wapi ?🐼

Lile somo la historia la kiswahili liliishia wapi ?🐼

Limeanza mwaka huu na ndio limechukua nafasi ya civics ambayo Sasa imekuwa "historia ya Tanzania na maadili" linafundishwa kwa lugha ya kiswahili japo vitabu sivioni
 
Hayo masomo yote ni mazuri shida nyenzo zake za kufundishia hakuna vitabu syllabus Wala machapisho madogo madogo
 
Inaonekana bado haswa hatujajua tatizo LETU la msingi kwenye Elimu na jamii kiujumla.

Bado tunafikiria kinadharia sana.
 
Vizuri
Rais Samia amesema kuwa Ujasiriamali litakuwa somo la lazima kwa wanafunzi wa sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ili kuwaandaa kujitegemea. Akisisitiza kuwa mabadiliko haya ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuleta mageuzi katika sekta ya elimu ili iendane na mahitaji halisi ya soko la ajira na maendeleo ya taifa.

"Sera hii inajibu hitaji la muda mrefu la kuweka mfumo wa kutambua na kurasimisha ujuzi na stadi zinazopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo tulionao". amesema Rais Samia

Soma, Pia: Rais Samia atishwa na kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu

Sambamba na hilo, Rais Samia ameongeza kuwa ujuzi, sera na mitaala hiyo pia imeleta somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
 
Shida ya mfumo wetu wa ELIMU uko kinadharia na hauendani na Kasi ya dunia.

Vijana wanatakiwa wafundishwe skills based subjects, pamoja na technolojia toka shule ya msingi na tuhakikishe kuna labs za kutosha.

Mfano, shule ya msingi vijana wafundishwe kufix simu hizi smarts, computer na application yake, kuwe na labs za kutosha.
Vijana wafundishwe programming, coding etc.
Vijana wafundishwe basics za mechanics, automotives technolojia, construction works etc.

Kijana akimaliza form 4 anakuwa na knowledge ya ziada mfano welding, hapo ataomba welding machine tu na electrodes.
Kijana akimaliza form four ana addition knowledge yakufix computer au programming anaweza kuwa na chakuanzia.
Vijana wanamaliza form six wanasubiri kwenda CHUO kikuu hawana addition skills yeyote yakusurvive kitaa, kijana Hana hata knowledge ya plumbing.

Kijana anayemaliza course yeyote university anapaswa kuwa na addition skill ya kusurvive kitaa nje ya taalum au ndani ya taalum unayoweza kutumika mitaani akaishi, sasa vijana wetu anamaliza Elimu ya kukariri, anabeba vyeti anaanza kukimbizana na ajira kitaa.
 
Vizuri lakini tumechelewa tungeanza mapema
 
Sambamba na hilo, Rais Samia ameongeza kuwa ujuzi, sera na mitaala hiyo pia imeleta somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
Si waliona Nyerere alikuwa mjinga wakafuta EK mashuleni
 
Back
Top Bottom