Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,534
- 7,866
Unapoteza muda na energy yako : kama unafanya kazi, ni sawa na mtu akuombe uache kazi ili na yeye apate, wewe utakula wapi.?Sio bahati mbaya rais Samia amekwenda Marekani wakati huu taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani likiwa katikati ya mtanange mkali wa uchaguzi. Na mara hii ni kati ya mhafidhina Donald Trump na mwanamama Kamala Harris.
Mtu hawezi kushindwa kufikiri kuwa kimya kimya rais Samia amekuwa kwenye kampeni za urais wa Marekani kwa kujua ama kwa kutojua. Hii ni mara ya pili rais Samia anakwenda Marekani ndani ya kipindi cha takriban mwaka mmoja hivi.
Wamarekani wakati huu wa uchaguzi wakimwona rais mwanamke tena kutoka nchi ya dunia ya tatu ambapo demokrasia ni majaaliwa tu basi wamarekani wanajisikia kuwa nyuma ki-demokrasia na jambo hili linaweza kuathiri maamuzi yao wakati wa upigaji kura.
Ama kweli siasa ni sayansi na ingekuwa tunafanya siasa zetu kisayansi tungekuwa mbali sana.
Swali ni je, rais Samia atarudi amejifunza nini kuhusu demokrasia na uchaguzi huru na wa haki? Je Samia ataguswa kujenga mazingira yanayoruhusu uchaguzi kufanyika chini ya tume huru ya uchaguzi? Je Samia atajifunza “fair play “ kwenye chaguzi zetu ambazo Tumeona wagombea wengi wakipitishwa bila kupingwa huku wapinzani wakienguliwa bila sababu za msingi?
Hiyo ndio zawadi tunayoisubiri kutoka kwa rais wetu mama Samia pindi arudipo kutoka ziarani Marekani na Cuba.
Demokrasia haiombwi, it has to be demàded Even by bloodshed, in demanding…… there comes a respect
Nimekua nikisema snaa ; there is no way chama cha upinzani kitashinda bila katiba mpya. Kama unadhan wakuu wa wilaya, wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri wanachaguliwa na rais kwa bahati mbaya haya, hao ndio wapishi wa kuhakîkisha kura zinaenda chama tawala
A cut off ya hao watu kuwa presidential appointment ni lazima
DG wa NEC ni presidential appointements, still mtu ana expect démocracy kwenye ouchaguzi, that is absard.
NEC inatakiwa iwe independent entity na DG wake achaguliwe na wananchi
Rais hapaswi kuteua DED, wala mkuu wa wilaya wala mkoa , ni watumishi na hawapasw kuwa na affiliation na yeyote
Kama hayo hayafanyika, achaneni na story za demokrasi
Pigeni maokoto Kama kina mbowe life isonge