Rais Samia, ulitaka kutuhutubia au kuzungumza nasi?

Rais Samia, ulitaka kutuhutubia au kuzungumza nasi?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Binafsi nilijiandaa sana kuja kuongea na Mh. Rais nimweleze changamoto na masuluhisho kadhaa kwa baadhi ya changamoto tulizo nazo vijana mitaani.

Achana na mawaziri hawajui changamoto zetu sababu hawajavaa viatu vyetu. Mimi sikuja na chama chochote. Nilikuja na hoja na naona ntaondoka nazo kama nilivyokuja nazo.

Niliamini tunakuja zungumza na Rais wetu. Kumbe tunakuja elezewa mambo kadhaa na watu kadhaa
 
Haya mambo ya kiongozi mkuu kuongea na wananchi mara nyingi ni Public Relations na kupiga Kampeni. Mfumo mzuri na sustainable na wenye tija ni kero zote kupitia kwa wawakilishi ambao wapo kila ngazi, na sababu Rais ni Taasisi nina uhakika hata akitaka kujua kama bei ya nyanya imepanda pale barabara ya saba chini ya mwembe mkoani Tanga hashindwi.

Hivyo basi nguvu nyingi itumike kwenye kurekebisha kero (sio kujifanya tunasikiliza kero ambazo nina uhakika hata miaka 15 iliyopita zilikuwa ni hizi hizi tu)
 
Maneno haya mawili hapa bongo hayajawah pata tafsiri kamili hasa kwa wanasiasa

KUHUTUBIA/HOTUBA

KUONGEA

Katika maneno haya mawili mwanasiasa anaweza iamuru hata BAKITA na ikakubaliana na matakawa ya wanasiasa

aione ONI SIGALLA kwenye jalada

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Masaa sita hakuna vijana hata wa risala tu.
Wabunge,
Mawaziri,
Singeri,
HOYE NYINGI,
Bora hata wazee wa Dar walitoa nyongo zao.

KATAMBI NA JENISTER wamefanya kazi yakuwanadi wenzao.

Vijana walitakiwa kuongea nje ya vijana waliopo kwenye mfumo
 
Binafsi nlijiandaa sana kuja kuongea na Mh. Rais nimweleze changamoto na masuluhisho kadhaa kwa baadhi ya changamoto tulizo nazo vijana mitaani.

Achana na mawaziri hawa wahajui changamoto zetu sababu hawajavaa viatu vyetu. Mimi sikuja na chama chochote. Nlikuja na hoja na naona ntaondoka nazo kama nlivyokuja nazo.

Nliamini tunakuja zungumza na Rais wetu. Kumbe tunakuja elezewa mambo kadhaa na watu kadhaa
Tangia lini Babu kama Wewe ukawa Kijana?
 
Nilitegemea mic itembee kwa hadhira hiyo. walau vijana 50, Waseme.

Then tupate sample studies za vijana waongee hapo juu.

Wapendekeze solutions.

Etc etc etc.

Disappointed.
Alijua sana yale mliyotaka kuongea that's why hakuona sababu ya kutembeza mic kwa vijana wote 50.

Wewe binafsi, una jambo gani jipya kwa mfano?
 
Binafsi nlijiandaa sana kuja kuongea na Mh. Rais nimweleze changamoto na masuluhisho kadhaa kwa baadhi ya changamoto tulizo nazo vijana mitaani.

Achana na mawaziri hawa wahajui changamoto zetu sababu hawajavaa viatu vyetu. Mimi sikuja na chama chochote. Nlikuja na hoja na naona ntaondoka nazo kama nlivyokuja nazo.

Nliamini tunakuja zungumza na Rais wetu. Kumbe tunakuja elezewa mambo kadhaa na watu kadhaa
Nilivyoona tu anaenda kukutana na vijana kwemye uwanja wa michezo wa nyamagana nikajua hapa hamna kitu
 
Back
Top Bottom