Rais Samia, ulitaka kutuhutubia au kuzungumza nasi?

CCM hawajui lugha ya kiswahili vizuri.
Hebu msikilize mwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo,uvuvi na maji,tarehe 14 pale Misungwi.
 
Excellent views.
 
Excellent views.
Hivi wewe unaakili kweli? Kama kila mtu aliyekuwepo pale amgetaka kuongea na Rais wangetumia siku ngapi kukamilisha ndio maana kukawekwa wawakilishi wetu. Kwa akili hizi ndio maana hatujielewi tunataka nini.
Huna akili wewe.
 
Saiv ni mwendo wa hotuba tu,zilizosheheni maneno matamu na vionjo vya kizanzibar hakuna jipya,msukuma wampelekea maneno tu xjui kama akuelewa
 
Ujima na usanii si aliondoka nao dhalimu wako na sasa tuko vizuri au?

Dhalimu alikuwa mjima wa level ya juu kabisa, ila kaacha wajima kibao nyuma yake.
 
Naunga mkono hoja, ni kweli kabisa mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kuna haja gani ya kiongozi wa juu( Rais) kabisa kufanya mikutano ya namna hiyo wakati kuna mfumo kutoka chini ambao unatakiwa kufikisha taarifa kwake. kiongozi wa juu kwenda kuongea na wananchi ambao wana wawakilishi wa kila namna, je ni ishara ya kuwa kiongozi huyo anakiri kuwa kuna mfumo uliopo ni wa ovyo ulioshindwa kufanya kazi!, je ikiwa kila jambo kiongozi huyo ataenda kuongea na wananchi kwa hali tuliyonayo ataenda mara ngapi!

Mimi naamini kiongozi mkuu anatakiwa kurekebisha mfumo unaomletea taarifa, ili apate taarifa sahihi na kwa wakati, haya mambo ya kuongea sijui na vijana na makundi mengine sioni kama kuna tija, wadau wengi humu wamedai kuwa vijana hawakupewa nafasi ya kuelezea changamoto zao, ila hakika nakuambia kama mfumo uliopo ni mbovu hata hao vijana ambao wangepewa nafasi ya kuuliza wangepangwa na viongozi wasio waaminifu. Pia wangepangiwa kitu cha kuuliza, hivyo kiongozi huyo wa juu asingepata taarifa sahihi.

Ushauri wangu ni kwamba mfumo wa kupeleka taarifa kwa kiongozi wa juu yaani Rais urekebishwe, viongozi ambao wanaomwakilisha ambao hawatimizi majukumu yao waondolewe, harafu Rais atenge siku maalum ya kulihutubia taifa, kwa kujibu hoja zilizoletwa mezani kwake pia kutoa majibu ya changamoto zote ambazo zililetwa kwake kwa kupitia vyanzo vyake mbalimbali.
Mwisho wa kuwasilisha.
 
Wanapenda sana kutumia hayo makundi ya wazee, wanawake, vijana nk kupaka rangi upepo.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Vipi ulipata T-shirt?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…