Endeleeni kuupiga mwingi si ndio nyie mlipiga vigelegele kuwa sasa mumempata mtu wa watu, msikivivu na misifa kibao, leo kulikoni? sisi wengine bado tuko kwenye maombolezo ya mwendazake, enzi zake haya mambo yasingetokea asilani. Kama mwendazake aliweza iweje sasa huyu ashindwe? jua kuna kitu hapa, mngeanza kwanza kumkataza kuruhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo haina tija na kuna watu wanufaika na hiyo kandarasi ya kitapeli na ndio sasa wanakomaa ili wao na familia zao wazidi kuneemeka, pamoja na ukwasi walio nao lakini bado tamaa zimewazidi, sasa wamekuwa ndio Alfa na Omega wa nchi hii, enzi za mwendazake waliwekwa kapuni. Kwa haya yanaoendelea tutazidi kumkumbuka jabali mwendazake.