Rais Samia umekubali kutukuzwa hivi? Yanayofanyika shuleni siku yako ya kuzaliwa siyo sawa

Duu aibu naona mimi sasa hapo kwenye jukwaa la mwenye basidei nani atakaa au Mama itabidi aende pale Benjamini Mkapa? Kwao walitenga bajeti kwaajili ya Besidei ya Rais? No wonder unaweza kukuta shule ina upungufu wa madawati au maji yamekwatwa kwa kudaiwa lakini wana bajeti ya besidei ya Rais duu

Hichi ni kiwango cha juu sana cha kujipendekeza aiseee...
Na hapo hapo ukute kuna wanafunzi hawana hata daftari , mie nilipo ona kwenye TV ya chichiemu nikasema loloooo.....
 
Kusherehekea Siku ya kuzaliwa Rais ni kutukuzwa? Siku ya Furaha Mkuu wa nchi kufurahi na watoto wa shule na raia wengine ni kosa? Tusipende kujadili na kukuza vitu.
Tuseme kimefanyika Tanzania tu...kwani Tanzania lazima iige Biden, Boris Johnson au Macron wanafanyaje? Ni style yetu mpya ya Rais kushare furaha na raia wake.[emoji120][emoji120]
Si tulikubaliana sisi sio kisiwa? Tunaenda na dunia inavyotaka? Au?
 
Screenshot_20220128-033147.jpg
 
Jamani hizi sherehe zisiwe zinapita hivi hivi bila sisi wananchi kupewa keki au hata pilau.
 
Style ya Magufuli naona imewaafect wengi hapa nchini sababu ilikubalika kwa wapumbavu wengi waliokuwa wanapelekeshwa bila kuelewa jamaa anafanya nini?

Lakini pia hiyo style inatumiwa na wanasiasa wengine kwa sasa yani unakuwa mwizi Ila unajifanya unawapenda sana wamasikini na unawaita wanyonge ili waendelee kukuona wewe ndio mteyezi wao ingali wewe unaishi ikulu na unapiga dili zako fresh kabisa unahakikisha sababu wewe pekee na kikundi chako ndio mnaoiba basi wengine wanakuwa hawaibi ili uonekane unawatetea hao wanyonge.

Style ya Magufuli hata mie nikiingia madarakani nitakutumia kujihakikishia nawatawala wapumbavu mpaka nitakapokufa sababu watu hawaamini kwenye utawala wa kupokezana na kuheshimu Katiba.

Huyu mama anaweza kubakia mpaka atakapokufa Kama aliamua kwenda na style ya Magufuli Ila naona ni kasehemu kadogo sana anafanya hamuwezi Yule dikteta aisee.

Magufuli alihakikisha machinga halalamiki ili yeye anapopiga na machinga asimfuatilie. Yani anakuja anasema hili daraja liwe limejengwa wiki ijayo hapo ni upigaji sababu halina bajeti iliyokaa kupitisha huo ujenzi Wala procurement.

Anaibuka anasema ijengwe lami hapa na hakuna bajeti iliyokaa kupitisha huo ujenzi. Hapo kumbe anahakikisha kampuni zake zinajenga na analipwa fasta sababu halina kusubiri paymaster general aidhinishe vibali vya malipo yani unampigia Rais ndio anakulipa.

Ule ni ushenzi mkubwa ambao watu wameona ndio unafaa nadhani bila Katiba ya maana atakuja kutokea mwehu mwingine akatupa shida sana.

Uzuri wa hii nchi watu hawakubali mambo ya kuingia msituni ni either tunakushauri ukikataa wanakumaliza fasta usisumbue taifa maana alikokuwa anaelekea lazima tu angekuja kupinduliwa.

Uongozi wa kiimla huwa na matokeo mabaya ndio maana Nyerere mwenyewe pamoja na yote alifika sehemu akaamua aachie ngazi wengine watawale maana alibana mno kila siku anataka tuwaze Kama yeye tu.

Akina Kambona wanakuja na mawazo mbadala Ila hakubali anawaza kimasikini tu. Alikoswakoswa kupinduliwa Mara 10 na alipokuwa anaelekea angeshangaa anapinduliwa maana Marekani walikuwa washamuweka kwenye target ndio maana akarudisha utawala wa kidemokrasia .

Sasa huyu mama sitamshangaa maana watu wanapenda kukimbizwa Kama mbuzi ndio wanaona huo ndio utawala Yani unahakikisha hakuna anayehoji kitu wapumbavu ndio wanaona huo ndio utawala. Yaani unalala na mkeo anakushauri kesho ujenge airport kijijini kwenu na unaamka unampigia simu Waziri wa ujenzi akajenge haraka bila kuwaza.

Kimada wako alisema anataka lami mtaani kwao unampigia Waziri wa ujenzi akajenge lami haraka sana.

Huu ndio upuuzi ambao tumefikia tunaona ndio uongozi. Wacha twende na hiyo style tuone.
Desa refu ukimkandia Magufuli wakati mada iko wazi kuhusu Hangaya. Kweli nyie watu iko na ttz kichwani.
 
Hakuna mambo ninayoyachukia kama kusifu sifu mtu na kumtukuza matokeo yake mambo ya kusifu na kuabudu yanarudi tena mdogo mdogo .
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, yaani Birthday ya mama Mwakitozo ndiyo imekuwa ajenda nchi nzima - kweli ?
 
Ni wivu tu (kwa sauti ya Gwajiboy) 😁😁
 
Birthday ya Baraka Obama mliijua na kusherehekea kimoyo moyo, birthday ya Queen Elizabeth mnajua, etc. Raisi Samia Suluhu Hasan - Huyu ni one of our heroes (Mkwawa, Kinjekitile, Nyererr, Magufuli, Mkapa, Ali Hasan etc) - ni mashujaa wetu. Tufurahie na waliopo hai tusherehekee nao. Kataa/kubali - like it or not, she is our hero. Kwa walio hai tuwaonyeshe upendo tusingoje wakufe! Kipende chako kwanza! Huyu ni Raisi wetu, tumtakie mema. Yupo kwa niaba yetu.

Happy birthday Samia(Raisi, Amir jesh mkuu, mwenyekiti wa CCM, Mama na mke wa mtu).
Mungu wangu Hero?😁
 
Style ya Magufuli naona imewaafect wengi hapa nchini sababu ilikubalika kwa wapumbavu wengi waliokuwa wanapelekeshwa bila kuelewa jamaa anafanya nini?

Lakini pia hiyo style inatumiwa na wanasiasa wengine kwa sasa yani unakuwa mwizi Ila unajifanya unawapenda sana wamasikini na unawaita wanyonge ili waendelee kukuona wewe ndio mteyezi wao ingali wewe unaishi ikulu na unapiga dili zako fresh kabisa unahakikisha sababu wewe pekee na kikundi chako ndio mnaoiba basi wengine wanakuwa hawaibi ili uonekane unawatetea hao wanyonge.

Style ya Magufuli hata mie nikiingia madarakani nitakutumia kujihakikishia nawatawala wapumbavu mpaka nitakapokufa sababu watu hawaamini kwenye utawala wa kupokezana na kuheshimu Katiba.

Huyu mama anaweza kubakia mpaka atakapokufa Kama aliamua kwenda na style ya Magufuli Ila naona ni kasehemu kadogo sana anafanya hamuwezi Yule dikteta aisee.

Magufuli alihakikisha machinga halalamiki ili yeye anapopiga na machinga asimfuatilie. Yani anakuja anasema hili daraja liwe limejengwa wiki ijayo hapo ni upigaji sababu halina bajeti iliyokaa kupitisha huo ujenzi Wala procurement.

Anaibuka anasema ijengwe lami hapa na hakuna bajeti iliyokaa kupitisha huo ujenzi. Hapo kumbe anahakikisha kampuni zake zinajenga na analipwa fasta sababu halina kusubiri paymaster general aidhinishe vibali vya malipo yani unampigia Rais ndio anakulipa.

Ule ni ushenzi mkubwa ambao watu wameona ndio unafaa nadhani bila Katiba ya maana atakuja kutokea mwehu mwingine akatupa shida sana.

Uzuri wa hii nchi watu hawakubali mambo ya kuingia msituni ni either tunakushauri ukikataa wanakumaliza fasta usisumbue taifa maana alikokuwa anaelekea lazima tu angekuja kupinduliwa.

Uongozi wa kiimla huwa na matokeo mabaya ndio maana Nyerere mwenyewe pamoja na yote alifika sehemu akaamua aachie ngazi wengine watawale maana alibana mno kila siku anataka tuwaze Kama yeye tu.

Akina Kambona wanakuja na mawazo mbadala Ila hakubali anawaza kimasikini tu. Alikoswakoswa kupinduliwa Mara 10 na alipokuwa anaelekea angeshangaa anapinduliwa maana Marekani walikuwa washamuweka kwenye target ndio maana akarudisha utawala wa kidemokrasia .

Sasa huyu mama sitamshangaa maana watu wanapenda kukimbizwa Kama mbuzi ndio wanaona huo ndio utawala Yani unahakikisha hakuna anayehoji kitu wapumbavu ndio wanaona huo ndio utawala. Yaani unalala na mkeo anakushauri kesho ujenge airport kijijini kwenu na unaamka unampigia simu Waziri wa ujenzi akajenge haraka bila kuwaza.

Kimada wako alisema anataka lami mtaani kwao unampigia Waziri wa ujenzi akajenge lami haraka sana.

Huu ndio upuuzi ambao tumefikia tunaona ndio uongozi. Wacha twende na hiyo style tuone.
Tutajie na Mali zake alizozipata akiwa kiongozi !! Maana wengi wetu hatuzijui !! MTU anaiba lakini Mali hazionekani,! ??
 
Nimeona jambo ambalo sikuwahi kuliona kwa maraisi wengine wote na imebibidi nishtuke kidogo. Wanafunzi wa mashule mbalimbali za msingi na sekondari Dar na mikoani nimeona leo wameimbishwa na kurekodiwa madarasani kuhusu birthday ya mama Samia.

Hawa wanafunzi hawajui chochote kuhusu siku yako ya birthday ni wazi waliletewa hilo Jambo na kuambiwa waimbe.
Sasa nachojiuliza haya yote ya nini? Yana faida gani?

Shule ya Benjamini Mkapa leo hapo inafanywa sherehe ya birthday yako na Watoto wapo nje kusheherekea hii birthday yako. Nasisitiza hawa hawafanyi kwa utashi wao kwa kuwa hata pegine hawajui tarehe yako ya kuzaliwa bali wanafanya kwa msukumo.

Kusheherekea birthday ni Jambo zuri na sina tatizo nalo, Ila huku kwenda mashule mbalimbali hadi mikoani na kuwaimbisha kisha kuwarekodi Sio sawa kabisa.

Nimeona kituo kimoja cha redio wakisema hii siku ya tarehe 27 iwe siku ya mama kitaifa.
Umekubali kutukuzwa hivi? Ikiwa umeridhia haya basi pia sina tatizo.
Happy birthday SSH.

View attachment 2097063View attachment 2097064View attachment 2097066View attachment 2097067View attachment 2097068
Yuko kwenye campaini za 2025
 
Back
Top Bottom