Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
1.Mhe Rais naomba kuchukua Nafasi hii binafsi kukushukuru Kwa maamuzi makubwa uliyofanya Kwa maslahi mapana ya Taifa. Mimi ni mwana Chadema na siku zote msimamo wangu utabaki kuungana na wanaotenda haki na wanaostawisha Taifa na Dunia.
2. Mhe. Rais nina watoto na wajukuu, naamini wewe pia una watoto na wajukuu. Sisi bibi zao tumefika hapa tulipo Kwa sababu Kuna watu wakiwemo akina Mwalimu Nyerere walioweka misingi ya Taifa letu. Wangeboronga may be Mimi na wewe tungekulia ukimbizini au tusingekuwepo Duniani Kwa machafuko.
3. Naomba niseme hapa kwamba Tanzania iliaribika awamu ya nne na Tano. Awamu ya nne ilijenga Tanzania yenye kunuka Rushwa, waliosimama kukemea Rushwa awakuwa wana ccm Bali walikuwa Chadema na CUF. Napenda kukumbusha kwamba awamu ya nne hata Marehemu JPM na Mkapa awakupaza sauti kukemea Rushwa. Wote walikaa kimya wakishuhudia manyanyaso dhidi ya watetezi wa haki wakiongozwa na Dr. Slaa . Hivyo tukubaliane kwamba waliompotosha JK Kikwete ni Wana CCM na siyo Watanzania .
4. Awamu ya Tano ilipoingia agenda yake ya kwanza ilikuwa kupambana na Rushwa, this was chademas agenda. Nimpongeze JPM alifanya vyema sana kwenye mapambano ya Rushwa. Lakini wapinzani waliyaona mapungufu yake wakamwambia, ikiwemo kuminya demokrasia ,kukamata wasio na hatia, madhara ya wasiojulikana nk. Mzee wetu aliwaona Hawa ni maadui na ccm ikagongelea msumari kwamba kweli upinzani wanamkwamisha Mzee. Wapinzani wakafungwa, wakapotezwa, wakatekwa na kupigwa risasi. Tujiulize kosa lao lilikuwa Nini? Kosa la wapinzani linabaki KUSEMA UKWELI KWA WATAWALA. Walsema JK wakakamatwa na sasa waliposema JpM mambo yakawa magumu zaidi. Maana yake , Bado ccm haikumsaidia JPM na hivyo kufeli kwa JPM kulitokana na kufeli kwa ccm siyo kufeli kwa Taifa
5. Ameondoka JPM umeingia wewe, jiulize ni viongozi wa CcM wamewahi kukukushauri au kuzungumza adharani kuonyesha kuna sehemu unakosea? Unataka kusema wanaokuzunguka awajui Wananchi wanataka Nini? Chokochoko za Katiba zilipogeuka Ugaidi washauri si walikuwepo? Walikueleza madhara yake? Hapana naamini waliendelea kuwa praising team.Washauri wako walichofanya nikusisitiza kwamba hakuna siasa Tanzania tufanye kazi wakati wao kila siku wanafanya siasa. Leo huko Sumbawanga Polisi bado wameendelea na slogan ya kuzuia wanasiasa wa upinzani wasifanye siasa. Wasijadili katiba, wasizunguzie tume huru nk. Hawa watu Wanawaza kushiba siyo Taifa lishibe.
6. Umefanya miradi mingi, umetembea nje, lakini nikuambie jambo moja Katika yote....Hawa wapiga kura awakusikilizi. Waekuweka KUNDI Moja na utawala ULIOPITA na hivyo wanasubiri siku uwe wewe.
7. Pamoja na kutokukusikiliza Leo umekutana na Tundu Lisu, napenda kukufahamisha kwamba Taifa Lina furaha. Wasaidizi wako wamejitua mzigo wa masononeko, wanaaini Sasa watafanyia kazi utawala wa haki. Wanaamini Sasa kwamba wataanza kulipwa Kwa kufanya kazi za haki siyo dhuluma . Wanaiona Tanzania mpya mbele Yao. Fuatilia kurasa za mitandao ya kijamii uone wasaidizi wako wa Kisiasa wameandika Nini? Walichokiandika wamewahi kukushauri ukifanye huko awali? Fuatilia comments za Wana CCM uone wameandika nn? Kwanini awali awqkukushauri ufanye maridhiano kama kweli waliona nchi inapasuka? Umebaini kwamba Leo hata Kijiji wanajua umekutana na Lisu? Unajua Dunia inashabgilia? Umefanya Jambo kubwa sana, JK na JPm walishindwa kuwasikiliza wapinzani kwenye mambo ya kitaifa ila wewe umefanya. Umeibuka shujaa, watu wanakupongeza kwa sababu wanajua umuhimu wa maridhiano na upendo wa wazazi katika Taifa.
8. Nikuombe Kwa moyo huohuo wataftie Watanzania Katiba Mpya. Siyo lazima uongoze miaka kumi, tumia miaka hii mitano wekeza kwenye katiba Kisha simamia uchaguzi 2025 weka Kiongozi mwingine madarakani kakaeni ule pensheni. Miaka mitano yenye Katiba itamtengeneza mjukuu wako kuwa Rais kuliko miaka kumi yakupabana kuiletea nchi yenye mifumo mibovu maendeleo. Fanya maendeleo ya watu then step down waachie webgine watumie misingi ya Katiba kufanya maebdeleo ya vitu. JPm alijaribu lakini ametoka watu awaoni alichofanya wanataka ifumo ya haki.
Kwa nukta hii naomba niende likizo Kwa muda kusherekea ushindi wa maridhiano uliopatikana Leo Brussels, nijiandae kwenda mahakamani ijumaa kumpokea Mdogo wetu MBOWE Kisha nipate air Tanzania nikale supu ya Samaki Bukoba. Ninafuraha Sana kuona Tanzania inafuraha. Watu wataanza kusalimiana ,, naamini hata wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama watalala usingizi . Walibebeshwa mzigo mkubwa sana na wanasiasa. Unamchukia mtu anayekutetea upate maslahi, unamchukia mtu ambaye ujawahi kukutana naye. Kingai anawatesa makomando waliotolewa kwenye kazi zao binafsi bila hatia. Jaji anahukumu vitu visivyombariki Mungu.