Rais Samia, umerithi wasaidizi hivyo umerithi miiba pia

Rais Samia, umerithi wasaidizi hivyo umerithi miiba pia

Sio kweli ,

Rais baada ya kuingia ikulu tu alibadilisha timu nzima ya wasaidizi wake pale ikulu , kateua ma DC, RC's bado mkeka wa DED na DAS ,

Sasa hao wasaidizi unaowazungumzia wewe mleta mada ni kina nani.

Maamuzi yakishafanyika sidhani kama Kuna namna ya kujiondoa katika kuwajibika.

MaDED sidhani kama wataguswa hawa walishiriki na kuratibu wizi wa kura sioni wakibadilishwa au kuondolewa.
 
Ukwapuaji wa fedha ba bandarini upi huo? Ripoti gani ya cag imesema hivyo?
 
Utaratibu gani unatumika kuondoa miiba bustanini!? Tunaichoma moto yawe majivu kurutubisha mazao ama tuna iweka pembeni kuzuia wanyama waharibifu wasiharibu mazao!?
 
Hivi ilikuaje makamu akaenda ziarani Tanga wakati rais akiwa mahututi?
Kutokana na michezo ya kisiasa inavyoendelea nchini, sisi wananchi tunaona kabisaa wasaidizi ama washauri wa Rais wanamzunguka na wanahakikisha anaenda kuanguka kwenye uchaguzi mkuu 2025.

Issues ambazo seems unazungukwa ni hizi hapa
  1. Wasaidizi uliohama nao kutoka Awamu ya Tano
  2. Katiba Mpya
  3. Ripoti ya ukaguzi wa CAG kuhusu ukwapuaji Bandarini
  4. Sheria ya Kodi 2021/2022 hasa kwenye Tozo za Miamala ya Simu
  5. Majanga ya moto yanayoendelea nchini
  6. Ushauri wa kisiasa
Wasaidizi wako wanatafuta turufu ya kuaminiwa na Chama kupeperusha bendera hapo 2025, humo wapo pia ambao walishawahi kuomba kupeperusha bendera nafasi ya Urais 2015. Wapo ambao mpaka leo wanaamini katika fitina za kisiasa ndiyo maana unaona kuna kundi kubwa mitandaoni linalojitoa ufahamu kuhakikisha wanafarakanisha uongozi wako dhidi ya Mtangulizi wako.

Mama Samia, shtuka mapema kabla mambo hayajaanza kwenda jojo.
 
Rais wangu Samia....nakusalimu!

Nimesikitishwa sana na Kauli ya mteule wako waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, Mwigulu.

Wakati Serikali inatekeleza sera mpya ya fedha katika mwaka huu, mabadiliko mapendekezo ya sera yameoneshwa kupingwa. Na ni haki ya wananchi kupinga kwakua maoni yao hayo kupitia mitandao na platforms mbalimbali ndiyo yana-inform govt policy zijazo au hata kuinfluence mabadiliko ya sera ya sasa.

Ajabu Waziri mwenye dhamana badala ya kutumia muda wake kuelimisha umma kwanini serikali yao imekuja na sera hiyo na kujenga hoja kwanini wananchi waipokee kwa mikono miwili (kwa kueleza rationale ya policy) yeye amekuja na kauli za kebehi, kejeli na ubabe.

Ni kweli katika zama hizi bado tunao Mawaziri wanaoweza kutoa kauli za kipumbavu kama hii ya kusema "mwananchi asiekubaliana na sera ya nchi ahamie Burundi"....are we serious!!?

Waziri anaongea haya katika media na katika mazungumzo very formal. Media imempa nafas ya kufafanua sera yeye akiwa waziri mwenye dhamana....Mwigulu anatusi wananchi. Rais upo!

Ni kweli serikali yako Mama yetu Samia haijali wananchi wake kutoridhishwa na utendaji wa kiongozi huyu ama yule na kwamba jibu muafaka kwa wananchi hao ni kuwataka wahame nchi??!

Yeye Mwigulu kwani kuna mwananchi aliyemwambia kama analeta sera hizo wanazozikataa aondokee hapa Tanzania azipeleke Burundi? Kwamba yeye hapa Tanzania ni kwake zaidi ya hao wananchi anaotaka waondoke??! Mbona wao hawajamfukuza??!

Hizi ni kauli mbaya kwa kiongozi mwenye dhamana. Hakua na sababu ya kuropoka na kuongea kibabe kana kwamba hajali chochote wananachosema wananchi. Serikali na Viongozi wapo kuwahudumia wananchi.

Katika zama hizi za Serikali tukufu ya awamu ya 6 chini ya uongozi wako mahiri Mama Samia Suluhu Hassan, waropokaji aina ya mwigulu wanatia doa serikali yako na kwa kifupi hawafai.

Mama sisemi umuondoe. Ila umkanye kwakua wewe ndiye mamlaka ya uteuzi. Ingefaa aombe radhi ama akishupaza shingo mle kichwa na ninakuhakikishia hata akiondoka Mwigulu KAZI ITAENDELEA.

Marashi
 
IMG_9998.JPG

Nenda Burundi Mkuu...[emoji23]
 
Rais wangu Samia....nakusalimu!

Nimesikitishwa sana na Kauli ya mteule wako waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, Mwigulu..
Mwigulu anautaka Urais na alishajaribu 2015. Huyu kwa jinsi alivyo mpumbavu anaamini atachukua nchi Ila akumbuke walikuwepo akina lowasa, nchimbi na wengine waliishia kuwa disappointed.

Rais anapaswa kumpoteza kwenye ramani mapema sana Ila kama haamini ataona 2025 ndio atajua wenzie wanaunda magroup ya Urais ujao.

Asione kimya wenzie wanamng'ong'a tu aombe sana mzee wa fitna JK awe bado hai atamsevu fitna.
 
Katika watu ambao mara zote sikukubaliana kuteuliwa kwao kuwa waziri huyu ni mmojawapo.
Hafai kuwa ktk wizara yoyote.

Hapa mama na watangulizi wake walibugi.
 
Mwigulu, Nape, Makala, Lugola na wengine kadhaa hawafai kupewa nafasi walizo pewa ktk nyakati tofauti.
 
Nadhani kuna mtu anamshauri rais!!! Ajibu hoja kwa hoja! Asiwe na ghadhabu! Nadhani amewajbu BBC kwa ghadhabu na ametoa kauli mbaya sana iliyoonyesha kama vile mwenye nia mbaya na wapinzani!
Kama ndivyobasi aliwaahidi kuwaona kwa kuwadanganya!!
Kama angekuwa mwungwana angekutana nao wa kwanza kwani ni political partners!!
Lakini angewaambia nini akikumbuka waliyoyatenda 2020 yakamfikisha hapo alipo?????
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Back
Top Bottom