Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mheshimwa Rais.
Umesikika ukiagiza vyombo vyako kufanya uchunguzi wa masuala ya utekaji hata hivyo nasikitika kukwambia kuwa
1. Vyombo vyako haviaminiki tena
Tangu jeshi la polisi na mamlaka mbalimbali za uchunguzi kukataa/kushindwa kuchunguza tukio la Lissu kupigwa risasi, kupotea kwa Ben Saa nane na kupotea kwa Azory Gwanda, wananchi hawana imani na jeshi la polisi kuchunguza matukio utekaji yenye sura za kisiasa
2. Ubambikizwaji wa kesi ya uhaini kwa Akina Dr Slaa
Mheshimiwa rais juzi umesema umepewa taarifa za uwepo wa kikao huko Arusha chenye kula njama za kukuondoa madarakani kinguvu. Hata hivyo ni vyombo hivyohivyo kupitia jeshi la polisi viliatangaza uwepo wa jaribio la uhaini nchini lililopelekea akina Mwabukusi, Mdude Nyagali na Dr Slaa wakiwekwa ndani. Hata hivyo wakaja kuachiwa bila kesi kuunguruma mpaka mwisho. Hapa inaonyesha vyombo vyako vilichemsha
3. Wewe Rais serikali yako ilipeleka muswada bungeni wa kubadili sheria na kuifanya usalama wa Taifa iwe inakamata watu.
Mheshimwa Rais, kwa sheria hii uliyopeleka muswada wake bungeni na kisha kuisaini wewe mwenyewe wa kuwapa rungu watu hawa wa usalama wa Taifa kukamata watu, huku tukijua kuwa hawa hawana vituo vya kawaida vya kuhifadhi watuhumiwa, amabpo raia wanaweza kuwafuata, kuwajulia hali, wakawekwa kwenye reja za kawaida maana yake ni kuwa watu wa usalama wa Taifa wanafanya kazi gizani zaidi. Ni vigumu pia wananchi kuamini kuwa Idara hii pia katika masuala haya ya utekaji nchini.
4. Wapo wahanga wa utekaji na jeshi la polisi halijawahoji
Mtu kama SATIVA analalamika kutekwa, anatuma taarifa za watesi wake, alipigwa risasi akatupwa porini. Lakini jeshi la polisi halijaona umuhimu wa kumhoji ili kuchunguza tukio lake.
5. Wewe Mwenyewe umewahi kulituhumu jeshi la polisi kwa mauji
Uliagiza Waziri mkuu wakati fulani kuunda tume ya kulichunguza jeshi la polisi kwa mauji, ukasema jeshi la polisi lenyewe ni mtuhumiwa. Sasa kama wewe umewahi kudhani kuwa Si busara kwa jeshi la polisi kujichunguza kwa sababu ni mtuhumiwa, Je unadhani wananchi watakuwa na maoni tofauti katika matukio ya hivi karibuni ya mauaji ya mzee Ally Kibao na utekwaji wa watu mbalimbali hasa wananchama wa CHADEMA?
6. Juzi umesema ulisikia clip, Dr Slaa akizungumza tuhuma za utekaji hata hivyo vyombo vyako mpaka sasa vimezubaa havijamuita kumhoji kwa jambo hilo mpaka sasa
Mheshimiwa Rais, imagine wewe umepata clip ya Dr slaa akitoa kauli hiyo, tena miaka kadhaa iliyopita,lakini cha ajabu vyombo vyako eti havijaifanyia kazi clip hiyo kwa miaka yote hiyo. Sasa mheshimiwa rais kama vyombo vyako ni incompetent kiasi hiki, je unadhani raia wataamini kuwa vinao uwezo wa kuchunguza matukio kama hayo ambayo vimeshindwa kuchunguza kwa miaka kadhaa sasa?
SASA Mheshimiwa Rais:
Kama hilo jeshi lako la Polisi limeshindwa kufanya uchunguzi juu ya matukio lukuki ya utekwaji na mauaji nchini hasa yenye mrengo wa kisiasa unadhani wananchi watakuwa na imani na hilo unaloita "agizo" hivyo vyombo vichunguze?.
Mheshimiwa Rais nchi hii imewahi kuwaleta wachunguzi kutoka nje juu ya mauaji ya Padri huko Zanzibar, na sasa Wananchi wanataka wachunguzi huru waje wachunguze matendo ya kidhalimu kabisa ya mauaji ya watu wasi na hatia nchini.
BY THE WAY, TANGU LINI MTUHUMIWA AKAJICHUNGUZA MWENYEWE?