Rais Samia, unawajua Wakenya?

Rais Samia, unawajua Wakenya?

Inaonekana hawajui wakenya vizuri. Mfumo wao licha ya kuwa wa kikabila, ni wa kibinafsi mno. Wachunguzeni ambao unawajua wanaoishi Tanzania. Wengi ambao nimekuwa na mawasiliano na mahusiano nao, mara nyingi huwa wanaongelea ujinga na upumbavu uitwao ukabila hata kama wana elimu ya juu kiasi gani. Wanaishi na kuwaza kikabila. Ni wabinafsi na walafi. Kama tunahitaji watu wa kushirikiana nao nadhani waganda, wazambia na hata wacongo, wamalawi, wanafaa kuliko hawa waliobaki kwenye jumuia yetu ya afrika mashariki.
Mama anapotoshwa, Yaani wenyewe wanabaguana kwa ukabila, ndio waje waelewani na Watanzania
 
Hivi akisema waje ina maana anawaita kiholela au wakija kuna utaratibu unafuatwa, kenyatta kasema tukafanye biashara bila permit ila sidhani kama amemaanisha wamachinga wakaje Nairobi, sheria itakayotumika kuwabana Australia, Marekani,China na yyt yule itawabana na Wakenya pia.

Ninachikiona mimi ni kwamba Watanzania kwa miaka mingi tumekuwa waoga wa ushindani, kila kitu tunaogopa tutapigwa, tumelala wakati fursa zimejaa kila kona, tuamke tukimbizane na dunia, nimebahatika kutembea hii Nchi karibu mikoa yote ya Tanzania, hakuna mkoa usio na utajiri, lakini angalia watu wake, unachoka kabisa jinsi walivyo maskini, wakati majirani wakija ndani ya muda mfupi tu wanatengeneza hela ya hatari.

Nimalizie kwa kutoa mfano mmoja wa sekta ya madini, Wazawa kwenye eneo la madini tumelala sana, kuna wakati niilikuwa maeneo ya Isimani, nikatembezwa porini milimani ndani ndani kabisa nikiambiwa kuna madini, kweli niliwakuta vijana wanafanya kazi ya uchimbaji na wanapata, kuna dhahabu na vito vya kuvuna miaka na miaka, nani wa kwenda, hakuna! vijana wapo kwenye keyboard wanalalamika Wakenya watatuzidi, jamani tuamke kama ni kuzidiwa wakenya walishatuzidi sana tu, cha msingi tujifunze kutoka kwao.

Namuunga mkono Rais kuwakaribisha Wakenya au yoyote yule, cha msingi sheria zifuatwe.
 
Hivi akisema waje ina maana anawaita kiholela au wakija kuna utaratibu unafuatwa, kenyatta kasema tukafanye biashara bila permit ila sidhani kama amemaanisha wamachinga wakaje Nairobi, sheria itakayotumika kuwabana Australia, Marekani,China na yyt yule itawabana na Wakenya pia.

Ninachikiona mimi ni kwamba Watanzania kwa miaka mingi tumekuwa waoga wa ushindani, kila kitu tunaogopa tutapigwa, tumelala wakati fursa zimejaa kila kona, tuamke tukimbizane na dunia, nimebahatika kutembea hii Nchi karibu mikoa yote ya Tanzania, hakuna mkoa usio na utajiri, lakini angalia watu wake, unachoka kabisa jinsi walivyo maskini, wakati majirani wakija ndani ya muda mfupi tu wanatengeneza hela ya hatari.

Nimalizie kwa kutoa mfano mmoja wa sekta ya madini, Wazawa kwenye eneo la madini tumelala sana, kuna wakati niilikuwa maeneo ya Isimani, nikatembezwa porini milimani ndani ndani kabisa nikiambiwa kuna madini, kweli niliwakuta vijana wanafanya kazi ya uchimbaji na wanapata, kuna dhahabu na vito vya kuvuna miaka na miaka, nani wa kwenda, hakuna! vijana wapo kwenye keyboard wanalalamika Wakenya watatuzidi, jamani tuamke kama ni kuzidiwa wakenya walishatuzidi sana tu, cha msingi tujifunze kutoka kwao.

Namuunga mkono Rais kuwakaribisha Wakenya au yoyote yule, cha msingi sheria zifuatwe.
Kupata work permit Kenya inaweza kukuchukua miaka 2 na pengine zaidi, labda utoe rushwa
 
Mama amesena wanaofikiri Kenya na TZ wanapaswa kusigana kila Siku hao wana roho ya kimaskini, vision finyu na wana akili mbovu.

Nakubaliana naye 100% ,tuchape kazi tuache kulalamika, Mbona wachina wamejaza bidhaa zao hapa hatuwaoni maadui?

Tujiulize Kwann wawekezaji wa nje na ndani wanapenda kuajiri wakenya kuliko sisi?tujirekebishe ule upuuzi wa Jiwe wa kutaka kututenga Kama Korea kaskazini hauwezi kutusaidia kwenye ulimwengu wa kibepari
 
We Mtu zamani nilikuwa nakuona wa maana sana lakini tangu uje na utopolo wako wa kujaribu kunichafua, na ukaangukia pua, nimekuona mbabaishaji flani.

Kuna genge la waganga njaa mliokuwa mnanufaika na siasa za chuki. Mlipata fedha za mabeberu kwa jina la kupigania demokrasia. Sasa Mama Samia anapita mlemle mlikukua mnatumia kupatia fedha, mnatweta. Sooner than later mtaishia kutengwa na jamii, kwa sababu itabainika kuwa tatizo lenu si uongozi wa Mama Samia bali maslahi yenu binafsi.

Wenye akili hubadilika kuendana na wakati. Yes, CCM ni ileile lakini it's the person at the helm who really matters, na so far, Mama Samia ameonyesha mwelekeo mzuri.
 
Mleta mada ulitakaje?
Ulitaka Mama asiwakaribishe wakenya kuwekeza kwenye madini? Akiwekeza mchina au mmarekani ndio atatuonea huruma?

Ulitaka wakenya wasije Tanzania kuwekeza kwenye maelfu ya ardhi yetu ambayo hatuitumii ipasavyo?

Kwani sheria zetu hapa Tanzania zinabagua wawekezaji kwa misingi ya utaifa wao?

Ukweli ambao unaopaswa kuufahamu ni huu.
1. Wawekezaji wengi wa ndani na nje ya tanzania (hususani wakenya) walikimbia kuwekeza hapa Tanzania kipindi cha Magufuli. Sio rahisi tena kurejea, na njia rahisi ni Rais wa sasa kupiga promo ili warejee. Na wawekezaji wa kweli na uhakika wa nje ni wakenya, wanaijua vyema Tanzania na rahisi mnoo kufanya biashara na watanzania.

2. Kenya ni miongoni mwa wawekezaji wakuu hapa Tanzania tokea tunapata uhuru. Tanzania haiwezi kuikwepa Kenya daima. Lazima ufanye lobbying ya kuwavutia waje Tanzania. Wakenya wanaitamani ardhi yetu na madini yetu. Washawishi waje wawekeze.

3. Serikali ya Tanzania kwa sasa ina ukata mkubwa na i(natabiriwa ukata utaongezeka zaidi), mapato yameshuka, ukuaji wa uchumi umedorora, madeni yameongezeka, uwekezaji umeporoka na matumizi ya serikali yameongezeka maradufu. Jawabu la kiuchumi ni moja tu, watu waje kuwekeza tena hapa nchini ili pesa ije mtaani na serikali ikusanye kodi.

4. Mama anapambana kurejesha imani iliyokuwa imepotea baina ya Tanzania na wahisani, majirani na mabeberu. Ameanza ziara na majirani (Kenya, Uganda na wakati wowote atakwenda DRC, Rwanda au Zambia), anafanya mazungumzo na wahisani (WB, IMF, European union, US). Hana ujanja, serikali ina njaa kali.
 
Msomeni malisa mtaelewa

Mama ana akili kubwa hadi MATAGA wanashindwa kumuelewa. Mbuga ya Massai Mara (Kenya) na Serengeti (TZ) ni moja. Mpaka unaotenganisha nchi hizi umepita katikati ya mbuga. Lakini wanyama hawajui habari za mipaka. Wanavuka kwenda Kenya na baadae wanarudi Tanzania. Ni ikolojia ya kawaida.

Sasa kama wanyama ni ndugu, sisi ni nani tushindwe na wanyama? Undugu wetu na Kenya sio wa hiyari ni wa asili. Kama sio wakoloni kutuwekea mipaka wachagga, wakamba na wataita wangekua jamii moja. Wakurya wa TZ na Kurya Kenya wangekua jamii moja, Wajaluo wa TZ na Jaluo wa Kenya wangekua jamii moja, Wamassai wa TZ na Maasai wa Kenya wangekua jamii moja.

Wamakonde wa TZ na "Ntwala" wa Msumbiji wangekua jamii moja. Waha wa Kigoma na Watwa wa Burundi wangekua jamii moja. Wanyambo wa TZ na Watutsi wa Rwanda wangekua jamii moja. Wanyakyusa wa Mbeya na Wabemba wa Zambia wangekua jamii moja. Wahaya wa Bukoba na Waganda wangekua jamii moja.

Hatukuchagua kuwa ndugu, nature ndiyo iliyotuamulia. Sasa kwanini kuchukiana? Kwanini kujimwambafai? Kwanini uchome vifaranga vya ndugu yako kisa tu havijalipiwa kodi? Yani vifaranga havina ugonjwa wowote, isipokua vimeingizwa bila kulipiwa kodi unavichoma? Si ungevitaifisha uwape watu wafuge?

Kwanini ukamate mifugo ya ndugu yako uipige mnada eti kisa imeingia kwako bila taarifa? Ulitaka ipige hodi? Ulitaka iombe kuja kula nyasi kwako?" Chuki buana. Halafu kwanini useme ndugu yako anatumiwa na mabeberu kukuhujumu? Kama mabeberu wangetaka kukuhujumu kwanini wamtumie ndugu yako? Si wangekuja direct kama walivyoenda Libya, Iraq etc. Unadhani wangeshindwa?

Anyway, napenda kukujulisha tu kwamba sasa tunaanza upyaaaa (kwa sauti ya Mbunge Bwege). Kama unachukia huko ulipo upasuke tu, lakini undugu wetu tutauenzi, maana umewekwa na Mungu mwenyewe. Tutaishi kwa amani na upendo maana sisi ni ndugu wa damu. Ukichukia pasuka tena.!
GJ Malisa
 
Mama amesena wanaofikiri Kenya na TZ wanapaswa kusigana kila Siku hao wana roho ya kimaskini, vision finyu na wana akili mbovu.

Nakubaliana naye 100% ,tuchape kazi tuache kulalamika, Mbona wachina wamejaza bidhaa zao hapa hatuwaoni maadui?

Tujiulize Kwann wawekezaji wa nje na ndani wanapenda kuajiri wakenya kuliko sisi?tujirekebishe ule upuuzi wa Jiwe wa kutaka kututenga Kama Korea kaskazini hauwezi kutusaidia kwenye ulimwengu wa kibepari
100% Nakubaliana na wewe Chief, sisi ni wavivu mimi kuna jamaa namfahamu ni Mtanzania, miaka kadhaa nyuma alikuwa anafanya kazi kwenye moja ya makampuni ya simu, alikuwa anapenda sana kuwainua Watanzania wenzake kwa kuwapa kazi za designing, printing, branding nk, lakini sasa mpaka aje kukabidhiwa hiyo kazi, atafuatilia mpaka kero, mwisho wa siku anawapa Wakenya au Wahindi, fasta anapata kazi yake kwa wakati.
 
Aisee sasa sisi mnyonge wenu ni nani dunia hii.

Sikujua kama tunawaogopa wakenya kwa kiwango hiki??
 
Sio mbaya kumpa madam President na Wakenya the "benefit of the doubt" kwa maana labda bunge la Kenya watabadilisha sheria zao ili Watanzania waweze kufanya biashara "faster" bila vikwazo.

Leo Rostam Aziz ameweka wazi kupigwa sound kwa miaka minne (2017-21) licha ya kuonana na Rais Uhuru Kenyatta na akapewa baraka zote za kuwekeza Kenya kwenye gas kwa mtaji wa USD 30 mil (sawia na TZS 69.57 bn)

Rostam Aziz ana makampuni makubwa yafuatayo
  • Shareholding in Vodacom Tanzania, the leading mobile telephone network in the country, a subsidiary of Vodafone.
  • Caspian Limited, the largest contract mining company in Tanzania. Mining contractor to DeBeers, Barrick Gold
  • Ownership of the port of Dar es Salaam, in partnership with Hutchison Wampoa
  • Wembere Hunting Safaris Limited
  • Africa Tanneries Limited
  • Tanzania Leather Industries Limited
Tunapoenda mbele kwa ahadi nzuri za madam President baada ya kupata fursa ya kuhutubua mabunge mawili ya Kenya, ni lazima tukumbuke yafuatayo;
Kenya wamewahi kutaka kufanya smuggling ya vifaranga, vilipokamatwa na kupigwa moto, walilalama kana kwamba ilikuwa ni sawa kuvunja sheria kwa kuingiza viranga bila kufuata taratibu za kisheria na wao wanajua ni nini cha kufanya upaoingiza mifugo.

Kenya walifanya ukora kwa kupora mali za jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya jumuia kuvunjika. Hata ndoa huwa zinavunjia, Jeff Bezoz na Mckenzie Scott wameachana na kugawana mali. Hata Barclays na ABSA waliwahi ku-merge biashara na baadae wakagawana kila mmoja chake. Kuna na mbia anaejinasibu kama ndugu ila moyoni ni mkora, hapa iko haja kuingia nao kwa tahadhari sawia na JK alivyowahi kutuasa, akili za kuambiwa, changanya na zako.

Ni hawahawa Kenya wakiongoza kundi la "coalition of the willing"; kama udugu wanaotaka uwe wa kweli na wenye equity, ilitakiwa suala la kuwa na vitambulisho vya kitaifa kama hati ya kuingia nchi yoyote na kupiga mishe zozote, ilitakiwa JK alipowataka watupe muda, wangetuelewa. Uhuru alikuwepo wakati huo wa hizo "mishe mishe" za umoja wa walio tayari.

Kenya wanavyojinasibu kama ndugu, wanajua tulikuwa tunapoteza mapato mengi ya kikodi kutokana na smuggling ya Tanzanite kupitia Kenya. Unapokuwa na jirani anajinasibu ni ndugu, na anaona unabiwa mali zako na hakuwahi kukusaidia kukamata mwizi, na yeye kufaidika na huo wizi, huyo ndugu kuna haja ya kuwa na tahadhari nae kama kweli ni ndugu wa kweli.

Nihitimishe kwa kusema, tusubiri kuona kama kweli sheria zao zitabadilika na kama kweli sense of humanity na civilization wataionesha kuwajibika ikiwamo kubadili sheria zao na kuwa na equitable treatment kati yetu Tanzania na wao wenyeji pale tukienda kwao.

Ifahamike, kuna Wakenya wengi sana tumewapa fursa za kununua vitunguu mpaka mashambani, jambo ambalo kwao isingewezekana, kuna Wakenya kibao wanakuja Chalinze kununua nanasi; Tanzania kuna wakenya kibao wamejificha tukiotoa hao wanaofahamika kama CEO wa kampuni tokea Kenya.

Hongera madam President kupata heshima ya kuhutubia mabunge ya Kenya, tuishi nao kwa akili sana hawa majirani ambao mioyo yao kihistoria ni watu wa ndimi mbili;

JMT, kazi iendelee. Zege halilali.
 
Back
Top Bottom