Rais Samia, unawajua Wakenya?

Rais Samia, unawajua Wakenya?

Kubali kuliwa ili ule kama vile Kaaba anavyonunuliwa kwa elf 20 yeye kesho akapata mlo.

Wewe lala ndani Mimi nitoke tuone nani atarudi na chochote jion

Business is all about risk.
Hivi 'Business' mmeigundua Kenya?

Mbona watu hamueleweki?

Haya yote ni maonyesho ya kimazingaombwe tu, subiri kitakachotokea kama utakiona!
 
Nimekaa na Kusoma pia na hawa Wakenya hawana Ujanja ( Usamjo ) huu mnaousemea hapa tena hakuna Watu ambao Tanzania imewatega pazuri na Wao pia kuingia Mtegoni Kwetu kama hawa Wakenya.

Kuhusu Ujasusi sidhani kama kuna Taifa hapa Afrika Mashariki linaogopeka na Idara yake ya Ujasusi iko vizuri na inajua inachokifanya dhidi ya Marafiki Maadui kama ya Tanzania ( namaanisha TISS ) na kidogo ungeniambia kuhusu Rwanda ningekuelewa kutokana na sababu kadhaa za Kimkakati walizokuwa nazo ila sitoziweka hadharani kwa sasa.
 
Muhimu kulinda interests....

Wenyewe wanasema "Sometimes you have to go to bed with people you would not share a table with", let us be firm and fair.
 
Mama amesena wanaofikiri Kenya na TZ wanapaswa kusigana kila Siku hao wana roho ya kimaskini, vision finyu na wana akili mbovu.
Hilo nalo tatizo. Asijefikiri kuwa Ikulu basi ana akili kuliko wengine.
 
Huyu mama ni kimeo sasa hivi ccm haina nguvu hata ya kuhoji wamebaki kusifu wapinzani nao wamelala huu mida ulikuwa wa kuonyesha udhaifu wa ccm ila wanamwangaria rais kama rais barala ya kumwangalia rais kama mtawala toka ccm
 
Wewe jamaa kusema ukweli, unapotosha jamii yako ya Tz.
Why? - Mimi natokea KE na sio mwanasiasa, in fact sipendi siasi, lakini hiyo point uliyoweka ati tunaitamani ardhi yenyu toka zamani, na tunainyemelea ili tuimiliki ju ya migodi, that's a gaddamn lie bro.

Sababu, hakuna venye Wakenya watakuja Tz kuchukua tu biashara hiyo bila rukhusu, vibali au hata kuzuiwa kabisa sababu ya sheria mlizonazo ju ya migodi, labda. Na hao mabeberu wote uliowataja hapo chini, ndio hatari kwa maendeleo ya nchi. Watakuja na pipi zao aka madolari, kuwaziba macho ili kuiba kimya kimya huku wakiwachekesha, mwisho wa siku, migodi ikikauka, hao kwao, walikokuendeleza kupitia nyie wagwana.

So usiseme ati KE tunatamani Tz, maybe kutamani kutembea lakini mengine yasiyo na msingi, unayajua wewe. Kila raia anapigania taifa lake, mambo ya ukoloni waachie Wachina. Mfano mzuri, SA, nchi iko chonjo ile, sasa wale jamaa wa Zimbabwe wanavyovuka border kiharamu haramu, serikali ya SA mbona haijawahi tuhumu nchi ya Zimbabwe kwa kutaka kuzomba ardhi na mali yao? Hiyo issue wana deal nayo, wenyewe, internally sababu ni wananchi na sio nchi wenye kulaumiwa.

Hiyo story ya kuoa Mkikuyu, hata hakuna aliyetaka kujua kabila mkuu. Ungesema tu, mkenya, hiyo point ingefika. Lakini venye chuki imekujaa dhidi ya wakikuyu, sijui walikufanyaje, unaona ulete ukabila hapa. Mambo yako ya ulioa kabila gani, hatuna haja nayo na hatutaki kujua mnaambiana nini kuhusu KE ndipo ifikie kutufananisha na Watusi.

Hapo umefeli sana. Leo news nacheki wadada wa Tz walioolewa KE, wanaongea na sijaskia mtu ata mmoja kutaja kabila la mumewe, wote ni "nimeolewa na mkenya" ama "mme wangu mkenya", sasa unashangaza kutangaza kabila la mkeo, ndio iweje vile?

"Pretend that you need them more, while your intention is to suck their blood"... Hii slogan mkuu sidhani ka kuna mtu mwenye akili timamu haijui na hajawahi itumia kwenye pita pita zake maishani. Sana sana makazini, ukiwa chini, lazma unyenyeke, ujifanye pumba, ila akilini uko na kitu ume target hapo kazini na huwezi kipata bila ya kuwa "mjanja-mjinga".

Sasa hapo kwa mama Mh. Suluhu kukutana na Mh. Uhuru, kila mtu ameenda akijua anavutia kwake, na ndio wajibu wao huo. So sioni mtu anayepigwa changa la macho na mwenzie hapo.

Kila rais, amekuja amejihami kiakili, wana usaidizi wa wataalamu wa mambo hayo, na wanataka mazuri kwa kila mwananchi wake. Sababu ukisema Rais Uhuru ni mjanja kuliko Mama Mh. Suluhu, huoni unamponda rais wenyu live?

Kila mmoja wetu alipewa akili ya kutumia kwenye maisha yetu ya kila siku. So ni wajibu wetu kuitumia vyema.

Kumbuka, hata hao mabeberu unaowasifia maana mko kwao, wao pia walitumia ujanja enzi hizo za ukoloni hadi wa leo pahali wamefika, wamejijenga vizuri katika kila Sector, hiyo yote ni ujanja, hakuna ujinga uliotumika hapo.

So, it's up to each and every individual member of both countries to decide,whether they'll make use of any chance given to them to expand economically and socially or they'll continue throwing endless trush, that'll take nobody nowhere in this life.
Think about that! 🇰🇪 🇹🇿
 
Nimeandika Uzi humu ndani watu wakatoka mapovu.

Yaani Matatizo waliyotaka wenyewe waje kusaidiwa huku, nilishangaa Rais aliposema Tanzania ina Ardhi anawakaribisha Wakenya, Akanichosha aliposema Tanzania ina madini wakenya waje, utadhani watu hatuijui Kenya.

Hivi Wakenya wangapi watakuja Tanzania kuwekeza Madini Tanzania tusiwaite wachimbaji wadogowadogo,
Pasipo maono taifa huangamia.
 
Kwanini uchome vifaranga vya ndugu yako kisa tu havijalipiwa kodi? Yani vifaranga havina ugonjwa wowote, isipokua vimeingizwa bila kulipiwa kodi unavichoma? Si ungevitaifisha uwape watu wafuge?
Siamini kama Malissa anaweza kuandika maeleozo niliyo nukuu!!!
Kwamba hajui utaratibu wa kuzuwia magonjwa ya mifugo na mimea kwa kupitia taratibu flani za wizara ya kilimo na mifugo?
Mwandishi mkubwa kama yeye hajui nchi kam Australia na Uingereza si rahisi kuingiza hata kifaranga mmoja wa kuku au mche mmoja tu wa mmea wowote?

Kwanini asiende kwenye tovuti ya wizara husika aone zile fomu za kujaza na uhakiki wa chanjo zinazo stahili, uhakiki wa mbegu unayo leta isiharibu mbegu zetu za wanyama na mimea?
 
Mkuu, kenya ni Hatari sana, yaani hatutakubali eti waje washike vitalu vya madini, yaani hawa tukiwaruhusu Watanzania watabaki maskini wa kutupwa
Karma itawaandama Kama mnavyowafanyia Wazanzibari Nanyi mtafanyiwa hivyo hivyo
 
Nina mashaka na Uwezo wa kuamua wa Rais wangu, au kuna kundi linalonunulika linamshauri, yaani kikubwa ambacho Kenya itaifanyia Tanzania ni kuruhusu Mahindi, alafu sisi tutaruhusu Masuala ya Anga, Utalii.

Wao Wanazuia Shirika letu la ndege kufanya Kazi,ila lao wanataka tulihusu, Eti Mtalii afike Kenya ndio aje Tanzania, Kwa nini asianze Tanzania

Mama alipaswa amuache Kabudi kwenye wizara ya mambo ya nje aisee,
Mliyowafanyia Wazanzibari yatawarudia wenyewe, Karma inaanza kujibu
 
Uzi wako ni Mzuri isipokuwa hautoi solutions za muda mrefu zaidi kutuogopesha tu kwasasa. Ni lazima tupambane tuwe Kama wenzetu. Bora mkoloni toka Kenya kuliko mkoloni huyu Musukuma na mwenzake Magufuli
 
Embu tuwaze tu kirahisi, leo hii makampuni zaidi ya 500 ya wakenya yaliyowekeza hapa Tanzania yakaamua kufunga shughuli zao na kurejesha mitaji yao Kenya, nini kitatokea kwetu sisi watanzania?

Baadhi ya watanzania wanaumia sana kuona wakenya wakifaidika na rasilimali zetu, lakini wanasahau kuwa hao wakenya wametumia fursa zilizowekwa wazi, wakawekeza pesa, muda, akili na nguvu zao zote hapa Tanzania kihalali ili kuvuna faida.
 
Back
Top Bottom