Rais Samia, unawajua Wakenya?

Rais Samia, unawajua Wakenya?

wakenya sio watu poa kbsa kwanza ni wabinafsi , wajuaji na wana figisu sana na kama watawekeza tanzania hawana tofauti na wachina maana kwenye maslahi pia wanajijali wao kama wao kwanza, suala la hujuma pia wako vizuri mbona mifano ipo mingi tu yaani ni bora kufanya kazi na watu wa uganda kuliko wakenya
Akili hizi, Kenya ndio wanaongoza kwa uwezaji hapa Tanzania kwa Bara la Africa, hao unaowaita wabinafsi, na ni wa 5 kwa dunia, zaidi ya 1.7b usd wamekeza.
 
Sio mbaya kumpa madam President na Wakenya the "benefit of the doubt" kwa maana labda bunge la Kenya watabadilisha sheria zao ili Watanzania waweze kufanya biashara "faster" bila vikwazo.

Leo Rostam Aziz ameweka wazi kupigwa sound kwa miaka minne (2017-21) licha ya kuonana na Rais Uhuru Kenyatta na akapewa baraka zote za kuwekeza Kenya kwenye gas kwa mtaji wa USD 30 mil (sawia na TZS 69.57 bn)

Rostam Aziz ana makampuni makubwa yafuatayo
  • Shareholding in Vodacom Tanzania, the leading mobile telephone network in the country, a subsidiary of Vodafone.
  • Caspian Limited, the largest contract mining company in Tanzania. Mining contractor to DeBeers, Barrick Gold
  • Ownership of the port of Dar es Salaam, in partnership with Hutchison Wampoa
  • Wembere Hunting Safaris Limited
  • Africa Tanneries Limited
  • Tanzania Leather Industries Limited
Tunapoenda mbele kwa ahadi nzuri za madam President baada ya kupata fursa ya kuhutubua mabunge mawili ya Kenya, ni lazima tukumbuke yafuatayo;
Kenya wamewahi kutaka kufanya smuggling ya vifaranga, vilipokamatwa na kupigwa moto, walilalama kana kwamba ilikuwa ni sawa kuvunja sheria kwa kuingiza viranga bila kufuata taratibu za kisheria na wao wanajua ni nini cha kufanya upaoingiza mifugo.

Kenya walifanya ukora kwa kupora mali za jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya jumuia kuvunjika. Hata ndoa huwa zinavunjia, Jeff Bezoz na Mckenzie Scott wameachana na kugawana mali. Hata Barclays na ABSA waliwahi ku-merge biashara na baadae wakagawana kila mmoja chake. Kuna na mbia anaejinasibu kama ndugu ila moyoni ni mkora, hapa iko haja kuingia nao kwa tahadhari sawia na JK alivyowahi kutuasa, akili za kuambiwa, changanya na zako.

Ni hawahawa Kenya wakiongoza kundi la "coalition of the willing"; kama udugu wanaotaka uwe wa kweli na wenye equity, ilitakiwa suala la kuwa na vitambulisho vya kitaifa kama hati ya kuingia nchi yoyote na kupiga mishe zozote, ilitakiwa JK alipowataka watupe muda, wangetuelewa. Uhuru alikuwepo wakati huo wa hizo "mishe mishe" za umoja wa walio tayari.

Kenya wanavyojinasibu kama ndugu, wanajua tulikuwa tunapoteza mapato mengi ya kikodi kutokana na smuggling ya Tanzanite kupitia Kenya. Unapokuwa na jirani anajinasibu ni ndugu, na anaona unabiwa mali zako na hakuwahi kukusaidia kukamata mwizi, na yeye kufaidika na huo wizi, huyo ndugu kuna haja ya kuwa na tahadhari nae kama kweli ni ndugu wa kweli.

Nihitimishe kwa kusema, tusubiri kuona kama kweli sheria zao zitabadilika na kama kweli sense of humanity na civilization wataionesha kuwajibika ikiwamo kubadili sheria zao na kuwa na equitable treatment kati yetu Tanzania na wao wenyeji pale tukienda kwao.

Ifahamike, kuna Wakenya wengi sana tumewapa fursa za kununua vitunguu mpaka mashambani, jambo ambalo kwao isingewezekana, kuna Wakenya kibao wanakuja Chalinze kununua nanasi; Tanzania kuna wakenya kibao wamejificha tukiotoa hao wanaofahamika kama CEO wa kampuni tokea Kenya.

Hongera madam President kupata heshima ya kuhutubia mabunge ya Kenya, tuishi nao kwa akili sana hawa majirani ambao mioyo yao kihistoria ni watu wa ndimi mbili;

JMT, kazi iendelee. Zege halilali.
Jirani akusaidie kuzuia mwizi kwako, mwizi anayeshirikiana na wanao Huyo jirani anaanzaje? Tanzanite haiwezi kuibiwa bila wa TZ wenyewe kubariki mkenya wacha afaidi mpaka tutakapo amka kweli. Tumelala sana bana nasi.
 
Hivi akisema waje ina maana anawaita kiholela au wakija kuna utaratibu unafuatwa, kenyatta kasema tukafanye biashara bila permit ila sidhani kama amemaanisha wamachinga wakaje Nairobi, sheria itakayotumika kuwabana Australia, Marekani,China na yyt yule itawabana na Wakenya pia.

Ninachikiona mimi ni kwamba Watanzania kwa miaka mingi tumekuwa waoga wa ushindani, kila kitu tunaogopa tutapigwa, tumelala wakati fursa zimejaa kila kona, tuamke tukimbizane na dunia, nimebahatika kutembea hii Nchi karibu mikoa yote ya Tanzania, hakuna mkoa usio na utajiri, lakini angalia watu wake, unachoka kabisa jinsi walivyo maskini, wakati majirani wakija ndani ya muda mfupi tu wanatengeneza hela ya hatari.

Nimalizie kwa kutoa mfano mmoja wa sekta ya madini, Wazawa kwenye eneo la madini tumelala sana, kuna wakati niilikuwa maeneo ya Isimani, nikatembezwa porini milimani ndani ndani kabisa nikiambiwa kuna madini, kweli niliwakuta vijana wanafanya kazi ya uchimbaji na wanapata, kuna dhahabu na vito vya kuvuna miaka na miaka, nani wa kwenda, hakuna! vijana wapo kwenye keyboard wanalalamika Wakenya watatuzidi, jamani tuamke kama ni kuzidiwa wakenya walishatuzidi sana tu, cha msingi tujifunze kutoka kwao.

Namuunga mkono Rais kuwakaribisha Wakenya au yoyote yule, cha msingi sheria zifuatwe.
Hakuna nchi duniani, isiyojali raia wake kisa kuwekeza. Mataifa makubwa uangalia kuwapa uwezo raia wake wawekeze. Hakuna nchi iliyoendelea kwa uwekezaji toka nje. Si mara ya kwanza Kenya kuwekeza. Angalia miradi walio wekeza mfano kiwanda cha maziwa Arusha. Maziwa yanachukuliwa na wanaandika made in Kenya. Parking inafanyika Kenya. Kisha wanarudi kutuuzia.
Wameuwa general tyre. Kuna Insurance agency moja. Miaka ya nyuma kuanzia mkurungezi hadi karani walikuwa wakenya. Na huyu boss alikuwa rafiki yangu. Wote walofanya kazi walikuwa wakikuyu. Wanaukabila sana.
Nilishuhudia balozi wa Kenya waki lobby na kuongea na wafanya biashara kutumia bandari ya Mombasa bila balozi kutoa taarifa kuwa atakuwa na maongezi sehemu fulani ktk mkoa husika. Wakenya ni wajanja sana.
Mara ngapi wameingiza watalii wengi ktk mbuga na mlima kilimanjaro. Miaka fulani nimekutana na watalii wakanambia walipanda mlima Kilimanjaro kupitia Kenya na kutembelea Serengeti.
Tulipoteza kodi kiasi gani na hao wakenya wenu. Uwezi fungulia milango kiasi hicho. Kikubwa nchi yetu iangalie kuwawezesha wananchi waweze wekeza ndani. Hii inawezekana.
Angalia nchi ilovunja umoja wa Afrika Mashariki ilikuwa Kenya kwa tamaa zao. Wakakatalia baadhi ya mali za Afrika mashariki. Kenya inajua Tanzania ndo mshindani wake. Hivyo hawatatupenda toka moyoni. Sikatai uwekezaji lakini tuwe makini. Uwezi mfurahisha kila mtu. Wakenya si mara ya kwanza kuwa na tofauti. Tumekuwa nao tofauti toka kipindi cha Nyerere. Kuna wakati tulikuwa na vita ya maneno. Hadi kuitana Nyang'au. Tulikuwa na vita ya maneno na Malawi hao wote jirani. Uwezi kumchekea kila jirani ati diplomasia. Uchumi wa kidiplomasia si kuchekeana. Angalia Marekani na China.
 
Utaitwa sukuma gang sasa ivi na vijana wa bongo flava 😂😂
 
Msomeni malisa mtaelewa

Mama ana akili kubwa hadi MATAGA wanashindwa kumuelewa. Mbuga ya Massai Mara (Kenya) na Serengeti (TZ) ni moja. Mpaka unaotenganisha nchi hizi umepita katikati ya mbuga. Lakini wanyama hawajui habari za mipaka. Wanavuka kwenda Kenya na baadae wanarudi Tanzania. Ni ikolojia ya kawaida.

Sasa kama wanyama ni ndugu, sisi ni nani tushindwe na wanyama? Undugu wetu na Kenya sio wa hiyari ni wa asili. Kama sio wakoloni kutuwekea mipaka wachagga, wakamba na wataita wangekua jamii moja. Wakurya wa TZ na Kurya Kenya wangekua jamii moja, Wajaluo wa TZ na Jaluo wa Kenya wangekua jamii moja, Wamassai wa TZ na Maasai wa Kenya wangekua jamii moja.

Wamakonde wa TZ na "Ntwala" wa Msumbiji wangekua jamii moja. Waha wa Kigoma na Watwa wa Burundi wangekua jamii moja. Wanyambo wa TZ na Watutsi wa Rwanda wangekua jamii moja. Wanyakyusa wa Mbeya na Wabemba wa Zambia wangekua jamii moja. Wahaya wa Bukoba na Waganda wangekua jamii moja.

Hatukuchagua kuwa ndugu, nature ndiyo iliyotuamulia. Sasa kwanini kuchukiana? Kwanini kujimwambafai? Kwanini uchome vifaranga vya ndugu yako kisa tu havijalipiwa kodi? Yani vifaranga havina ugonjwa wowote, isipokua vimeingizwa bila kulipiwa kodi unavichoma? Si ungevitaifisha uwape watu wafuge?

Kwanini ukamate mifugo ya ndugu yako uipige mnada eti kisa imeingia kwako bila taarifa? Ulitaka ipige hodi? Ulitaka iombe kuja kula nyasi kwako?" Chuki buana. Halafu kwanini useme ndugu yako anatumiwa na mabeberu kukuhujumu? Kama mabeberu wangetaka kukuhujumu kwanini wamtumie ndugu yako? Si wangekuja direct kama walivyoenda Libya, Iraq etc. Unadhani wangeshindwa?

Anyway, napenda kukujulisha tu kwamba sasa tunaanza upyaaaa (kwa sauti ya Mbunge Bwege). Kama unachukia huko ulipo upasuke tu, lakini undugu wetu tutauenzi, maana umewekwa na Mungu mwenyewe. Tutaishi kwa amani na upendo maana sisi ni ndugu wa damu. Ukichukia pasuka tena.!
GJ Malisa
Sasa Malisa ana akili kweli?

Kama hayo akiyosema anaona ndio maslahi unategemea nini?

Mtu anaewaza mataga kukomolewa unafikiri ana akili tena huyo?
 
Iko hivi kwa taarifa yako Wasukuma ndio wanaogoza kuwekeza kwenye migodi ya Kenya au unafikiri Kenya hakuna migodi?

Kuanzia Migori hapo kwenda mpaka kisumu kuna migodi kibao na wakazi wa huko ni wasukuma na wajaluo.

Sasa wewe sijui unataka wawekezaji kutoka wapi ndio waje wawekeze na mchanga wabebe

Hii nchi watu tunashindwa kujua kitu tunachokitaka..

Kwenye swala la uwekezaji na kukuza uchumi niko na mama.

Ila tutagombana kwenye democracy na ufisadi na katiba mpya.

Ni WaTz wangapi wanakula na kushiba democracy na katiba mpya kama siyo hao wachache wanaotaka madaraka?

Hushangai wanaanza kumpamba Mama kwa lugha yenye kila pambio?

Ukiona adui anajipendekeza kwako ujue umenasa.
 
Hivi akisema waje ina maana anawaita kiholela au wakija kuna utaratibu unafuatwa, kenyatta kasema tukafanye biashara bila permit ila sidhani kama amemaanisha wamachinga wakaje Nairobi, sheria itakayotumika kuwabana Australia, Marekani,China na yyt yule itawabana na Wakenya pia.

Ninachikiona mimi ni kwamba Watanzania kwa miaka mingi tumekuwa waoga wa ushindani, kila kitu tunaogopa tutapigwa, tumelala wakati fursa zimejaa kila kona, tuamke tukimbizane na dunia, nimebahatika kutembea hii Nchi karibu mikoa yote ya Tanzania, hakuna mkoa usio na utajiri, lakini angalia watu wake, unachoka kabisa jinsi walivyo maskini, wakati majirani wakija ndani ya muda mfupi tu wanatengeneza hela ya hatari.

Nimalizie kwa kutoa mfano mmoja wa sekta ya madini, Wazawa kwenye eneo la madini tumelala sana, kuna wakati niilikuwa maeneo ya Isimani, nikatembezwa porini milimani ndani ndani kabisa nikiambiwa kuna madini, kweli niliwakuta vijana wanafanya kazi ya uchimbaji na wanapata, kuna dhahabu na vito vya kuvuna miaka na miaka, nani wa kwenda, hakuna! vijana wapo kwenye keyboard wanalalamika Wakenya watatuzidi, jamani tuamke kama ni kuzidiwa wakenya walishatuzidi sana tu, cha msingi tujifunze kutoka kwao.

Namuunga mkono Rais kuwakaribisha Wakenya au yoyote yule, cha msingi sheria zifuatwe.
Wewe wasema nchi ni tajiri, hivyo hutofautiani na Rais aliyesema WaTz hawana mitaji ya kuwekeza kwenye ardhi na madini. Ila kumbuka Hayati alisisitiza nchi ni tajiri akaanza kujenga mazingira ya kuwawezesha WaTz kuwa mabilionea.

Kwa kufungua milango wazi ya uwekezaji, hata kwenye rasmali za nchi (ardhi, madini, mbuga za wanyama, nk - ndio utajiri wenyewe) ndoto hiyo ya hayati inayeyuka.
 
Mtanzania katika ubora wake wa kuishi na uoga na wasiwasi usio na sababu.

Tukumbuke kuwa mahindi yetu yamepatiwa ruhusa ya kuingia Kenya baada ya kukaa pale mpakani kwa miezi kadhaa.

Kenyatta katoa agizo mzigo uingizwe, Kenya ni soko la uhakika la mazao ya chakula.

Mzigo ungekwama maana yake huu unaoendelea kulimwa ungekosa pia soko. Umaskini kwa mkulima ungeendelea kuwepo na kukata tamaa kungefuatia.

Diplomasia ni muhimu sana na ni silaha ya mdomo kuliko ile hatari yenye kuambatana na watu kubeba bunduki.

Mama Liberata kapewa mambo ya nje na mojawapo ya kazi zake ni hii ziara ya Kenya.

Jirani yako huwezi kumkwepa cha muhimu ni kutafuta maarifa ya kuishi nae.
 
Wewe wasema nchi ni tajiri, hivyo hutofautiani na Rais aliyesema WaTz hawana mitaji ya kuwekeza kwenye ardhi na madini. Ila kumbuka Hayati alisisitiza nchi ni tajiri akaanza kujenga mazingira ya kuwawezesha WaTz kuwa mabilionea.

Kwa kufungua milango wazi ya uwekezaji, hata kwenye rasmali za nchi (ardhi, madini, mbuga za wanyama, nk - ndio utajiri wenyewe) ndoto hiyo ya hayati inayeyuka.
Hayati huyo huyo alisema kuwa hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu peke yetu.

Alisema maneno hayo mbele ya viongozi wa sekta ya madini na viongozi wa dini.

Hatuwezi kuishi kama visiwa, tunawategemea wa nje na wa nje wanatutegemea sisi.
 
Sababu, hakuna venye Wakenya watakuja Tz kuchukua tu biashara hiyo bila rukhusu, vibali au hata kuzuiwa kabisa sababu ya sheria mlizonazo ju ya migodi,
Tatizo lenu mna janja janja nyingi sana.

Unakumbuka kipindi cha nyuma Kenya ilikuwa inaongoza kwa kuuza tanzanite, vipi mna machimbo ya hayo madini huko kwenu?

Tunataka kufanya biashara na nyie ila kwa umakini wa hali ya juu...sio kwa ulegevu aliouonyesha mama.
 
Tunatengeneza reli hadi ili kumfaidisha kale kajamaa kamodo kaswahiba ka Shujaa halafu hata kwenye msiba hakuja 😀😀😀😀

Ila tuachage upumbavu Watanzania kwa hiyo Wakenya wakiingia TZ watachukua ardhi? Kwani sheria ya umiliki wa ardhi ipoje? Kenyatta mwenyewe mbali ya kuturuhusu kwenda Kenya lakini kasisitiza lazima iwe kwa vigezo vya kisheria vya Kenya. Tuache hizi mindset za kijamaa za miaka ya 70 zilizokua zinapigiwa chapuo na jiwe, tutalalamika milele tu. Tubadilike aisee

NB: Heko kwa Mwendazake mama anajimwambafy angani na kaka yake Bombardier aka Airbus, kitu kimenunuliwa kwa Cash
 
Mama anafanya kazi nzuri Sana, huu ulioweka hapa ni uchochezi.
Chapeni kazi achana na propaganda
#nipo na mama# kazi iendelee#
Enzi ya nyerere walivunja muungano, enzi ya kikwete walimuona si chochote na kijfanya wanajitenga kufanya yao, enzi ya magufuli kila siku wanafunga mipaka mara wazuia magari mara vyakula bila sababu
Unategemea kwa samia wataheshimu kitu hawa?

Wao wametoa ofa ya kufanya biashara na kazi bila vibali kuwatega, kisha nyie nao mjichanganye muone.

Kenya wewe utawekeza wapi kama kila sehemu zinamilikiwa na watu,
Je nyie watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kenya mpo wangapi?
Na matawekeza kwenye nini?

Tanzania kila sehemu tuna vitu vya kuwekeza kuanzia madini ardhi maziwa na mito, kisha wawekeze na nwao watake wafanyakazi wao wapewe vibali vya kazi bila mashart uone kama mtanzania atapata kazi kwenye huo uwekezaji labda awe anatumika tu kwa maslahi yao,

Mtaingizwa force king kisha mnauliwa kweupe.
Wacheza draft wanajua.
 
Mijitu mingine hewa kabisa ,eti mama unaijua Kenya?, we kweli akili yako imekosa oil,hivi unafikiri samia ni kisoda kama wewe au aliamka tuu akajipodoa akaamsha popo kwenda Kenya , unafikiri anafanya maamuz kama wewe ulivyofanya maamuz ya kutupia huu Uzi bila kushirikisha halmashaur,bichwa kubwa akili ya kuku
 
Hayati huyo huyo alisema kuwa hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu peke yetu.

Alisema maneno hayo mbele ya viongozi wa sekta ya madini na viongozi wa dini.

Hatuwezi kuishi kama visiwa, tunawategemea wa nje na wa nje wanatutegemea sisi.
Hakika hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu pekee au kuishi kama kisiwa, lakini vile vile hatuwezi kushindana pasipo na mazingira yaliyo ya usawa na rafiki.
Enzi ya nyerere walivunja muungano, enzi ya kikwete walimuona si chochote na kijfanya wanajitenga kufanya yao, enzi ya magufuli kila siku wanafunga mipaka mara wazuia magari mara vyakula bila sababu
Unategemea kwa samia wataheshimu kitu hawa?

Wao wametoa ofa ya kufanya biashara na kazi bila vibali kuwatega, kisha nyie nao mjichanganye muone.

Kenya wewe utawekeza wapi kama kila sehemu zinamilikiwa na watu,
Je nyie watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kenya mpo wangapi?
Na matawekeza kwenye nini?

Tanzania kila sehemu tuna vitu vya kuwekeza kuanzia madini ardhi maziwa na mito, kisha wawekeze na nwao watake wafanyakazi wao wapewe vibali vya kazi bila mashart uone kama mtanzania atapata kazi kwenye huo uwekezaji labda awe anatumika tu kwa maslahi yao,

Mtaingizwa force king kisha mnauliwa kweupe.
Wacheza draft wanajua.
Ni jibu tosha la hoja yake Phillipo Bukililo, kwamba tuwe makini na Wakenya ambao hadi kesho wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani. Wayatendayo kwa jirani zao mipakani (Uganda, Tanzania, Somali) yanatosha kueleza jinsi walivyo. Isitoshe tuna majirani zaidi wa kufanya nao biashara kuliko Kenya.

Swali la kujiuliza ni kwa nini Uhuru ghafla alimwarika Rais SSH mara tu baada ya kuhutubia Bunge letu? [emoji848]
 
Marekani haina wafanyakazi wa Kigeni wa machinga, inachukua cream kutoka kwenye mataifa mengine.
Hizo "krimu" ni pande moja tu, wana mamilioni ya watu kutoka Meksiko, Amerika ya Kusini wanaovuna matunda kwenye mashamba kwa mishahara duni , kufanya kazi ya mtumishi wa nyumbani . . .. .
 
Rais wangu,na mama yangu Samia,kwanza nakupongeza sana kwa hatua uliyochukua ya kuanza kuboresha mahusiano ya kidiplomasia na Kenya kwa sababu yalianza kufa kimya kimya, yaani Tulikuwa na uhusiano wa kinafiki,ktk hili sina muda wa kulieleza kwa kina kwa sababu lipo wazi kabisa.

Rais wangu,Tasnia ya mahusiano ya Taifa na Taifa inahitaji akili nyingi sana,kwa sababu, ktk slogan ya kijasusi kila Taifa la jirani yako ni adui yako,kwa maana ya kwamba linaweza hata kutumika kukupiga na adui wa mbali.

Hii ina maana ya kwamba,tunakuwa majirani na ndugu tusioaminiana kwa kila kitu.

Ktk vinywa vyetu sisi ni marafiki wa kufa na kuzikana, ila ktk uhalisia sisi ni adui.
Rais wangu, Kenyatta ni Rais mwenye akili mno na mwingi wa hekima, kwa nje utamwona kawaida, lakini Kenyatta ni bonge la Intelligent.

Rais wangu, hakuna anayeweza kukueleza ukweli, kwa sababu Chama chenu kina slogan ya kusifia kila kitu, hiyo imefanya hadi idara ya usalama wa Taifa TISS,kuwa dhaifu kupindukia.

Rais wangu,hivi unajua kuwa, Kenya kwa miongo mingi mno iliyopita imekuwa ikiitamani sana ardhi ya Tanzania? Unaposema kuwa unawakaribisha Wakenya wawekeze kwenye madini,maana yake ni kwamba unawapa mwanya wa kumiliki ardhi ya Tanzania ili watimize ndoto zao,ktk hili hapana,waite Wa Australia,Wamarekani, Waingereza,Wa Canada, lakini siyo Kenya ktk sekta ya madini.

Wakenya na Wachina hawana Tofauti, mimi nimeolea kenya,mke wangu ni mkikuyu,Tulikutana Australia,na wala hajui kuwa jina langu fake ni "My son drink water",nawajua vizuri sana hawa watu,hawana Tofauti na Watusi, ukweli unauma ila hauna budi kusemwa.

Rais wangu, ziara yako Kenya ilikuwa ni ya manufaa ya Kenya na si Tanzania, Kenyatta alikuwa ameshafanya calculation nzuri sana, kitaalamu inaitwa,"Pretend that you need them more, while your intention is to suck their Blood".

Sikatai kwamba Wakenya wasiwekeze Tanzania, ila hawa watu ni wajanja kama nyoka.

Message sent and Delivered
Mkuu yani inauma sana.....kwenye madini hapo ndo kule tanzanite ya Tz lkn nchi inayoongiza kuuza ni keny,s.africa.....oh mara india....ujinga huu hauvumiliki kwa kweli
 
Mnaosema wakenya wabinafs , sijui wanakuja kuchukua madini haya tuoneshen taifa ambalo halina hizo sifa
 
Mkuu, kenya ni Hatari sana, yaani hatutakubali eti waje washike vitalu vya madini, yaani hawa tukiwaruhusu Watanzania watabaki maskini wa kutupwa
Ajira wazitajazo zitokanazo na uwekezaji ni politics tu and short consideration......tunaacha long run consideration....du very painful
 
Back
Top Bottom