Sio mbaya kumpa madam President na Wakenya the "benefit of the doubt" kwa maana labda bunge la Kenya watabadilisha sheria zao ili Watanzania waweze kufanya biashara "faster" bila vikwazo.
Leo Rostam Aziz ameweka wazi kupigwa sound kwa miaka minne (2017-21) licha ya kuonana na Rais Uhuru Kenyatta na akapewa baraka zote za kuwekeza Kenya kwenye gas kwa mtaji wa USD 30 mil (sawia na TZS 69.57 bn)
Rostam Aziz ana makampuni makubwa yafuatayo
- Shareholding in Vodacom Tanzania, the leading mobile telephone network in the country, a subsidiary of Vodafone.
- Caspian Limited, the largest contract mining company in Tanzania. Mining contractor to DeBeers, Barrick Gold
- Ownership of the port of Dar es Salaam, in partnership with Hutchison Wampoa
- Wembere Hunting Safaris Limited
- Africa Tanneries Limited
- Tanzania Leather Industries Limited
Tunapoenda mbele kwa ahadi nzuri za madam President baada ya kupata fursa ya kuhutubua mabunge mawili ya Kenya, ni lazima tukumbuke yafuatayo;
Kenya wamewahi kutaka kufanya smuggling ya vifaranga, vilipokamatwa na kupigwa moto, walilalama kana kwamba ilikuwa ni sawa kuvunja sheria kwa kuingiza viranga bila kufuata taratibu za kisheria na wao wanajua ni nini cha kufanya upaoingiza mifugo.
Kenya walifanya ukora kwa kupora mali za jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya jumuia kuvunjika. Hata ndoa huwa zinavunjia, Jeff Bezoz na Mckenzie Scott wameachana na kugawana mali. Hata Barclays na ABSA waliwahi ku-merge biashara na baadae wakagawana kila mmoja chake. Kuna na mbia anaejinasibu kama ndugu ila moyoni ni mkora, hapa iko haja kuingia nao kwa tahadhari sawia na JK alivyowahi kutuasa, akili za kuambiwa, changanya na zako.
Ni hawahawa Kenya wakiongoza kundi la "coalition of the willing"; kama udugu wanaotaka uwe wa kweli na wenye equity, ilitakiwa suala la kuwa na vitambulisho vya kitaifa kama hati ya kuingia nchi yoyote na kupiga mishe zozote, ilitakiwa JK alipowataka watupe muda, wangetuelewa. Uhuru alikuwepo wakati huo wa hizo "mishe mishe" za umoja wa walio tayari.
Kenya wanavyojinasibu kama ndugu, wanajua tulikuwa tunapoteza mapato mengi ya kikodi kutokana na smuggling ya Tanzanite kupitia Kenya. Unapokuwa na jirani anajinasibu ni ndugu, na anaona unabiwa mali zako na hakuwahi kukusaidia kukamata mwizi, na yeye kufaidika na huo wizi, huyo ndugu kuna haja ya kuwa na tahadhari nae kama kweli ni ndugu wa kweli.
Nihitimishe kwa kusema, tusubiri kuona kama kweli sheria zao zitabadilika na kama kweli sense of humanity na civilization wataionesha kuwajibika ikiwamo kubadili sheria zao na kuwa na equitable treatment kati yetu Tanzania na wao wenyeji pale tukienda kwao.
Ifahamike, kuna Wakenya wengi sana tumewapa fursa za kununua vitunguu mpaka mashambani, jambo ambalo kwao isingewezekana, kuna Wakenya kibao wanakuja Chalinze kununua nanasi; Tanzania kuna wakenya kibao wamejificha tukiotoa hao wanaofahamika kama CEO wa kampuni tokea Kenya.
Hongera madam President kupata heshima ya kuhutubia mabunge ya Kenya, tuishi nao kwa akili sana hawa majirani ambao mioyo yao kihistoria ni watu wa ndimi mbili;
JMT, kazi iendelee. Zege halilali.