Leo DCI ametoa taarifa aliyoiita kuwa ni matokeo ya uchunguzi.
Kwangu mimi, na nadhani kwa Watanzania walio wengi, Polisi hawakuwa taasisi sahihi ya kufanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Hamza dhidi ya polisi na pia kifo chake yeye mwenyewe Hamza.
Kwa nini?
Katika tukio la mauaji ya polisi na Hamza, kulikuwa na maelezo kuwa mauaji ya Hamza yalikuwa ya kulipiza kisasi dhidi ya polisi ambao kabla ya shambulio, walikuwa wamempora mali yake. Hii tayari ilikuwa ni tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa na uzito wa wazi kutokana na shambulio la Hamza kuwalenga polisi na siyo mauaji holela dhidi ya raia.
Hoja ya pili, kwetu tulio wengi, au hatuna imani au tuna imani ndogo kwa jeshi la polisi kutokana na historia ya jeshi hili. Miaka ya nyuma polisi waliwahi kupora pesa kutoka kwa wafanyabiashara wa madini, kisha wakawaua hao wafanyabiashara, tena wakaenda kuwaulia msituni.
Wakatengeneza kile walichokiita kamati ya uchunguzi, nayo ikaleta taarifa kuwa eti wale wafanyabiashara walikuwa majambazi, na walikufa kwa kupigwa risasi wakati wanakimbia kutoroka mkono wa dola.
Uchunguzi wa baadaye ulithibitisha kuwa polisi walifanya kazi kama genge la majambazi ambapo wapo waliowapora wafanyabiashara wale, wengine wakawaua, na wengine wakawalinda wahalifu wenzao kwa kutoa taarifa ya uwongo dhidi ya marehemu.
Tunataka kuujua ukweli, na ukweli hauwezi kutoka kwa mtuhumiwa. Polisi nao, kama wanataka kujisafisha na tuhuma hizi, nao wasisitize uchunguzi ufanywe na chombo kingine, kilicho huru.
Uchunguzi wa kitaalam, wa kina na ulio wa kweli ndio utakaolisababishia Taifa kuepuka matukio ya kutisha kama haya yaliyotokea hivi karibuni.
Mungu naomba uwajalie hekima watawala katika kufanya maamuzi yenye kulihakikishia amani ya kweli Taifa letu.